Majira: Gazeti Huru la Kila Siku | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majira: Gazeti Huru la Kila Siku

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ng'wanangwa, Oct 8, 2010.

 1. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Kama Mtanzania mwenye akili timamu, ninayetaka mabadiliko, mwenye utashi na hamu ya kuchagua viongozi kwa kufuata sera (badala ya ukada na ushabiki wa kijinga), ninapenda kulipongeza gazeti la majira kwa kupuuza utafiti haramu wa uliotangazwa jana na mmoja wa watu wanaojipendekeza kwa Kikwete Bwana Benson Bana.

  Nimeperuzi gazeti la Majira la leo Ijumaa tarehe 8 Oktoba 2010 na kugundua kwamba hakuna mahali, japo aya walipoandika kuhusu REDET na uchafu wao unaopotosha jamii.

  My Take:
  Majira la leo limejipambanua kuwa chombo huru cha habari ambacho kinajua thamani ya habari kwa jamii. Kwa namna siasa za Tanzania zilipofikia sasa, ni mwenda wazimu tu atakwambia Kikwete na Slaa wanapishana kwa margin kubwa kiasi hicho, hata kama Kikwete atashinda. Sijui magazeti yaliyochapisha uzushi wa REDET yameadika nini, lakini nadhani msimamo wa majira unastahili kuigwa.

  Kikwete hawezi kushinda kihalali uchaguzi huu. Njia itakayomuokoa ni kuiba kura. Kwa hiyo Bana na vibaraka wenzake wanaendelea na harakati zao za hovyo za kutaka kuendelea kusaidia kutawazwa kwa watawala wala rushwa na mafisadi kwa faida ya familia zao, wakiacha Watanzania wanateseka na umasikini. Machozi tunayotoa Watanzania masikini lazima yatawachuruzikia hata siku ya kufa kwenu enyi vibaraka wa mafisadi. Huo ni ubinafsi na ubaguzi, hata kama Bwana Bana anajipendekeza. Utafiti wao unapalilia harakati za kuiba kura ili uje utumike kuwa ni ushahidi kuwa walifanya utafiti.

  Mlaaniwe na hila zenu REDET!!!
   
Loading...