Majukumu ya mbunge: Ni kutoa fedha yake mfukoni? kwa ajili ya maendeleo ya watu na jimbo lake. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majukumu ya mbunge: Ni kutoa fedha yake mfukoni? kwa ajili ya maendeleo ya watu na jimbo lake.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by matunge, Apr 13, 2011.

 1. m

  matunge JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 60
  Nimekuwa nikisikia waheshimiwa wabunge wametoa mali ama fedha zao binafsi kwa ajili ya kusaidia huduma za jamii.Hili hunishangaza sana.Naomba kuuliza wakuu katika JF.Je hii si aina ya rushwa?. Kwa mtazamo wangu; kazi ya mbunge ni kuishawishi serikali ili iweze kutekeleza ilani ya chama tawala kwa namna itakayonufaisha watu na jimbo lake, kwa kutumia fedha za walipa kodi kote nchini, na si kutoa fedha zake mwenyewe.Naomba kuwasilisha.
   
 2. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,578
  Likes Received: 1,674
  Trophy Points: 280
  Sio hela zao hizo, ni za mfuko wa jimbo!
   
 3. m

  matunge JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 60
  Mkuu natambua kuna fedha ya mfuko wa jimbo.Misaada wanayotoa baadhi ya waheshimiwa ni zaidi ya fedha inayotolewa kwa kila jimbo.
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  Mbunge achangia fedha za madawati

  Imeandikwa na Na John Nditi, Morogoro; Tarehe: 12th April 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 25; Jumla ya maoni: 0
  MBUNGE wa Mvomero, Amos Makalla (CCM) ametoa Sh milioni 1.6 kwa ajili ya kuwezesha
  kutengeneza madawati katika shule ya msingi Mgudeni, wilayani Mvomero.

  Fedha hizo zenye uwezo wa kutengenezesha madawati 40, amezitoa kutokana na ombi
  lililowasilishwa kwake na uongozi wa serikali ya kijiji cha Mgudeni la kutaka kukabili uhaba wa madawati 80 shuleni hapo.

  Katika ombi la wanakijiji hao, Ofisa Mtendaji wa Serikali ya Kijiji hicho, Hassan Mrisho, alisema wanafunzi wanakaa sakafuni kutokana na wananchi kukosa uwezo wa kuchangia fedha za kutengeneza madawati awamu kwa awamu.

  Akijibu, mbunge huyo alisema kuwa suala la elimu lazima liwekewe msukumo zaidi kwa
  wananchi kujitokeza kuchangia ili kuunga mkono juhudi za Serikali za kuboresha elimu kuanzia msingi hadi vyuo vikuu.
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Apr 13, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,233
  Trophy Points: 280
  PHP:
  Nimekuwa nikisikia waheshimiwa wabunge wametoa mali ama fedha zao  binafsi kwa ajili ya kusaidia huduma za jamii.Hili hunishangaza  sana.Naomba kuuliza wakuu katika JF.Je hii si aina ya rushwa?.  Kwa mtazamo wangukazi ya mbunge ni kuishawishi serikali ili iweze  kutekeleza ilani ya chama tawala kwa namna itakayonufaisha watu na jimbo  lakekwa kutumia fedha za walipa kodi kote nchinina si kutoa fedha  zake mwenyewe.Naomba kuwasilisha.
  Ukweli hizi ndizo takrima ambazo siku nyingi tumezikataza lakini hakuna anayesikia............................tatizo la takrima zinaleta ubaguzi ya kimapato ndani ya jamii na wasionacho kamwe hawatona ngazi za uongozi kwenye taifa lao...................
   
 6. m

  msambaru JF-Expert Member

  #6
  Apr 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Mbunge ni chachu au link kati wa wananchi na serikali sio mfadhili unless akikaribishwa ktk sherehe za kijamii kwa heshima yake.Tazama anachofanya Mama yangu Anne Kilango same mashariki, amewaunganisha wapiga kura wake na wanunuzi wa tangawizi moja kwa moja wa dola inapatikana same huyo ndo aina ya wabunge tunawataka sio kama Dewji, Mahindi anayanunua yeye kupitia mawakala wake singida lakini sembe anayozalisha wanyaturu na wanyiramba wale hawawezi kumudu bei yake wa nini sasa mtu huyu?
   
 7. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #7
  Apr 13, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ulivyonena, ndivyo inavyotakuwa kuwa (de jure), lakini hali halisi (de facto) ni kwamba umaskini unawafanya watu wawafanye wabunge wao viATM. Hata baadhi yetu tukienda likizo vijijini watu wanaandamana kuomba misaada, sembuse wabunge? Ubunge katika nchi maskini ni mzigo mkubwa sana.

  POLENI WABUNGE WETU.
   
Loading...