Majira, Habari Leo na MWANANCHI hii adhabu mliotupa leo sisi Wasomaji wenu mtatupoza na nini?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,214
Gazeti la Majira.... Waliofaulu kwenda Kidato cha Tano ni 93,000
Gazeti la Habari Leo.... Waliofaulu kwenda Kidato cha Tano ni 96,000
Gazeti la MWANANCHI.... Waliofaulu kwenda Kidato cha Tano ni 98,000

Vyombo vya Habari na Waandishi wa Habari wa Tanzania mkiwa mnadharauliwa msiwe mnachukia kwani kiukweli huwa mnajitakia wenyewe na nadhani sasa ile Sheria ya Vyombo vya Habari inabidi ianze kufanya Kazi haraka.

Tumewachoka.
 
Hawako makini kabisa

Kumbe na ndiyo maana hata Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mzee Mkapa huko nyuma alishawahi kuwatukana kwa kuwaambia ni Wapumbavu / Mapopoma. Wengi hiyo siku alipowatukana hivi tulidhani kuwa huyo Nguli wa masuala mazima ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano Rais Mstaafu Mkapa aliwaonea au aliwakose adabu lakini kwa huu muendelezo wao wa Upupu / Upuuzi sasa nimeanza kumuelewa Kindakindaki Mzee Mkapa.
 
Hawa ndio wanaadika mafuruku badala ya marufuku...
 
CHA KUJIULIZA NI WAPI WANAPATA DATA HIZO JE NI CHANZO KIMOJA AU!!!!

Nadhani ifike muda sasa Data Journalism ipewe Kipaumbele mno na hata huko Vyuoni Kwao ifundishwe kwa umakini mkubwa kwani dunia ya sasa Wasomaji wengi hasa walio makini na siyo wale Mangumbaru / Hohehahe wanapenda mno kusoma taarifa zenye data za uhakika na za Kutukuka kabisa.
 
kabisaa yaani
Kumbe na ndiyo maana hata Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mzee Mkapa huko nyuma alishawahi kuwatukana kwa kuwaambia ni Wapumbavu / Mapopoma. Wengi hiyo siku alipowatukana hivi tulidhani kuwa huyo Nguli wa masuala mazima ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano Rais Mstaafu Mkapa aliwaonea au aliwakose adabu lakini kwa huu muendelezo wao wa Upupu / Upuuzi sasa nimeanza kumuelewa Kindakindaki Mzee Mkapa.
 
Wao wametoa wapi hiyo habari?

Labda katika Mibichwa yao mibovu. Mkuu wanaudhi mno na nakumbuka hata humu humu JF tumeshawahi kuwapigia sana Kelele kuwa wabadilike kutokana na hili Kosa ambalo kiukweli limekuwa likijirudia sana katika Uandishi lakini masikio yao wameyaweka nta hivyo nadhani sasa ni wakati murua kabisa kwa sisi kuwasema / kuwashambulia kwa nguvu zetu zote humu JF ili waamke na wabadilike upesi.

Ukweli ni kwamba tumewachoka!
 
GENTAMYCINE naona umeamua kuwapandia hewani na kutiririka mubashara hawa jamaa. Ina maana wana vyanzo tofauti vya habari au ni ukosefu wa umakini? Ina maana 3, 6 na 8 ndio imeleta taharuki kiasi hicho?

Kama kawaida yangu Mkuu huwa sipendagi ujinga na simkopeshi Mtu / Watu. Ndiyo maaana kumbe Wakenya na Waganda wanazidharau mno Media zetu Tanzania hadi inafika muda hata tu ukienda huko au ukikutana nao wakikuuliza unafanya Kazi gani unatunga tu uwongo na kuwaambia Mjasiriamali uliyetukuka kwani unaogopa ukiwaambia tu ama Wewe ni Mwanahabari au Mdau wa Habari na Mawasiliano wanaweza hata kukufukuza hapo ulipo au hata kukutemea mate. Wanatudharau mno na nadhani sasa kwa aina hii ya Uandishi wa Habari na Waandishi wetu tulionao Wakenya na Waganda wanastahili na wana haki ya Kutudharau.

Nimekereka sana Mkuu huwezi amini na naona hasira zinazidi tu kunipanda kwa huu Upuuzi / Upupu wao usiokoma.
 
Nimecheka kama kichaa maana nimeshika mwananchi

Umeiona hiyo figure yao lakini inayotuchanganya sisi Wasomaji? Mimi hapa nimeshika Majira, Habari Leo na hilo hilo MWANANCHI kwa jinsi hizo figure zao zilivyonichanganya na hata kunikasirisha natamani tu sasa haya Magazeti yote niliyonayo mkononi mwangu niyageuze kuwa Toilet Papers labda yanaweza kunisaidia kwa upande huo.

