Majirani mwizi huku

Mallata Jr.

JF-Expert Member
Feb 24, 2014
461
392
Kuna mwizi aliingia nyumba flani kuiba, mwenye nyumba alikuwa ni hohehahe kupindukia kiasi ambacho hakuwa na shati wala tshirt, maisha yake yote alikuwa anashinda kifua wazi.

mwizi baada ya kuingia ndani akakosa cha kuiba, lakini pembeni aliona chungu kilikuwa na unga wa muhogo. jamaa akaona sio haba bora achukue chochote; akavua shati lake akalitandika chini akasogea kwenye chungu cha unga ili aumiminie kwenye shati alilolitandika chini ili aubebe kirahisi bila kuondoka na chungu, kumbe mwenye nyumba anamuona.

Jamaa alivyogeuza mgongo tu kuchukua chungu, kwa kasi ya umeme mwenye nyumba aliliiba lile shati na kurudi chumbani fasta, mwizi aliporudi alipolitandaza shati hakulikuta, akaguna kwa sauti Mhhh!

Mke wa mwenye nyumba akumuuliza mumewe kama naskia kuna mwizi, jamaa akamwambia hakuna mwizi tulale tu! Mwizi akapiga kelele hapana mwizi yupo mbona shati langu silioni!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom