Majini, Mashetani, Mapepo na Mahayawani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majini, Mashetani, Mapepo na Mahayawani

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Sumbalawinyo, Aug 4, 2010.

 1. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Hivi kuna tofauti gani kati ya Majini, Mashetani, Mapepo na Mahayawani?
  Naomba msaada wenu ndugu wataalam.
  Maana kanisani utasikia wakikemea pepo toka, Masheikh utawasikia wanafukuza majini.
  Yaani vinanichanganyachanganya/
   
 2. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,919
  Likes Received: 608
  Trophy Points: 280
 3. w

  wyclefmore Member

  #3
  Jul 8, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  maneno hayo yote yana maana moja ila inategemeana na mahali.wabantu huita mapepo,majini au mizukan.k waarabu huita masheytwain.maruhani au majini.lakini kitheolojia yote yana maana moja tu kuwa ni roho chafu zinazoyokana na shetani.
   
 4. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #4
  Jul 8, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160

  Majini
  ndio hao wanajulikana kwa majina mengine kama vile Mapepo, demons, Nephilim na majina mengine kadhaa wa kadhaa... they have no physical bodies.

  Wameitwa MaJINNI kwa sababu ya kutokuonekana kwao na watu, na hii ni kwa sababu kila kisichoonekana kwa jicho la binadamu katika lugha ya kiarabu jina lake hutokana (hutoholewa) na herufi mbili hizi; Jiym na Nuun.


  Mashetani: Hili neno linatokana na jina Shetani, na hii ni sifa mbaya na si jina.

  Mahayawani: Hayawani حيوان (hayawani) neno hayawani peke yake lina maana ya Mnyama.

  Ila wakati mwingine utumika kwa kuwapa watu sifa mbaya, sifa ya unyama, ndio utasikia mtu anaitwa Hayawani, wakimaanisha kuwa huyu mtu ni Mnyama. Mwenye tabia ya matendo machafu, unyama, Mazimbwezimbwe, ujinga, ukatili, n.k

  Kuhusu demons, fungua viumgo hivi:

   
 5. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Majini au mapepo ni viumbe ambavyo havionekani kwa macho, ni viumbe kama malaika isipokuwa majini na mapepo yalifukuzwa mbinguni pamoja na shetani baada ya kuasi, na yalitupwa duniani yakisubiri siku ya mwisho ya hukumu.

  Shetani na majini, wanajua kabisa kuwa jehanum ya moto ipo kwa ajili yao, ndiyo maana wanafanya kila mbinu wasiingie peke yao huko jehanum, shetani ni mwongo, laghai anawatumia sana wachawi, waganga wa kienyeji, wasoma nyota kupandikiza majini, kuiba nyota yako ya mafanikio, kuchukua watu misukule nk.

