Majini yamepungua umaarufu siku hizi, Unakumbuka story gani miaka ya nyuma mashuleni au mtaani..?

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Miaka ya nyuma, saa Saba mchana ulikuwa ni muda wa majini
Kuna mti ulishawahi kuanguka mguu wa Kuku, wote mbio eti pale palikuwa na majini wanakula Kuku,
Kuna shule ya msingi nimewahi kusoma Choo kimoja chenye rangi nyeupe kilitengwa eti kina majini
Kuna waliokuwa wanawahi shule asubuhi na kusema eti wamekutana na jini refu sana njiani
Kuna bibi mmoja mtaani njia ya nyumba yake tuliaminishwa kwenye miembe yake ukipita usiku unakutana na mtu mrefu saana ukileta ubishi hata vibao unakula. Nakumbuka siku nikipita pale mwenyewe hata kama ni mchana najikuta nimetoka nduki Bila kujua kwa nini.

Kwa nini miaka ya chini ya 2000 majini yalikuwa maarufu kuliko siku hizi...

Umewahi kukutana na stori hizi au live na hawa wadudu...
 
Tulikua tunaambiwa ukisalimiwa na mtu usiku jifanye ujaskia anaweza kua jin ukiitka tu anajua umemuona pia story za mayai viza njia panda zilikua nyingi bora ata hayo mambo skuiz yanapotea
 
Mguu wa kuku kuanguka toka kwenye mti nahisi kunguru aliubeba tu amna jingine
Yes enzi hizo shule ata baathi ya vyoo tulikuwa atuingii kisa eti kuna majini
Kweli ukute mwewe alikuwa anamalizia Kuku aliyemuiba sehemu. Imani potofu mbaya sana
 
ha ha ha kufika 2025 waganga wa kienyeji nao wote watapotea.. watu watajua ukweli kwamba uchawi haupo ni stori tu
Tunakoelekea wachawi na majini zitabaki stori au usumbufu wa wachache wanauhusudu au kama vipi waje huku online maana jamii inahamia huku yote.
Ila vijijini ni balaa
 
Mkuu,kutonakana na wataalam wa dawa za miti kupungua,hasa kutokana na wanaozijua kutorithisha vizazi vyao,uchawi mkubwa uliobaki ni wa majini,

Tunakoelekea huko ni hatari zaidi kwa sababu wataalam wa tiba za ukweli za asili wanapungua,na hawarithishi utaalam huo kwa vizazi vyao,lakini wachawi ni sharti amrithishe mwanae au nduguye ,kwa hiyo wachawi watazidi kuwa wengi kuliko wataalam wa kuutibu.

Rais 2020,jichawi ,mshana jr ,MziziMkavu ,Mtu mzito
 
We Jamaa umenikumbusha mbali sana, Shuleni kweti kuna Choo, tulikuwa hatukitumii, tulikuwa tunaambiwa ukienda ukianza kujisaidia tu unasikia sauti ya mtoto inalia ng'aa ng'aa
 
Kuna miti huwa ina harufu.Mfano mikaratusi na mingineyo.
hata shule ikiwa karibu na pori au vichaka, kenge, nyoka au chatu, hasa nyoka huwa wanatoa harufu kama ya pilau/wali/mihogo hilo pia linawezekana.
Cha kushangaza kwa nini majini hao wapende kutisha watoto wa shule ya msingi wasiojitambua, au nao hawapendi elimu.
Au tuko nyuma kielimmu kwa sababu ya majini :D:D:D:D
 
Muda huu nayo Yanasoma tu huu uzi ili yaanze kivingine ila haya comment na yakicomment basi yataweka rangi nyekundu
Sisi shuleni kwetu tulikuta ugali na damu chooni
 
Zaman sana pale makambako shule ya msingi an ukienda choooni unasikia mtu kama anaakaanga samaki hv mala haruf ya pilau mala vishindo vikubwa kwakweli sijawahi kuwahi shule mm
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom