Majukumu ya familia

Reagan Carima

Member
May 20, 2015
44
194
Katika familia zetu desturi iliyopo ni kuwa baba ndie msimamizi wa issue zote hasa masuala ya kifedha.

Tumezoea kumuona mama akimuomba baba pesa kwa ajili ya mambo fulani either yake binafsi, watoto au familia nzima.

Hii desturi binafsi sioni kama ina manufaa hasa kwa mustakabali ya familia nzima.
Kumfanya mama kuomba pesa kwa baba kunamfanya anajiona mtumwa, mnyonge na ombaomba.

Masuala haya ndio yanayowafanya wanawake wengi wanakuwa na uchu wa kuwa na vyakwao.
Wanajitahidi kadri ya uwezo wao ili siku wawe na sehemu itakayowapa kipato chao ili wasiwe wanaomba omba.

Au unadhani wanapenda ile hali ya kuomba kila kitu? Embu vaa uhusika wake Je! Wewe ungependa kuomba kila ambapo unakuwa na uhitaji?

Tabia hii imezaa matunda mabaya hasa kwa wasichana ambao wanaingia kwenye majukumu hivi sasa, kwakuw awalizoea kuona mama akiomba kila kitu basi nao wakiolewa chakwanza wanataka kuona nao wakiwa na uhuru wa matumizi eithee kwa siri au kwa wazi.
Jambo ambalo mwisho wa simu ni migogoro isiyo isha.

Hitimisho:
Wanaume tuangalie namna ya kusimamia majukumu katika familia zetu, tusiwafanye wake zetu wajione watumwa hata kama mkeo hana kazi usimfanye akajiona mtumwa. Usiwafanye watoto au Mkeo wakaona kuwa kila kitu nicha Baba bali waone ni mali za familia na wote wazifurahie.

Kama tutaweza kulisimamia hili kwa busara basi turazalisha vizazi vyenye nguvu sana.

Karibu kwa nyongeza
 
Ni kweli uyasemayo, wengi hatuna uhuru wa kiuchumi kwa hiyo tunajitahidi angalau kujenga mazingira mazuri ya usimamizi wa fedha kwa kadiri baba wa familia anavyoona inafaa, wengi wetu wanaume ndio wamekuwa wasimamizi wa fedha na mwanamke anapohitaji fedha basi atapewa kadiri ya mahitaji yake au kilichopo.
Mimi binafsi sipendi kuombwa fedha na wife naye hapendi kuomba mara kwa mara fedha kwa ajili ya mahitaji ya nyumba, tunachokifanya ni kununua mahitaji ya msingi ya nyumbani kwa wingi yanayotunzika na kisha kuacha fedha mezani kwa ajili ya matumizi madogomadogo ya nyumbani.

Tuliwahi kujaribu kupanga bajeti ya mwezi mzima pamoja kisha nikamuachia fedha mke wangu, fedha zilikwisha baada ya wiki tu. Nikaachana na utaratibu huo
 
Ni kweli Mkuu! Kutokana na mahitaji ya familia huwezi kuweka bajeti ikawa constant hivyo labda kwa mbinu nyingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom