Major General Mbuge Kuwa RC kutoka Mkuu wa JKT Kapanda Cheo au kashuka?

kuna walakini mkubwa katika suala la kuwapigia salute wana siasa,huwa wanapenda sana kwa sababu za kujikweza lakini huwa hakuna uhalisia,hebu chukulia mkuu wa majashi ni nani halafu tulinganishe

MKUU WA MAJESHI:- CDF

Majukumu ya Msingi ya JWTZ


• Kulinda Katiba na Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

• Ulinzi wa Mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

• Kufanya Mafunzo na Mazoezi ili kujiweka tayari Kivita wakati wote.

• Kufundisha umma shughuli za Ulinzi wa Taifa.

• Kushirikiana na Mamlaka za Kiraia katika kutoa misaada ya kibinadamu na uokoaji wakati wa maafa.

• Kukuza elimu ya kujitegemea na uzalishaji kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

• Kushiriki katika shughuli za Ulinzi wa Amani Kimataifa.
Dhima ya JWTZ

Kulinda nchi na kutetea maslahi ya Taifa la Tanzania, kutoa msaada kwa Mamlaka za kiraia na kuwezesha kufikiwa kwa malengo ya Kitaifa na Kimataifa.

The TPDF is a unified force consisting of the Army or infantry brigades, Air Force, Navy, and National Service. The army does not operate in its command, but consists of infantry brigades directly under the command of the Chief of Defense Forces (CDF).

Higher Defense Organization

The Commander in Chief (C in C)


The Constitution of the United Republic of Tanzania, empowers the President of the United Republic of Tanzania to be the Commander of the Armed Forces. As the Commander in Chief he is empowered to declare war and commit the Defense Forces or part of it to active operations in or outside Tanzania.

The National Defense and Security Council (NDSC)

The NDSC is the highest decision-making authority in defense and security matters. It formulates defense and security strategies to meet the objectives of national defense. It comprises the President of the United Republic, the President of the Revolutionary Government of Zanzibar, ministers responsible for defense and security, and the chiefs of the defense and security organs.

The Ministry of Defense

The Tanzanian Ministry of Defense is designed to support Tanzania’s foreign policy and security policy objectives. It guides the contributions of the Defense Forces to meet defense and security goals, and shapes their structure and capabilities. The Ministry of Defense has the responsibility to ensure consistency in training and maintaining the Armed Forces in accordance with the defense doctrine.

The Defense Forces Committee (DFC)

According to the National Defense Act of 1966, the DFC is a committee at the Ministry of Defense level responsible for policy review and formulation on all matters relating to the administration and running of the TPDF. It consists of the Minister of Defense, the Chief of Defense Forces, the Permanent Secretary, the Chief of Personnel, and any other officer who may be appointed by the Minister of Defense.


SEHEMU YA KWANZA: KUHUSU MKUU WA MKOA

- Ni sehemu ya Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

- Ofisi za Mkuu wa Mkoa zitakuwa kwenye Makao Makuu ya Mkoa husika

- Mkuu wa Mkoa atawajibika chini ya Waziri wa TAMISEMI

2. DHIMA YA KAZI HII

Kuhakikisha kuwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii yanapatikana kutokana na huduma bora za ushauri na uratibu ambazo zinajenga mazingira bora kwa Serikali za Mitaa na wadau kutoa huduma inayotarajiwa.

3. MAJUKUMU NA KAZI ZA MKUU WA MKOA

- Kuhakikisha uwepo wa Haki na Sheria kk mkoa

- Kuongoza na kusimamia operesheni za Maafa na Kufariji

- Kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa(RCC), Mkuu wa Mkoa atawajibika kufanya jitihada za kuhakikisha kutimizwa kwa sera za serikali juu ya Mkoa husika.

- Kufanya yale yote yatakayosaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa mkoa kwa ushirikiano na serikali za mitaa.

4. ELIMU

Mkuu wa Mkoa itampasa awe na Elimu Ngazi ya Shahada(Degree) au inayoshabihiana na hiyo kutoka kwenye Taasisi ya Elimu inayotambulika.

5. UELEWA

Mkuu wa Mkoa atapaswa awe ni mwenye ufahamu kuhusu Utawala wa Sheria, Utawala bora, Kanuni za Haki Asilia (Natural Justice), Sera na taratibu zake, Uongozi na Utawala pamoja na masuala yote ya msingi ktk utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo.

