Major spill of toxic sludge from Barrick's mine | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Major spill of toxic sludge from Barrick's mine

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Offish, May 19, 2009.

 1. Offish

  Offish Senior Member

  #1
  May 19, 2009
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 172
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Major emergency at Barrick's North Mara mine, Tanzania
  [FONT=&quot]It is reported that there has been a major spill of toxic sludge from Barrick's Mara mining operation into River Thigithe that flows into the Mara River. This happened Monday the 11th of May and nearby residents have reported that there are dead fish and all kinds of other dead water life along the river.The entire community is in a huge uproar and panic. People are very scared in the whole area.

  [/FONT]

  Taarifa kuhusu matukio katika mgodi wa North Mara

  Mara, 14 Mei, 2009 – Mgodi wa dhahabu wa North Mara (NMGM) umechukua hatua za haraka kukabiliana na tukio la kuvuja maji kutoka kwenye karo moja la kuhifadhia maji kwenye mgodi wake uliyopo kata ya Nyamongo, Wilaya ya Tarime, Mkoani Mara.

  Uchunguzi wa sampuli za maji umeonesha kwamba kiwango cha tindikali (pH) kwenye maji imerudia hali ya salama. Usimamizi na ufuatiliaji wa hali hiyo umepewa kipaumbele na NMGM na utaendelea kwa kadiri itakavyohitajika.

  Inatarajiwa kwamba kazi ya kuzuia na kubadili mwelekeo wa maji yanayoingia mtoni itakamilika wiki ijayo. Kuna njia kadhaa zinafikiriwa kukabiliana na hali kama hiyo katika siku za baadae.

  Mamlaka zote katika eneo zimefahamishwa, ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Wilaya, Wizara ya Nishati na Madini, Mamlaka ya Bonde la Ziwa Victoria na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC). Mikutano na wanavijiji imefanyika kuwafahamisha kuhusu hali halisi na kupata ushirikiano wao katika ufumbuzi wa muda mrefu.

  Ufuatiliaji unaoendelea katika Mto Tigithi, unaokatiza katika eneo moja la mgodi wa North Mara, unaonesha kwamba ongezeko la kiwango cha tindikali (pH) katika maji umedhihirika katika eneo dogo la mto ambalo liko karibu na eneo la tukio.

  Vipimo vinaonesha kwamba viwango vya pH takriban kilometa 4 – 5 chini ya eneo ni vya kawaida.

  Tukio la kufurika na kuvuja maji ni matokeo ya vitu viwili: ongezeko la mvua zinazonyeesha na hujuma kwenye utando wa karo la maji.

  Ongezeko kuu la kiasi cha tindikali kwenye maji linasadikiwa kusababishwa na maji kutiririka kutoka katika makaro maalum ya kuzuia maji yaliyogusana na masalia ya ufuaji madini. Ili kuzuia mtiririko huo, makaro hayo hutandikwa utando wa plastiki (PVC liner). Lakini katika mara kwa mara, plastiki hizo zimehujumiwa na vibaka. Kingine kilichosababisha ongezeko hilo ni lundo la madini fifi ambalo limetiririsha maji kutokana na ongezeko la mvua.


  Maelezo zaidi:

  §Kubainika kwa ongezeko la kiasi cha tindikali (pH) kwenye maji kulitokana na ufuatiliaji wa kawaida wa ubora wa maji ambao hufanyika NMGM.
  §NMGM imeongeza maeneo na kiasi cha ufuatiliaji na upimaji ubora wa maji.
  §Watalamu wa mazingira na maji wa NMGM walichunguza na kubaini yafuatayo:
  [FONT=&quot]o[/FONT]Kiasi cha tindikali kwenye maji mita 1000 chini ya eneo la tukio ni pH 4.8. (Kwa kawaida maji ya kunywa huwa na kiasi cha tindikali cha pH 6.5 – 7). Hakuna athari yoyote iliyobainika katika maji ya mto kilometa 4 – 5 chini ya eneo la tukio.
  [FONT=&quot]o[/FONT]Wingi wa maji (mtiririko) kutokana na mvua za masika zinaongeza uwezo wa maji kujichuja na hivyo kupoza mtiririko wa maji yaliyotoka mgodini.
  §Uongozi wa mgodi na viongozi wa kijiji na wilaya wamekuwa na mikutano ya mara kwa mara kujadili hatua zilizochukuliwa na kuhakikisha kuwa wananchi wanafahamishwa kinagaubaga kuhusu hali halisi.
  §Mgodi, kwa ushirikiano na wanakijiji, umekubaliana na hatua kadhaa za kuchukuliwa kukabiliana na hali iliyotokea. Hatua hizo ni pamoja na:
  1.Kutandika utando mpya wa plastiki kwenye makaro;
  2.Mbinu za kuzuia maji yenye kiasi cha juu zaidi cha tindikali kutiririka kutoka mgodini;
  3.Mgodi kuhamisha kwa muda madini fifi yaliyo hafifu zaidi;
  Wanakijiji kuhakikisha kuwa vitendo vya wizi vinavyohujumu usalama wa makaro havitokei tena
   

  Attached Files:

Loading...