Majukumu ya Ofisi Ya Msajili wa Vyama vya Siasa

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,396
IJUE SHERIA YA VYAMA VYA SIASA:

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ana jukumu la kusimamia chaguzi za ndani za vyama vya siasa na kuhakikisha ziko huru na haki

Ofisi hiyo inapaswa kutuoa muongozo na taratibu za mapato na matumizi ya fedha ndani ya vyama vya siasa

Kutoa elimu kuhusu Demokrasia, sheria zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa

Kuishauri Serikali kuhusu mambo yote yanayohusiana na siasa vyama vya siasa pamoja na kuwezesha mawasiliano mazuri kati ya Vyama vya Siasa na Serikali

20191223_100148.jpg
20191223_100211.jpg

====
MAJUKUMU YA OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imejikita katika usimamizi wa Sheria ya Vyama vya Siasa Na 5 ya mwaka 1992 na Sheria ya Gharama za uchaguzi ya mwaka 2010 ili kuhakikisha uwepo na ukuaji wa demokrasia ya vyama vingi nchini

Majukumu ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ni kusajili chama cha siasa kinachokidhi vigezo vya usajili kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, ikiwamo kufuta chama chenye usajili wa muda au kudumu ambacho kwa mujibu wa sheria kimepoteza sifa ya usajili

Msajili amepewa mamlaka ya kusajili na kuvifuta vyama vinavyokiuka masharti ya usajili kwa mujibu wa sheria

Majukumu mengine ni kuratibu shughuli za Baraza la vyama vya siasa, kufuatilia mapato na matumizi ya vyama vya siasa katika uchaguzi kwa mujibu wa Sheria ya gharama za uchaguzi ya mwaka 2010

Kufuatilia utendaji wa vyama vya siasa kwa mujibu wa sheria, kugawa ruzuku kwa vyama vya siasa vyenye sifa, kuwa kiungo kati ya serikali na vyama vya siasa nchini. Pia, kutoa elimu kwa umma kwa vyama vya siasa na wadau wa vyama vya siasa

Kwa mujibu wa tovuti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, kuna vyama 19 vyenye usajili wa kudumu
 
IJUE SHERIA YA VYAMA VYA SIASA:

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ana jukumu la kusimamia chaguzi za ndani za vyama vya siasa na kuhakikisha ziko huru na haki

Ofisi hiyo inapaswa kutuoa muongozo na taratibu za mapato na matumizi ya fedha ndani ya vyama vya siasa

Kutoa elimu kuhusu Demokrasia, sheria zinazosimamiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa

Kuishauri Serikali kuhusu mambo yote yanayohusiana na siasa vyama vya siasa pamoja na kuwezesha mawasiliano mazuri kati ya Vyama vya Siasa na Serikali

View attachment 1300986View attachment 1300987
Ni kosa gani na kifungo kipi kinakuondolea sifa ya kugombea uongozi km urais,ubunge na udiwani? Hivi sheria mtu akihama chama mpaka akae miaka kadhaa agombee je tayari hilo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom