Namwombea Mh Rais Magufuli kwa mwenyezi Mungu ili aendelee kutumbua majipu na vijipu na hasa wezi wa mali za umma, nchi yetu siyo shamba la bibi. Naomba asimuonee haya mtu yeyote iwe kwa nafasi, rangi, dini, kabila, utaifa wake n.k, pia asionewe mtu katika zoezi hili. Na mwisho niombe zoezi hili lisiishie njiani na hasa katika utawala wake, maana akiishia kwa baadhi tu inaweza ikatafisiliwa tofauti. Mh timiza hilo, maana ndio ndoto za Watanzania tulio wengi na tupo nyuma yako.