kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,423
- 13,935
Majukumu ya mwanamke yanafanana kabisa na majukumu ya viumbe vingine vyenye jinsi ya kike, na yatabaki hivyo hivyo kama yalivyotoka kwa Mungu. Kazi wanazofanya majike ya simba, ng'ombe, kuku na viumbe vingine ni hizohizo anazotakiwa kuzifanya mwanamke, na zile za madume ya simba, ng'ombe, kuku, n.k ni hizohizo anazotakiwa azifanye mwanaume. Mtu atakaetunga na kulazimisha mwanamke afanye majukumu ya mwanaume na mwanaume afanye majukumu ya mwanamke atakuwa anamkosea Mungu.
Mfano, majike ya viumbe vyote ndio wanaofanyakazi nyingi za kutunza watoto wao kwa saa 24 za siku, hivyo kumkataza mwanamke asifanyekazi ya kumuongezea kipato cha kutunza watoto wake atakuwa anamkosea Mungu. Anayemlazimisha mkewe ampikie na kumfulia mumewe atakuwa anamkosea Mungu, kwani majike ya simba, ng'ombe, kuku, fisi, n.k hawayahudumii madume wao kwa lolote lile zaidi ya kupeana mapenzi tu. Na huo ndiyo mpango wa Mungu kwa viumbe wake wote. kupika, kupiga deki, au kufua ni kazi ya mke na mume kwa pamoja, sio lazima kwa mwanamke. Mwanaume kumtunza mwanamke wake sio lazima ni hiari au maelewano yao tu. Mwanamke na mwanaume kupeana mapenzi ni lazima sio hiari. Mwanaume kuolewa na mwanaume mwenzake (ushoga) ni kumkosea Mungu, maana hata viumbe vingine havifanyi hivyo. Mume kuwa na mke mmoja sio sawa maana hata viumbe vingine havifanyi hivyo. Mke kukubali kuolewa/kutembea na mke dhaifu/mgonjwa sio sawa maana hata viumbe vingine hafifanyi hivyo....... itaendelea kesho, ha