Majira, Habari Leo na MWANANCHI hii adhabu mliotupa leo sisi Wasomaji wenu mtatupoza na nini?

Jana mwananchi waliandika sengereti badala ya serengeti ,shida tupu

Na huko ndiko kumejaa Degrees na Masters tupu Mkuu lakini angalia huo Upuuzi / Upupu wao wa Kiuandishi. Katika Uandishi wa Habari hakuna jambo muhimu kama Accuracy ya ama Figure au Facts zako kwani hivi vitu viwili ndivyo huongeza Credibility ya Gazeti au Chombo na kinyume chake ni Kudharaulika na Wasomaji / Watazamaji wako.
 
Wametafuta Kiki sasa wanapata walichokitaka kutoka Kwetu. Na inabidi watuvumilie tu Mkuu kwani wengine tulivyoumbwa naturally hatuwezi kuona jambo la Kijinga limetokea halafu tukanyamaza eti kwa kisingizio cha kuwapotezea. Mimi ukipatia nakusifu na tena nitakupamba hadi utakubalika ila ukinikera au ukiharibu tu nitakuwasha hadi uonekane hufai tena. Na kinachoniudhi Mkuu kama siyo kunizidishia tu hasira ni kwamba ukiondoa tu Gazeti za Majira ambalo Waandishi wengi hadi Wahariri wana Elimu yetu ile ya hapa na pale ( Certificate na Diploma ) ila Magazeti ya Habari Leo na MWANANCHI yanaongozwa na Wahariri na Waandishi wa Habari wenye Elimu kubwa kuanzia Degree na Masters Degree kitu ambacho Mimi binafsi sikutegemea kama wangefanya hivi bali nilidhani wao ndiyo wangeongoza kwa kuwa na umakini hasa katka Uandishi wao.

Ndiyo maana huwa sipendi kujiita au kujitapa kuwa Mimi ni Msomi kwani nimegundua Wasomi wa Tanzania wanalingana mno Kiaili na wale wasio Wasomi na pengine yawezekana hata wale ambao huwa tunasema hawajasoma kama Sisi wakawa na akili na upeo mkubwa kuliko Wasomi wenyewe.

Mama Ndalichako una Kazi kubwa na ngumu sana mbele yako na nitangulize tu pole zangu Kwako Professor.
Wanatia aibu sana mkuu.

:Silasc
 
Waandishi wa Tanzania ni makanjanja...... Hayo magazeti nimeachana nayo toka zamani.... JF inanitosha.
 
Kwani idadi halisi ni ipi Mkuu Gentamycine?

Nasikia ni hiyo ya Majira ya 93,000 Mkuu kwani nimejaribu kuangalia Magazeti mengine nayo yameandika idadi hiyo hiyo ya 93,000 ila sijui hawa Habari Leo na wenzao wa MWANANCHI hizo figures zao wamezitoa katika Source wa Mbingu gani.
 
Nadhani sio sawa kufikia conclusion yoyote bila kusoma contents za habari hizo. Inawezekana pia kukawa na maelezo yanayoweza kutoa mwanga kwa nini heading imewekwa hivyo.

Keyword: "Perspective"
 
binafsi waandishi wengi wote wa habari bao ni ndugu, rafiki au watoto wa rafiki zangu wana Sifa zifuatazo:-

1. form four wote walitoa dv iv za 30's

2. wameungaunga cert na dip za hapa na pale

3. hawana mikataba, wanasubiria press tu wakapewe maji na biscuits

nawashauri waige BBC, DW
 
Gazeti la Majira.... Waliofaulu Kidato cha Tano ni 93,000
Gazeti la Habari Leo.... Waliofaulu Kidato cha Tano ni 96,000
Gazeti la MWANANCHI.... Waliofaulu Kidato cha Tano ni 98,000

Vyombo vya Habari na Waandishi wa Habari wa Tanzania mkiwa mnadharauliwa msiwe mnachukia kwani kiukweli huwa mnajitakia wenyewe na nadhani sasa ile Sheria ya Vyombo vya Habari inabidi ianze kufanya Kazi haraka.

Tumewachoka.
jumlisha namba(tarakinmu) za mwisho gawanya kwa 3 hiyo namba jumulisha 90 utapata 'average '
 
Back
Top Bottom