MAJOR GENERAL Abdullah al-Senussi na tuhuma za kutekwa kwa kiongozi wa uislam Imam "Musa Sadr"

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,316
MAJOR GENERAL Abdullah al-Senussi (Head of Military Intelligence) na tuhuma za kutekwa kwa kiongozi wa uislam Imam "Musa Sadr"

fgfvcfd (3).jpg


Good afternoon jamiiforums

Mnamo tarehe 13 mwezi Agosti mwaka 1978, viongozi wa kidini wa Lebanon Imam Musa al-Sadr pamoja na Sheikh Muhammad Yacoub, na mwandishi wa habari bwana Abbas Badreddin, walikuwa kwenye ziara rasmi ya kiserikali nchini Libya.

Siku hiyo, takribani miaka 43 iliyopita, ndio walionekana kwa mara ya mwisho wakitokea katika hoteli na wasaidizi kadhaa wa rais kuelekea katika mkutano na ndugu Muammar Qaddafi. Hawajawahi kuonekana tena tangu wakati huo.

Maombi yote ya mashirika ya haki za binadamu kwa serikali ya Libya kutaka uchunguzi huru kufanyika hayakufaulu hata kidogo, licha ya taarifa/ripoti zilizokuwa zinaendelea kutapakaa mashariki ya kati kuwa Imam na wenzake wako hai.

Badala yake, kumekuwa na vitisho mbadala vya kutaka kuua ndugu wa familia za waliopotea na kutoa ofa ya rushwa za kifedha kwa mawakili wao ili waachane na kesi hizo.

Mamlaka za Libya zilichelewesha uchunguzi na kukataa katakata na kuamua kutunga uongo wa makusudi kwamba Imam aliondoka Libya na kwenda Italy usiku wa Agosti 31. Mara mbili, mnamo mwaka 1979 na 1982, majaji walifanya uchunguzi nchini Italy na kuikataa taarifa hiyo ya uwongo.

Hulka ya viongozi katika mamlaka za Libya zimekuwa zile zile za kuendelea kukana utekaji nyara ho, licha ya hotuba ya kwenye TV ya Rais Qaddafi mnamo mwezi Agosti mwaka 2002, ambapo ulimi wake ulitereza na kujikuta anakiri kwa kusema "the Imam had disappeared here, in Libya" kisha matangazo hayo ya mubashara kusitishwa ghafla.

Baada ya zaidi ya miaka ishirini ya upatanishi ambao haukuzaa matunda na viongozi wa kisiasa ulimwenguni, familia za waliopotea ziliamua kupeleka kesi nchini Lebanon, ambapo Imam na wenzake ni raia wa huko.

fgfvcfd (6).jpg


Baada ya miaka saba ya vita vikali vya kisheria huko mahakamani, jaji alitoa hukumu ndefu ya kurasa takribani thelathini mnamo mwezi Agosti 21, mwaka 2008, "akimkuta na hatia mshtakiwa mkuu Mu'ammar al-Qaddafi na shemeji yake Abdullah al-Senussi kwa kula njama katika utekaji nyara na mauaji hayo" ya Imam na wenzake wawili.

Nitaendelea........................

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom