Major Lazer waja na ‘Loyal’, awamu hii wakiwa na Kizz Daniel na Kranium

Kabota

Member
Aug 15, 2009
63
10
Major Lazer wameachia wimbo mpya, ‘Loyal’ waliomshirikisha staa wa Jamaica, Kranium pamoja na hitmaker wa Nigeria, Kizz Daniel, Jumatano hii. Wimbo huu umekuja na video yake, ya nne katika ushirikiano wa Major Lazer na muongozaji wa Afrika Kusini, Adriaan Louw

Tazama video ya Loyal hapa:Loyal 4000x4000 300dpi.jpg

‘Loyal’ ni wimbo wa mwisho katika nyimbo za ushirikiano kati ya Major Lazer na wasanii wa Afrika ikifuata baada ya ‘Tied Up’ wakiwashirikisha Mr. Eazi na Raye, “Orkant/Balance Pon It” wakimshirikisha muimbaji wa Afrika Kusini, Babes Wodumo na ‘All My Life’ wakimshirikisha staa wa Nigeria, Burna Boy.

Hivi karibuni Major Lazer waliachia mkusanyiko mpya wa nyimbo wa Afrobeats Mix, unaojumuisha muziki toka bara la Afrika na kuusambaza katika majukwaa yao ya kimataifa.

Bendi hiyo inafanya ziara yake Afrika kuanzia September na October na kupita katika nchi za Afrika Kusini, Malawi, Kenya na Uganda.

Pamoja na ziara ya kimuziki, Major Lazer wameungana na asasi ya VETPAW (Veterans Empowered to Protect African Wildlife) kusaidia kukuza uelewa kuhusu uwindaji haramu barani Afrika.

Wakiwa Afrika, Major Lazer watatembelea makao makuu ya VETPAW kushiriki katika kampeni za kutokomeza uharamia na kujifunza zaidi kuhusu changamoto zake na jinsi ya kubaliana nazo.
 
Jamanii eeeh natafuta jina la ule wimbo was afrika kusini upon kwenye muvi ya black panther..
Pale Tchala anaenda kule kwenye kiwanda cha technology zao...
 
'Particular' mpaka leo kuna somebody anasema ananikumbuka akiusikia!.. and hell yeah ule wimbo upo kwenye history nzuri kwangu!.. Major Lazer waliimba ile song bana!.
Although video was bad!.
 
'Particular' mpaka leo kuna somebody anasema ananikumbuka akiusikia!.. and hell yeah ule wimbo upo kwenye history nzuri kwangu!.. Major Lazer waliimba ile song bana!.
Although video was bad!.
Mkuu huu wimbo mkali audio mpaka video, ww hukuielewa video yake
 
'Particular' mpaka leo kuna somebody anasema ananikumbuka akiusikia!.. and hell yeah ule wimbo upo kwenye history nzuri kwangu!.. Major Lazer waliimba ile song bana!.
Although video was bad!.
sijawahi kusikia hao major lazer wameimba zaidi ya walioshirikishwa
 
Mkuu huu wimbo mkali audio mpaka video, ww hukuielewa video yake
Nilivyokuwa naiexpect na nilivyoiona haikuwa sawa!.
Naona kama ile video sawa na idea ya video kwenye nyimbo flani ya Vinc & Mensa - am i wrong!.
 
sijawahi kusikia hao major lazer wameimba zaidi ya walioshirikishwa
Zipo nyingi sana ila kali kwangu tafuta hizi:
• Major Lazer feat Ice Prince, Patoranking&Jidenna - Particular
• Major Lazer feat PARTYNEXTDOOR & Nicki Minaj - Run Up.
Kesho nishtue nikutumie Album yao kama utaitaka!.
 
Kuna wengine wanaitwa Dave East, Daft Punk na N.E.R.Dnao wanadrop some bombs kwenye mainstream sana!.
Fun nilimkubali kwenye ule wimbo wake wa 'we are young'.
David Bowie nikamuelewa kwenye 'Starman' na Beastie Boyz niliwakubali kwenye 'sabotage' au Ryan Leslie kwenye 'how it was supposed to be'.
Me kuna aina flani ya miziki huwa naipenda sana nikiwa na stress!!..
 
Zipo nyingi sana ila kali kwangu tafuta hizi:
• Major Lazer feat Ice Prince, Patoranking&Jidenna - Particular
• Major Lazer feat PARTYNEXTDOOR & Nicki Minaj - Run Up.
Kesho nishtue nikutumie Album yao kama utaitaka!.
nadhani hujanielewa hizo zote ninazo na nazipenda,, na maanisha wao kama wao major lazer kuimba.

wanafanya kama dj khalid, cavin harris, benny bannas na david guetta,
 
nadhani hujanielewa hizo zote ninazo na nazipenda,, na maanisha wao kama wao major lazer kuimba.

wanafanya kama dj khalid, cavin harris, benny bannas na david guetta,
Sasa kwenye hizo show zao wana perform nini? Au wanakua kama ma DJ
 
Hii loyal sichoki kuisikiliza toka imetoka mpaka leo ndio nyimbo ninayo isikiliza saaaana kwenye playlist yangu sababu kubwa ni kizz Daniel namkubali sana ndio msanii ninae mkubali Nigeria....Kali saaana
 
Sasa kwenye hizo show zao wana perform nini? Au wanakua kama ma DJ
wanakuwa na wasanii waliowashirikisha hata kama si wote.

mfano hao major lazer wametoa ngoma mfululizo na wasanii wa afrika si unaona wana ziara afrika, nadhani wanakuwa nao.
 
Back
Top Bottom