6. UJUZI

Kimsingi Mkuu wa Mkoa anapaswa kuwa na stadi zote za uongozi;

Ujuzi wa kujenga umoja, ujuzi wa kutatua changamoto, ujuzi wa kutoa ushauri nasaha, ujuzi wa maridhiano, ujuzi wa kuhimili msongo/mihemuko, sambamba na ujuzi kuhusu mahusiano ya umma na uwezo wa kuzungumza vizuri mbele za watu.

7. SIFA BINAFSI

Aonyeshe uwezo wa kutunza siri, kufanya maamuzi yenye tija, kufanya kazi pasipo mashinikizo, uelewa kuhusu mwenendo wa siasa na tamaduni za jamii, awe na heshima, mbunifu, mtenda haki, bila kusahau kuheshimu miiko ya kazi.

8. UZOEFU

Ni lazima Mkuu wa Mkoa awe ni mtu mwenye uzoefu kuhusu masuala ya utawala/siasa usiopungua Miaka 10.

9. MSHAHARA

Mkuu wa Mkoa atalipwa kiwango cha mshahara kwa taratibu zilizoainishwa na Ofisi ya Utumishi (kwa sasa salary scale yake ni LSS(P) 4).

TOFAUTI ILIYOPO ni kubwa mno ni mbingu na ardhi sababu inayo daiwa kuwa wakuu wa mikoa ni wawakilishi wa raisi katika maeneo yao sawa lakini kiutawala na majukumu wako chini ya idara zingine za serikali.
Mkuu wa mkoa = mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa

Mkuu wa majeshi= mjumbe wa baraza la usalama la taifa ambalo ni
Rais wa JMT na SMZ mawazili wa ulinzi na wakuu wa vyombo vya usalama.
Mkisema wilaya hapo ndio nachanganya oil na maji kabisa.
mkuu kufanya hivyo ni kuonyesha heshima na utii kwa mamlaka tu wala si kingine.

tukianza kupima kipi ni kipi tutajikuta tunajadili ni jinsi gani haifai cdf kupiga salute kwa rais.
 
Mabeyo alizingua
Jenerali Mabeyo hakuzingua.
RAIA anayepigiwa saluti na Askari Jeshi, ni ama AKIFARIKI, au akiwa Mteule wa Rais mwenye Cheo cha Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa, Waziri, Waziri Mkuu na Makamu wa Rais.
Pia Wakuu wa Mihimili, kwa maana ya Spika na Naibu Spika.
Upande wa Mhimili wa Mahakama, kuanzia Hakimu mpaka Jaji Mkuu wanapigiwa saluti.
 
Habari wanabodi? naomba kupata uelewa kidogo, kwa nafasi kama ya Major General Mbuge kutoka kuwa Mkuu wa JKT na kwenda kuwa RC je hapo kapanda cheo ama kashuka? naomba uelewa wa kina juu ya hili tafadhali.

Hongera kwake kwa uteuzi!!
Amepanda cheo.
Kiitifaki, Mkuu wa Mkoa yuko ngazi moja na Waziri.
Kwa mantiki hii, Maj. Gen. Mbuge amepanda Cheo
 
Habari wanabodi? naomba kupata uelewa kidogo, kwa nafasi kama ya Major General Mbuge kutoka kuwa Mkuu wa JKT na kwenda kuwa RC je hapo kapanda cheo ama kashuka? naomba uelewa wa kina juu ya hili tafadhali.

Hongera kwake kwa uteuzi!!
Ni demotion full stop. JKT imeanzishwa na sheria ya Bunge ya mwaka 1964 hivyo ni anawajibika nchi nzima. Pili ni Maj. Gen. Katika candidates wa kumrithi CDF alikuwa ni mmojawapo na alikuwa analisubiri hilo ambalo limeyeyuka. Wakuu wa kamandi husika ndiyo warithi halisi kuliko mtu ambaye eti amejenga ukuta wa Mererani. Taratibu na tamaduni za TPDF zifuatwe!
 
Ningekuwa Mimi Ningefanya Kama alivyofanya Maswanya aliekataa Uteuzi Wa DC, Kutoka Kuwa Mkuu Wa JKT Nchi Nzima Kuwa Rc.... Hapana
Jeshini hakuna hapana afande utatimuliwa kwa fedheha yeye ni mwanajeshi sio Raia amekuwa seconded kwenda kuwa RC hapaswi kujadili ni kutiii
 
Nani anakumbuka upandaji wa vyeo kwa huyu Major General Charles Mbuge!!....Paul Makonda analijua sana hili jambo

Huyu jamaa alizingua sana akiwa Mkuu wa JKT alikuwa anawachukia sana Makamanda waliokwenda shule na alipenda sana kuwaweka vibaraka wake kwenye nafasi mbalimbali JKT, professionalism kwa huyu Kamanda ilikuwa zeero kabisa!!

