Majipu yameisha, mbona nchi haisongi mbele?

Malata Junior

JF-Expert Member
Nov 29, 2011
3,104
2,549
Tuliaminishwa kwamba nchini yetu imegubikwa na umasikini wa kipindukia kwa sababu ya 'majipu' yaliyokuwa yameenea serikalini,taasisi za umma na sekta binafsi.

Tukaambiwa ili kuleta mabadiliko ni lazima majipu hayo yatumbuliwe.Wenzetu UKAWA wakatuambia kutumbua tu bila kurekebisha mfumo unaosababisha majipu hakutaleta mabadiliko yoyote lakini mtumbuaji na mashabiki wake wakawabeza.

Leo hii majipu yanaelekea maisha lakini hatuoni hata dalili za nchi kusonga mbele badala yake hali inazidi kuwa ngumu!
 
Majipu yaliyobaki yameota sehemu za siri kwa hiyo utumbuaji wake unampa maumivu makali sana mgonjwa. Sasa hivi amepewa dawa za kupunguza maumivu kwanza.
Na mengine inasadikika yamemwambukiza daktari mwenyewe. Sasa wataalamu wanafanya uchunguzi ili kubaini kama daktari alikuwa nayo muda mrefu au alipata maambukizi wakati akifanya matibabu.
 
Ivi mapato ya TRA miezi hii miwili ya mwisho yamekua kiasi gan vile ??

Utanganyika Gharama...acha tuone. Tehe
Hawataki tena mambo ya kutangaza mapato 'yanavyopanda',wamekusanya vimadeni vimeisha ...hawana ubunifu wala lolote jipya,sasa hivi itaanza kushuka maana bandarini walikokuwa wanategemea mapato yameshuka kwa 46%.
 
Back
Top Bottom