Hivi hao Waandishi walishindwa nini tu baada ya hiyo Press waliyokuwapo kumfuata na kuhakiki kwa huyo Authoritarian Source ili wote kwa pamoja hatimaye waje na actual figure ili Magazeti yao yasipoteze Credibility? Ukiwa nao katika Mikutano yao utasikia wanalalamika kuwa Magazeti yao siku hizi hayauzi na hadi kutulaumu sisi Wasomaji wao. Hivi kwa Upopoma / Upumbavu huu uliotukuka kuna Mtanzania gani makini atathubutu kupoteza Hela yake anunue Upuuzi / Upupu wenu?

Yaani leo nyie Wahariri na Waandishi wa haya Magazeti ya Majira, Habari Leo na MWANANCHI mmenikera kupita maelezo.
 
Wanakurupuka mkuu au wanataka kiki

Wametafuta Kiki sasa wanapata walichokitaka kutoka Kwetu. Na inabidi watuvumilie tu Mkuu kwani wengine tulivyoumbwa naturally hatuwezi kuona jambo la Kijinga limetokea halafu tukanyamaza eti kwa kisingizio cha kuwapotezea. Mimi ukipatia nakusifu na tena nitakupamba hadi utakubalika ila ukinikera au ukiharibu tu nitakuwasha hadi uonekane hufai tena. Na kinachoniudhi Mkuu kama siyo kunizidishia tu hasira ni kwamba ukiondoa tu Gazeti za Majira ambalo Waandishi wengi hadi Wahariri wana Elimu yetu ile ya hapa na pale ( Certificate na Diploma ) ila Magazeti ya Habari Leo na MWANANCHI yanaongozwa na Wahariri na Waandishi wa Habari wenye Elimu kubwa kuanzia Degree na Masters Degree kitu ambacho Mimi binafsi sikutegemea kama wangefanya hivi bali nilidhani wao ndiyo wangeongoza kwa kuwa na umakini hasa katka Uandishi wao.

Ndiyo maana huwa sipendi kujiita au kujitapa kuwa Mimi ni Msomi kwani nimegundua Wasomi wa Tanzania wanalingana mno Kiaili na wale wasio Wasomi na pengine yawezekana hata wale ambao huwa tunasema hawajasoma kama Sisi wakawa na akili na upeo mkubwa kuliko Wasomi wenyewe.

Mama Ndalichako una Kazi kubwa na ngumu sana mbele yako na nitangulize tu pole zangu Kwako Professor.
 
Gazeti la Majira.... Waliofaulu Kidato cha Tano ni 93,000
Gazeti la Habari Leo.... Waliofaulu Kidato cha Tano ni 96,000
Gazeti la MWANANCHI.... Waliofaulu Kidato cha Tano ni 98,000

Vyombo vya Habari na Waandishi wa Habari wa Tanzania mkiwa mnadharauliwa msiwe mnachukia kwani kiukweli huwa mnajitakia wenyewe na nadhani sasa ile Sheria ya Vyombo vya Habari inabidi ianze kufanya Kazi haraka.

Tumewachoka.
Bado wanataka uhimili wa 4 nchini hii
Baada ya serikali mahakama na bunge pia wawe wao tutafika tuendako !!
 
Bado wanataka uhimili wa 4 nchini hii
Baada ya serikali mahakama na bunge pia wawe wao tutafika tuendako !!

Kwa ukengeukaji wao huu sitokubali wawe the fourth pillar katika nchi hii mpaka wajitafakari na wajirekebishe upesi sana.
 
Umeiona hiyo figure yao lakini inayotuchanganya sisi Wasomaji? Mimi hapa nimeshika Majira, Habari Leo na hilo hilo MWANANCHI kwa jinsi hizo figure zao zilivyonichanganya na hata kunikasirisha natamani tu sasa haya Magazeti yote niliyonayo mkononi mwangu niyageuze kuwa Toilet Papers labda yanaweza kunisaidia kwa upande huo.

Hivi hao Waandishi walishindwa nini tu baada ya hiyo Press waliyokuwapo kumfuata na kuhakiki kwa huyo Authoritarian Source ili wote kwa pamoja hatimaye waje na actual figure ili Magazeti yao yasipoteze Credibility? Ukiwa nao katika Mikutano yao utasikia wanalalamika kuwa Magazeti yao siku hizi hayauzi na hadi kutulaumu sisi Wasomaji wao. Hivi kwa Upopoma / Upumbavu huu uliotukuka kuna Mtanzania gani makini atathubutu kupoteza Hela yake anunue Upuuzi / Upupu wenu?

Yaani leo nyie Wahariri na Waandishi wa haya Magazeti ya Majira, Habari Leo na MWANANCHI mmenikera kupita maelezo.
Mmenifanya ninunue majira sijawaelewa bado kwann figure ziko tofauti je ni kwamba hawajapata matokeo halisi au wameandika ili waonekane wa kwanza kuandika matokeo au imekuwaje magazeti tunayoamini sio ya udaku wanatufanyia hivi
 
Back
Top Bottom