Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,715
- 729,888
Kuna wakati lazima kiwepo chombo cha kumkumbusha rais majukumu yake.. yeye anabaki kuwa msimamizi mkuu wa sera serikali mahusiano ya kitaifa na kimataifa, na ndio maana kwa nafasi yake anakuwa ndie mwenyekiti wa baraza la mawaziri.
Utendaji wa siku kwa siku ni wa waziri mkuu sio wa rais.
Kufukuza/kusimamisha kazi ni jukumu la mwajiri au kupitia taratibu zilizopo lakini.
Kwasasa rais na mpaka watendaji wa chini kabisa kama wakuu wa wilaya wana nguvu ya kusimamisha watu kazi hata kwa makosa ya kutunga.
Sasa hivi rais ni waziri mkuu, waziri wa ujenzi waziri wa tamisemi waziri wa fedha....tunaenda wapi?
Kali zaidi ni ile ya Makonda kumuagiza Rais naye akakubali kuagizwa na Makonda kumfuta kazi Mkurugenzi wa jiji tena mahali pasipostahili?
Nani kasema Rais anaagizwa? Rais anashauriwa haagizwi.
Pamoja na dhamira safi ya kutetea wanyonge pamoja na uthubutu alionao kwenye kushughulikia mafisadi pamoja na uzalendo kwa taifa lake pamoja na ufahamu wake mkubwa kwenye mambo mengi hasa takwimu lakini hana subra wala tafakuri.
Hii ni hatari kubwa kwa mgawanyo wa madaraka na utawala wa sheria tunashangilia haya anayoyafanya kwasasa kutokana na nchi ilipokuwa imefikishwa na mtangulizi wake lakini ukweli ni kwamba katikati ya utendaji wake huu anatengeneza tatizo moja kubwa sana hasa yeye na Makonda wake
Bila kuambiwa mapema litakuja anguko kuu.