Kuna jamaa alimchukia sana kisa hakuenda kumpongeza alivyopandishwa cheo na mwendazake. Akaamua kumtupa Kigoma and then wakati wenzake wanapandishwa vyeo mwezi wa 2 kuwa Ma-Major jjna la huyo jamaa akalinyofoa makusudi tu kwa sababu ya chuki zake binafsi . Kwahiyo wenzake wamekuwa Ma-Major yeye bado ni Captain. Huyu jamaa yuko kambi ya Mtabila Kigoma na ni Msomi mzuri tu.

Acha karma imle!!!
Nidokeze PM mzee mtabila napajua nimeishi mule hata CO wa pale namjua labda Kama kabadilishwa

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Nyota mbili zinabakia palepale sema siyo tena mkuu wa JKT. Either itamlazimu Rais kumpandisha cheo brigedia general ili ashike nafasi hiyo ama atalazimika kumhamisha meja jenero mwingine ili awe mkuu wa JKT. Kwanza wamelundikwa huko hovyo hovyo tuu na hakuna wanalofanya. Madam chomoa kimeja kimoja kikave pengo!
Unaleta utani yaani major awe mkuu wa JKT kamandi kubwa Kama Ile

Jkt Kuna ma kanali kibao na mabrigedia na ma major general kibao tu

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Kama Mbuge kawa mkuu wa mkoa na mkuu wa mkoa ni mteule wa Rais ,swali je atapigiwa saluti na CDF?
Naomba majibu
Itategenea watakapokutana .

Wakikutana mbuge kavaa kiraia mabeyo vazi rasmi la jeshi mabeyo atapiga saluti

Wakikutana wote wamevaa sare za jeshi mbuge lazima apige saluti

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Kinachonishangaza kila mchangiaji kwenye hii mada anamjadili Charles Mbuge kama Major General wakati ukweli ni kwamba cheo chake alichonacho hadi dakika hii ni Brigadier General na wala siyo Major General.
Wewe ndio hujui mbuge Ni major janerali kapandishwa mwaka jana hapo dodoma na mabeyo ndio aliemvisha vyeo ofisi za jeshi dodoma .

Ubrigedia alipewa miwili au mitatu nyuma hadharani Tena kwenye mkutano na gari yake ikawekwa nyota

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Uongo mwingine uache,, dodoma na merelani ndo project zilizompa vyeo mbuge, na kama hujui the guy is brilliant engineer the army have, alitoka kuwa mkuu wa jkt ruvu, akaenda kusimamia ukuta merelani akanda cheo,, akapewa project ya dodoma akapanda vyeo,,for tangu operation merelani amekuwa akijihusisha zaid na ujenzi na sio uongozi,
Na kwa taarifa yako sio yeye anayehusika na kupandisha vyeo, acha kuongea upuuzi wako
Alikuwa mkuu wa JKT kwa kupendekezwa na mabeyo and no one else,,
Akiwa jkt kazi yake ni kusimamia kambi zote za jkt na ufanisi wake,, amefanya kazi bomba sana tangu akiwa msimamiz wa mafunzo ya jkt
Cjui unaongea bang gani
Mkuu tuwekee ushahidi kuwa alipendekezwa na MABEYO.
 
Ukisikia Mkuu wa JKT Tanzania nzima unadhani hao JKT ni kama mamilioni hivi? Kumbe hata 5000 hawafiki....hahaha ujinga kipaji. Mkuu wa mkoa kimajukumu is far a million than Mkuu wa JKT. Anzia hapo... Mwakilishi wa Rais Mkoa wenye watu zaidi milioni 3+ M/kiti wa Baraza la usalama la mkoa... Kuomba fedha kwa mkurugenzi ni formality sawa na wewe uwe boss wa taasisi then uombe fedha kwa watu wa finance.

Malizia hapa gari yake inapeperusha bendera ya nchi muda wote mpaka tu Rais anapokuwa mgeni wa mkoa husika.
Toa na idadi ya JWTZ, TISS, POLICE na majeshi mengine afu uisome upya comment yako
 
Back
Top Bottom