  Kuna aina nyingi za majini baadhi yake ni kama:-

  1) Murafari - hili ni jini linalozuia mafanikio ya kupata fedha, mafanikio ya elimu nk.
  2) Latifu - hili jini linaloleta ufukara, mateso, hata ukipata pesa matumizi yake yanakuwa ni hovyo
  3) Jahari - Jini anayetumiwa kuiba mali na kuzuia biashara kustawi
  4) Hasinani - jini hili ni la fujo, ulevi wa pombe, bangi na dawa za kulevya
  5) Jube - jini hili linasababisha utasa
  6) Subiani - jini la ajali, linasababisha wanawake kutokupata siku zao, na kunyonya damu za akina mama siku zao za hedhi ambapo wanapata maumivu makali sana.
  7) Sumil - jini hili huangamiza mimba changa
  8) Waidadat - jini hili husababisha wanaume kuvaa hereni kusuka nywele na kutoga masikio.
  9) Alibadiri - jini la kifo, likikupata kifo hutokea wakati wowote.
  10) Anzura - Linawazuia vijana wa kike na kiume kuolewa/kuoa
  11) Maimuna - linawakamata wanaume wenye ndoa zao hadi ndoa inavunjika
  12) Makata - linasababisha vifo vya mfululizo kwenye familia
  13) Faziur - jini la maandishi. Unaletewa barua ukiisoma tayari umelikwaa
  14)Subha - jini hili linasababisha mtu kuwa na kiburi sana na kujiinua.
  15) Maulan - jini linalofanya watu kuwa kichaa, au mtu ananuka wakati wowote
  16) Al-maul - jini hili linamfanya mtu kuwa ombaomba
  17) Zuhura au Zohari - Jini la fujo
  18) Araba - Jini hili linafanya mtu apende sana ubani
  19) Farkh - jini hili linatumwa hasa kwa wakristo kuangalia kama ana kinga (Wokovu)
  20) Baradi - jini hili likikupata basi ndoa yako ni lazima itavunjika.
  21) Shamsu - jini hili huvaa umbile la binadamu kwa sura yoyote.(sasa hivi mitaani majini haya yapo mengi sana)
  22) Abuni - jini wa hasira
  23) Kaimu - jini la kutambua nyota za watu
  24) Tajuruni - jini la utajiri wa kichawi - ni lazima utoe kafara ya mwanao, mkeo au kufanya tendo la ndoa na mama yako mzazi
  25) Al-taliki - jini hili linapoteza watu katika mazingira ya kutatanisha
  26) Naluju - linasimamia lugha
  27) Janatusi - linatumwa alfajiri kabla ya adhana kuleta usingizi kwa Wakristo wasifanye sala
  28) Riyaron - jini hili linamfanya mtu afanye kila kazi peke yake
  29) Zaitun - Jini hili linasababisha wasichana kuwa na maringo
  30) Ruyati - jini linalosimamia ndoto mbaya
  31) Al-rahabu - jini linalosababisha hitilafu ya umeme
  32) Hadharaji - jini hili linafanya kazi ya kukata kichwa cha mtu ili wapate damu
  33) Anazihaji - jini hili ndilo linachukua roho yako ukifa kwenye dhambi
  34) Nghruk - linasababisha maafa
  35)Munkara - jini la makaburini
  36) Takadhuru - jini linaloleta mali za masharti.
  37) Rabindi - jini la Waislamu pekee yao ili wafanye fujo.
  38) Balishebe - jini la magonjwa yasiyopona
  39) Sajiduri - jini linalokusaidia kupata pesa, kisha zinapotea kwa haraka
  40) Rumiran - linasimamia uwongo
  41) Lairlihabi - linasimamia hofu, kutojiamini na kukata tamaa
  42) Rohani - jini la mateso na fujo
  43) Betrah - jini hili linasimamia mapambo, kwa mwanamke huwa anajipamba isivyo kawaida, halikadhalika mwanaume
  44)Hanshari - linatumiwa sana na waarabu kulinda maduka yao
  45) Walihuni - linazunguka nyumba likilinda biashara
  46) Kurasih - jini la kupoteza fahamu
  47) Tarik - huondoa amani nyumbani, kazini. Linafanya watu wasielewane
  48) Atha - mungu wa kiarabu wa kuabudu sanamu
  49) Munakir - linapoteza watu kimiujiza
  50) Malik - jini la kumiliki biashara
  51) Ghatabu - jini la kulainisha macho wa wanawake. Wanakuwa wanarembua
  52) Khatuh - jini la uchawi wa kuchukua kucha, nywele na nguo za ndani
  53) Fanken - jini hili linasimamia mtu kuzunguza kiswahili cha pwani
  54) Zamzam - jini la marashi na kusimamia mikataba ya imani. Mkristo anaposilimishwa basi hutupiwa jini hili kupofushwa akili yake.
  55) Mukitala - linatumwa kuangalia kinga za watu
  56) Laufili - jini la uvivu
  57) Al-khah - linakula damu iliyoganda
  58 Abasaa - jini la hasira wivu na jeuri
  59) Aherumi - jini la homa za mara kwa mara
  60) Muba - jini la maradhi ya kuambikiza
  61) Kamariram - jini hili linatoa kinga kwa majambazi
  62) Zubiran - jini la uongo na uzushi
  63) Abadi - Jini la wizi, umalaya na ujambazi
  64) Muzamili- jini la matambiko ya kiarabu
  65) Ruhadi - jini la wizi, umalaya na umasikini
  66 Usuran - jini la wizi, umalaya, ujambazi na umaskini
  67)Tubuyali - jini hili linamfanya mtu kuiba vitu vya ndani ya nyumba. Haibi nje ya nyumba
  68) Zirach - jini la wizi, umalaya, ujambazi na umaskini
  69) Ashuran - jini la utasa na maradhi ya akina mama

  Kinga ya majini haya ni nyepesi ni KUOKOKA na kusimama katika neno la Mungu. Kama unayo dalili yoyote iliyosababishwa na majini hayo hapo juu na umeokoka, taja jina la hilo jini, ni lazima litaitika, kisha liwashie moto.

  Kama hujaokoka usiyarushie mawe au moto yatakuumiza. Mwuone kiongozi yeyote wa kanisa akuongoze sala ya toba, kisha anza kuwasha moto, hakika yatakimbia na kuacha biashara, kazi, ndoa, na watoto wako huru.
   
 6. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #6
  Jul 8, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Majini na Shetani, ni nini tofauti yake?

  Math. 16: 22-23
   
Loading...