Major Abdulrahman Shimbo: Kamanda wa Kikosi cha JWTZ kilichozima jaribio la mapinduzi Seychelles

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,402
54,878
Anaitwa Abdulrahman Amiri Shimbo.

Alikuwa katika kikosi cha JWTZ kilichotumwa Seychelles kufundisha Jeshi la visiwa hivyo.

Major Abdulrahman Shimbo alikwenda Seychelles mwaka 1978 kuwa katika kikosi cha JWTZ kilichoongozwa na Lt.Col.Hassan Ngwilizi.

Hassan Ngwilizi alikuwa mwalimu wa Abdulrahman Shimbo chuo cha maofisa wa jeshi MonduliJ

Mwaka 1980 Lt.Col. Ngwilizi alirudi Tanzania, hivyo Major Shimbo akawa mkuu wa kikosi kilichokuwa Seychelles.

Mwaka 1981 Seychelles ikavamiwa na askari wa kukodiwa waliolenga kupindua Serikali ya nchi hiyo.

Jaribio hilo lilizimwa na kikosi cha JWTZ na kupelekea mamluki hao kuteka ndege na kutoroka kwenda Afrika ya Kusini.

Abdulrahman Shimbo alipanda ngazi za utumishi JWTZ mpaka kufikia kuwa Mnadhimu Mkuu, na alistaafu akiwa na cheo cha Luteni Jenerali.

Sikiliza mahojiano aliyofanya na Azam TV kipindi cha Zumari kujua historia yake, na kilichotokea Seychelles mwaka 1981.

..anaitwa Abdulrahman Amiri Shimbo.

..alikuwa ktk kikosi cha Jwtz kilichotumwa Seychelles kufundisha jeshi la visiwa hivyo.
Upande wa pili wa coin(any story ina two side)ni tofauti kabisa jinsi wanavyotufanya tuamini kuhusu hii issue, PM wa kwanza aliondolewa madarakani kwa msaada wa jeshi letu ambalo liliwapa mafunzo(about 70 of them) PM Rene akaingia madarakani na kubadili mfumo wa kisiasa wa kisiwa hiki ikiwa ni pamoja na kukifanya kiwe chenye mfumo mmoja wa chama cha kisiasa.

PM aliyeondolewa akaamua kujaribu kurudi madarakani kwa kutumia mercenaries na plans zilivurugika pale Airport baada ya staff mmoja wa custom kugundua kuna weapons na aka rise alarm, mercenaries wakazidiwa na kuteka ndege ya india na kuondoka pale uwanjani baada ya brief engagements.

Wanajeshi wa Tanzania walipelekwa kuimarisha and to secure usalama wa airport na walifika pale wakati uwanja upo shwari.

Muda umepita hopes jeshi la Tanzania wata declassified information za hii operation ili ukweli ujulikane
 
..asante sana kwa kuchangia mada hii.

..Stori uliyoeleza nimewahi kuisoma ktk sources mbalimbali za kwenye mtandao.

..Naamini pia kiongozi wa mercenaries waliovamia Seychelles ameandika kitabu.

..lakini hii ni mara ya kwanza kukisikia kisa hiki toka kwa kiongozi wa ngazi ya juu ktk Jwtz kama Lt.Gen.Shimbo.

..Ni muhimu sana kwa Watz kueleza upande wetu wa HISTORIA. Tusiache watu wa nje watusemee mambo yetu.

..Shimbo na wenzake waliotumikia Seychelles ni MASHUJAA ambao mchango wao unapaswa kupigiwa mfano.

..Tunaye mwanachama mwenzetu Echolima ambaye alihudumu Seychelles.

NB:

..Shimbo pia amezungumzia kikosi cha Tz kilichokuwa Comorro miaka ya 1980.
 
Umeelezea vyema katika mchango wako wa mada hii,wote tunahitaji kujua UKWELI sio kuombiwa UONGO,na hakuna tabia mbaya kama UONGO,na ni vema sisi wenyewe tukawa wakweli na always ukweli utatuweka huru;
 
ni luteni jeneral ndomba, ndio alikuwa na tuhuma izo za kula hela za wajeda kaka kustaafishwa na jpm kabla ya muda wake wa utumishi jeshi kufika

..mpaka mnadhimu mkuu anatafuna pesa za wanajeshi, waziri wa ulinzi, katibu mkuu wizara, mkuu wa majeshi, watakuwa wapi?
 
Upande wa pili wa coin(any story ina two side)ni tofauti kabisa jinsi wanavyotufanya tuamini kuhusu hii issue, PM wa kwanza aliondolewa madarakani kwa msaada wa jeshi letu ambalo liliwapa mafunzo(about 70 of them) PM Rene akaingia madarakani na kubadili mfumo wa kisiasa wa kisiwa hiki ikiwa ni pamoja na kukifanya kiwe chenye mfumo mmoja wa chama cha kisiasa.

PM aliyeondolewa akaamua kujaribu kurudi madarakani kwa kutumia mercenaries na plans zilivurugika pale Airport baada ya staff mmoja wa custom kugundua kuna weapons na aka rise alarm, mercenaries wakazidiwa na kuteka ndege ya india na kuondoka pale uwanjani baada ya brief engagements.

Wanajeshi wa Tanzania walipelekwa kuimarisha and to secure usalama wa airport na walifika pale wakati uwanja upo shwari.

Muda umepita hopes jeshi la Tanzania wata declassified information za hii operation ili ukweli ujulikane
Sasa hao waliokufa walikufa kwa presha au
 
Ushujaa wa maafisa na wapiganaji wetu kule ushelisheli its a debate for another day,nini kiliwapeleka kule na je ni haki kuingilia na kusaidia kupindua serikali halali ya nchi nyingine ni ushujaa?binafsi nitajitahidi kupata both side of story ili ukweli niujue.

..mimi naamini jwtz walikwenda Seychelles na Comorro ili kulinda usalama wetu haswa ukanda wa bahari ya hindi.

..ukifuatilia taarifa za Zanu Pf utakutana na habari kwamba kulikuwa na meli za Tz zinazosafisha wapiganaji toka Mozambique kuja Tanzania kwa mafunzo.

..pia kuna tukio la makomando wa Afrika Kusini kufika Dsm kwa kupitia majini. Nadhani walitega mabomu.

.
 
Ahsante JokaKuu

Mtangazaji alimkatiza bila kumpa nafasi ya kueleza zaidi kuhusu Seychelles baada ya jaribio kuzimwa. Askari walitoka wapi na walikuwa na lengo la kumweka nani madarakani?
Wakati huo Albert Renne kama sikosei alikuwa wapi?

Pili, mtangazaji hakumpa nafasi ya kueleza amefanya kazi na akina nani.

Nadhani mwaandaji hakuwa na background ya kutosha.
Kwa CV ya shimbo hapo tungewasikia akina Sarakikya, Twalipo, Kiaro n.k.

Mtangazaji angeandaa sehemu ya pili na ni vema ikiwa Watangazaji watatafuta maoni kabla ya kuhoji watu wazito kama hao.

Mathalani angemuuliza Balozi Shimbo, wakati akiwa CoS kwanini alisema 'jeshi litachukua hatua wakati wa uchaguzi wa kiraia Tanzania"? Kulikuwa na viashiria gani wakati huo n.k
 
Magufuli aliagiza Shimbo arudishwe na next flight from Peaking ubalozini kwa kashfa ya kupiga hela za jeshi akiwa mnadhimu.

Akiwa Seychelles pia akaleta ukurya wa wanajeshi wetu kwa kutishia kutungua ndege ya abiria ya Air India. Rubani akamwambia wewe nani unanambia nisitue, Shimbo akamjibu "mimi mamlaka." Rubani akamwambia kama ni mamlaka unajua kufuata utaratibu sahihi wa mawasiliano ya kuiambia ndege isitue.

Shimbo akahamaki akapanga mawe na magari kwenye run way, akasema "ngoja tumuone atatua vipi." Very unprofessional, very ruthless and puerile, hajali chembe kuhatarisha maisha ya innocent civilians wa kimataifa. Ana bahati Magufuli hakumfunga walipopiga hela na Lugumi.
 
Alirudishwa na next flight kutoka ubalozini Peaking kwa kashfa ya kupiga hela za jeshi akiwa mnadhimu.

Akiwa Seychelles pia akaleta ukurya wa wanajeshi wetu kwa kutishia kutungua ndege ya abiria ya Air India. Rubani akamwambia wewe nani unanambia nisitue, Shimbo akamjibu kikurya-kurya "mimi mamlaka." Rubani akamwambia basi bwana mamlaka fata utaratibu sahihi wa mawasiliano ya kuiambia ndege isitue.

Shimbo akahamaki akapanga mawe na magari kwenye run away halafu akasema ngoja tumuone atatua vipi. Very unprofessional, very ruthless and puerile, hajali hata kidogo kuhatarisha maisha ya innocent civilians wa India na Seycheles. Ana bahati Magufuli hakumfunga walipopiga hela na Lugumi.
Anaonekana Ni fala sana
 
Back
Top Bottom