Majuto ya mnunuzi?

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,001
112,644
Nakumbuka waliimba kwa dharau, mikogo, majigambo, makeke, majivuno, na kila aina ya mbwembwe.

Wenyewe waliimba eti 'CCM mbele kwa mbele'
'Tumeipenda wenyewe, chaguo letu milele'
'Na wavimbe wapasuke, watajijua wenyewe'
'Acha waisome namba, watasoma namba'
'CCM mbele kwa mbele'
'CCM ni ile ile'



Lakini jambo lililo shani sasa hivi ni ukimya wao. Wamekuwa kete kabisa. Ngebe zimeisha. Hawapayuki payuki tena kama ilivyokuwa awali.

Ni kama vile fungate limeisha na sasa wamerudi katika uhalisia. Lakini pengine kuna la zaidi hapo.

Naona kuna kila dalili ya majuto ya ununuzi. Kwamba walichokipigia debe na mwishowe kukinunua sicho walichokidhania. Sasa wana 'buyer's remorse'.

Wanajuta lakini wanashindwa kusema na kukiri hadharani kuwa walikosea. Kwamba waliingizwa kingi na wao wakaingia kichwa kichwa bila kutafakari kwa umakini.

Hata humu wamepungua siku hizi. Wamebaki kuugulia kimya kimya tu. Hawana tena cha kutetea.

Huyo waliyempenda wenyewe kila afunguapo mdomo wake lazima aache wazi midomo ya wamsikilizao.

Ila wengine tulishasema humu kuwa huyo waliyempenda wenyewe ni bomu. Na wala haikuwa kazi ngumu kujua kuwa hata kabla ya kupendwa alikuwa ni bomu.

Sasa vilio vimejaa kila kona. Manung'uniko kila pembe. Na minong'ono ya kumtema ishaanza.

Hapa kazi tu imegeuka na kuwa hapa maumivu tu. Kila mtu anaisoma namba. Hata wale waloimba kuwa wenzao wataisoma namba nao wanaisoma namba. Labda wangeimba 'tutaisoma namba':D.

Majuto ya mnunuzi na majuto ni mjukuu.

Alamsiki.

NB: Uongo mbaya jamani...CCM mbele kwa mbele ni bonge la songi. KTMA tuzo vipi hapo?
 
Hebu waoneni hapa....they definitely were a sight to behold!

 
Yule aliyeweka mkata ngazi (January Makamba) ingawa alijitetea sana lakini ujumbe wake ulikuwa una maana sana kwa watanzania.
 
Huu uwimbo unaniburudisha sana . .walahi . .

Kusema ukweli ni bonge la ngoma.

Kuna siku nilipita pale Mwenye nikawaona wamama wa CCM wakiucheza....ebana ilibidi nipaki gari pembeni niwaangalie walivyokuwa wakinenguka.

Ilikuwa ni burudani kwelikweli.
 
Kusema ukweli ni bonge la ngoma.

Kuna siku nilipita pale Mwenye nikawaona wamama wa CCM wakiucheza....ebana ilibidi nipaki gari pembeni niwaangalie walivyokuwa wakinenguka.

Ilikuwa ni burudani kwelikweli.
Amen RA
 
Halafu walikuja kukosea walivyompa mpaka uenyekiti wa chama. Sasa hawana namna ya kumpunguza kasi hata pale anapowakanyaga wao wenyewe kwa style yake ya mwendo kasi.
 
Na hili liwe funzo. Siasa za upigaji zinatoweka kwa kasi kipindi hiki cha JPM.

Sasa hivi hutawasikia aisee. Hela za kugawana kwenye visandarusi kwishney!
 
Yeah.....maRC, DC, wakurugenzi nao wameanza kuisoma!:D:D
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom