Meja Jenerali Abdallah Senussi: Mkuu wa Idara ya Ujasusi wa Jeshi Libya aliyetishia kuita Fighter Jet kulipua Gereza la Abu Salim lililojaa wapinzani

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,316
MAJOR GENERAL Abdullah al-Senussi: Mkuu wa Idara ya Ujasusi wa Jeshi Libya (Military Intelligence Wing) aliyetishia kuita ndege vita (Russian Sukhoi Su-30 fighter) kuja kulipua gereza la ABU SALIM walimojaa wafungwa wa kisiasa (Political Detainees)

SHEIKH ABDULLAH AL-SENUSSI AKIWA NA SHEMEJI YAKE COLONEL MUAMMAR GADAFFI (MWENYE MIWANI NYEUSI) ENZI ZA UTAWALA WAO

IMG_20200420_125812_119.jpg


SHUHUDA WA KWANZA: Majira ya saa 11:00 jioni bomu la mkononi (grenade) ilitupwa katika moja ya ua za gereza. Sikuona ni nani aliyeitupa lakini nina uhakika ilikuwa grenade. Nilisikia mlipuko na punde tu baada ya mirindimo ya risasi za mara kwa mara tukasikia kuanza kutoka kwa milio ya silaha nzito ikiwemo Kalashnikov kutoka juu ya paa. Upigaji wa risasi uliendelea kutoka saa 11:00 hadi saa 1:35 jioni

SHUHUDA WA PILI: Sikuweza kuona wafungwa waliokufa ambao walipigwa risasi, lakini niliweza kuona wale ambao walikuwa wakipiga risasi. Walikuwa ni kitengo maalum na walivaa kofia za jeshi la khaki. Sita walikuwa wakitumia Kalashnikov

SHUHUDA WA TATU: Dakika tano au saba baada ya kuanza, walinzi kwenye paa walipiga risasi wafungwa ambao walikuwa kwenye maeneo ya wazi. Kulikuwa na wafungwa 16 au 17 walijeruhiwa na risasi. Hatimaye Wafungwa waliwachukua walinzi wawili mateka.

HUU NDIO MKASA HALISI WA MAUJI YA HALAIKI KATIKA GEREZA LA ABU SALIM HUKO MJINI TRIPOLI NCHINI LIBYA. FUATILIANA NAMI MPAKA MWISHO.

Katika msimu wa joto wa mwaka 1996, habari zilianza kutapakaa kote mashariki ya kati kutoka Libya kuhusu mauaji ya watu wengi katika gereza lenye kujaa ukatili pamoja na ulinzi mkali la Tripoli la Abu Salim.

Maelezo hayo yalibaki hafifu pasipo kuwa na ufafanuzi wa kutosha, na hapo awali serikali ilikana kwamba tukio hilo limetokea. Makundi ya Libya nje ya nchi yalisema hadi wafungwa 1,270 walikuwa wamekufa katika mkasa huo wa ajabu na kutisha ulioratibiwa na aliyekuwa mkuu wa kitengo cha Intelijensia ya jeshi (Military Intelligence Wing) Sheikh Abdullah Senussi ambaye pia alipata kuwa shemeji wa Rais wa wakati huo Colonel Muammar Gaddafi.

Mnamo 2001 na 2002, viongozi wa Libya walianza kuarifu baadhi ya familia na jamaa huko Abu Salim kwamba mwenzi wa familia yao (yaani family member) amekufa, ingawa hawakutoa mwili au maelezo juu ya sababu ya kifo.

Mnamo Aprili 2004 kiongozi wa Libya Mu`ammar al-Qadhafi alikiri hadharani kwamba mauaji yalifanyika katika gereza la Abu Salim, na akasema kwamba familia za wafungwa zina haki ya kujua nini kilitokea.

Mnamo mwezi Mei mwaka 2005 watetezi wa haki za binadamu walitembelea gereza la Abu Salim, lililoendeshwa na Idara ya Usalama wa Ndani (Internal Security Agency). Mkuu wa idara hiyo ya usalama wa ndani alisema serikali imefungua uchunguzi kuhusu tukio hilo la 1996, lakini haikutoa habari juu ya aina au muda wa uchunguzi. Baadaye watetezi wa haki za binadamu waliiuliza serikali ya Libya kwa maelezo juu ya uchunguzi, lakini serikali ilishindwa kujibu.

Wafungwa katika gereza la Abu Salim waliohojiwa na watetezi wa haki za binadamu mnamo mwezi Mei ila hawakutaka kusema juu ya tukio hilo, inaonekana ni kwa sababu ya hofu juu ya maisha yao. Mahojiano yalilenga kesi zao binafsi, na wote walisema kwamba hali katika gereza hilo zilikuwa bora zaidi jambo ambalo si sahihi.

Mnamo Juni 2004 na tena September 2006, watetezi wa haki za binadamu walimhoji mfungwa wa zamani wa Abu Salim ambaye anadai alishuhudia mauaji hayo.

Sasa akiishi Saudi Arabia, ambapo ameomba hifadhi, alisema alitumikia kifungo kuanzia 1988 mpaka 2000 huko Abu Salim kwa mashtaka ya uchochezi wa kisiasa, lakini hajawahi kufikishwa mahakamani (detention without trial)

Madai yake hayakuweza kuthibitishwa, lakini maelezo mengi yanaambatana na ripoti kutoka kwa kikundi cha wa Libya waishio nje ya nchi na maelezo ya wafungwa wengine walioshuhudia tukio lile.

Kulingana na maelezo ya mfungwa aliyenusurika katika tukio lile, tukio hilo lilianza karibu 4:40 asubuhi. mnamo Juni 28, wakati wafungwa katika block numba 4 walimkamata mlinzi ambaye alikuwa akileta chakula chao. Mamia ya wafungwa kutoka vitalu 3, 5 na 6 walitoroka seli zao. Walikasirika juu ya kutengwa kwa familia na hali duni ya maisha, ambayo ilikuwa imezorota baada ya wafungwa wengine kutoroka mwaka uliopita.

Nusu saa baadaye, shuhuda anasema, maafisa wawili wa ngazi za juu wa usalama akiwemo Abdullah Sanussi, ambaye ameoa dada wa mke wa Qadhafi, na mkuu wa gereza hilo walifika wakiwa katika gari aina ya Audi yenye rangi ya dark green akiwa na msafara mdogo wa walinzi wenye silaha kali (a contingent of security personnel)

Sanussi aliamuru ufyatuaji huo wa risasi usimamishwe mara moja na aliwaambia wafungwa wachague wawakilishi wanne kwa ajili ya kufanya nao mazungumzo na kufikia muafaka na kama wangegoma angemuamuru mkuu wa kikosi cha anga (Air Force Commander) kutuma ndege vita (Russian Sukhoi Su-30 fighter) kuja kusambaratisha gereza zima la Abu Salim kwa makombora ya ndege na wafungwa wote kubaki kuwa historia.

HII NDIO RUSSIAN SUKHOI SU-30 FIGHER.
IMG_20200420_135936_206.jpg


JE, UNAJUA NI NINI KILITOKEA BAADA YA HAPO? ITAENDELEA WIKI IJAYO. JUST STAY TUNED.
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom