Majivu ni alama ya nje, tujichunguze ndani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majivu ni alama ya nje, tujichunguze ndani

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kashaijabutege, Mar 9, 2011.

 1. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ninachowaomba wana JF Wakristu ni kujitahidi katika mfungo huu unaoanza leo kuishi maisha yanayo mpendeza Mungu. Ingawa twapashwa kuishi maisha ya utauwa kila siku, udhaifu wetu hutuvuta kutenda yaliyo mabaya. Tumwombe Roho Mtakatifu, atujalie nguvu ya kupigana na maovu ili jamii inayotuzunguka ione uwepo wa Mungu kupitia kwetu.

  La muhimu sio KUFUNGA KULA TU, bali ni kumrudia Mungu katika roho na kweli kwa kusali na kuomba, huku tukiutiisha mwili kwa roho. Tulio na ziada basi tuwasaidie maskini, na hiyo ndiyo funga sahihi.

  Na hapa JF katika post zetu tusitukanane, na hasa tusikejeli au kudharau imani za wenzetu.

  Nawatakia mfungo mwema.
   
 2. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  Ahsante kwa niaba yao maana sioni aliyerespond.
   
 3. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2011
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280

  Mimi hapa jamani.....Kashaijabutege habari za masiku bana....
   
 4. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Hivi yale majivu ni ishara ya nini? sie kanisani kwetu hakuna majivu
   
 5. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2011
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Sawa. Nawe pia kwaresma njema.
   
 6. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #6
  Mar 10, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Nzuri boss wangu. Mfungo huu usile Kaizer nyingi.
   
 7. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #7
  Mar 10, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ni alama ya nje ya toba. Sio ya lazima na hautendi dhambi yoyote kutoyapaka. Unakumbushwa kuwa BINADAMU NI MAVUMBI NA MAVUMBINI UTARUDI. Ni mapokeo ya Wayahudi ya kuonyesha toba kwa nje, mfano walivaa magunia, walijipaka majivu, n.k.

  Ikumbukwe kwamba kujipaka majivu pekee sio toba, ila ni alama ya nje tu. Inatakiwa kujikataa kwa ndani na kukumbuka mara kwa mara kuwa wewe mwanadamu ni VUMBI tu mbele ya MUNGU. Soma Zaburi 90.
   
 8. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #8
  Mar 10, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  ..kweli ni uzuniiii ..kwakifo chake bwan yesuuu...
  tutubu na kuziacha njia zetu mbaya..ehh mungubaba tusaidie..
   
 9. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #9
  Mar 10, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mungu hupenda moyo uliopondeka. Ahsante Rose kwa uamuzi huo.
   
Loading...