Majini, Mapepo, Maruhani, Uchawi na Kitimoto/Nguruwe; ukweli ni upi?

MwanajamiiOne

Platinum Member
Jul 24, 2008
10,470
6,562
Wadau Habarini,

Samahanini kama nitakuwa nimewakwaza but jana usiku nilikuwa nasikiliza mahubiri katika Radio moja, mhubiri alikuwa anaelezea vyakula ambavyo binadamu haturuhusiwi kula, mmoja wapo ni huyu mkuu wa meza bwana Kitimoto. Nikakumbuka kuwa ni vitabu vyote vinakataza huyu mkuu asiliwe.

Lakini ghafla likanijia wazo hivi si wanasema (Sijui kina nani nasikiaga tu) kuwa huyu mkuu wa meza majini hayampendi kabisa na kuwa huwa anayakimbiza?

Nikajiwa na wazo tu kwa nini tusiruhusiwe ili tujihami na majini? Au ndugu zetu wenye majini (nilishawahi kusikia kuwa wapo wenye majini mahaba, n.k wanapandisha yanadai sijui kiti wao alete nini na nini sijui) Kwa nini hawa watu wasiwe wanapewa mkuu wa meza kama tiba ya kuyaondosha badala ya kuyapunga tu yatulie?

Hebu nisaidieni wajameni!
 
Afu wewe? Umeamkia upande upi leo?
Vitabu vyote vipi?
Mi cha kwangu mbona kinaruhusu?
Ah nimipitiwa hapo nisamehe- vitabu vya dini mbili ya kikristo na kiislamu lol my bad.

Hata sijui mwayego mie leo naona nimeamka nimesimama. Kama sio mimi vilee!
 
9. Hata siku ya pili, walipokuwa wakisafiri na kuukaribia mji, Petro alipanda juu darini, kwenda kuomba, yapata saa sita ya mchana;
10. akaumwa na njaa sana, akataka kula; lakini walipokuwa wakiandaa, roho yake ikazimia,
11. akaona mbingu zimefunuka, na chombo kikishuka kama nguo kubwa, inatelemshwa kwa pembe zake nne hata nchi;
12. ambayo ndani yake walikuwamo aina zote za wanyama wenye miguu minne, na hao watambaao, na ndege wa angani.
13. Kisha sauti ikamjia, kusema, Ondoka, Petro, uchinje ule.
14. Lakini Petro akasema, Hasha, Bwana, kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu au najisi.
15. Sauti ikamjia mara ya pili, ikimwambia, Vilivyotakaswa na Mungu, usiviite wewe najisi.
 
9. Hata siku ya pili, walipokuwa wakisafiri na kuukaribia mji, Petro alipanda juu darini, kwenda kuomba, yapata saa sita ya mchana;
10. akaumwa na njaa sana, akataka kula; lakini walipokuwa wakiandaa, roho yake ikazimia,
11. akaona mbingu zimefunuka, na chombo kikishuka kama nguo kubwa, inatelemshwa kwa pembe zake nne hata nchi;
12. ambayo ndani yake walikuwamo aina zote za wanyama wenye miguu minne, na hao watambaao, na ndege wa angani.
13. Kisha sauti ikamjia, kusema, Ondoka, Petro, uchinje ule.
14. Lakini Petro akasema, Hasha, Bwana, kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu au najisi.
15. Sauti ikamjia mara ya pili, ikimwambia, Vilivyotakaswa na Mungu, usiviite wewe najisi.

Mkuu jioni nitafute. Una mzigo wako wa kilo moja na ndizi mbili. Vipi unapendelea rosti au ikaushwe? Kachumbari iwekwe pilipili? Hebu kagua senksi niliyokugongea hapo afu utabasamu kidogo!~
 
Ah nimipitiwa hapo nisamehe- vitabu vya dini mbili ya kikristo na kiislamu lol my bad.

Hata sijui mwayego mie leo naona nimeamka nimesimama. Kama sio mimi vilee!

Hat hapo umekosea, sema Agano la Kale na Qurani ndio tutakuelewa. Peter aliwekewa wanyama kila aina katika ndoto yake wakati Mungu anamwandaa kumpokea asiyekuwa Myahudi ili aombewe. Petro alipouliza kwamba hawezi kula kitu najisi japo ana njaa sana aliambiwa "Usikiite najisi kilichobarikiwa na Bwana....."

Paulo Mtume amechallenge pia watu wanaosema "usiguse, usionje ..... kwa maana vitu hivyo ni vitu viharibikavyo..." Hiyo ni kwa Wakolosai alipokuwa anawaandikia akiwashangaa wamerogwa na nani.

Hata kama unakula chungwa, usipoliombea baraka za Mungu unakula chungwa haramu. Hata chai uliyokunywa asubuhi ya leo kama hukuiombea baraka, umeinywa haramu. Nani anayekuja kutengua Agano Jipya la Mungu kwa Wanadamu, Ni nani Mkuu kuliko Mungu aliyesema "Huyu ndiye Mwanangu Mpendwa, msikilizeni yeye...."

Tunafanya dhambi nyingi kuliko tunavyofikiri, ndio maana Mungu anaangalia moyo wa binadamu na kuuona mchafu siku zote, hakuna aliye safi hata mmoja, wote tumeoza pia. Mlokole anajiita yeye, Mungu hamwiti hivyo. Walio wake Mungu anawajua Mungu mwenyewe. Binadamu tumechagua vitu vya kuviita "dhambi" lakini tunasahau kwamba yeye aliyesema USIIBE ndiye aliyesema USIMSEMEE JIRANI YAKO UONGO, na ndiye aliyesema UKIMWONA MWANAMKE KWA JICHO LA KUMTAMANI - TAYARI UMEZINI NAYE. Ni nani basi atakayeweza kuokoka? Wanafunzi wake Yesu walimuuliza alipomfananisha tajiri na ngamia (kamba) kupita tundu la sindano. Hakuna lisilowezekana kwa Mungu, hata Paulo alisema alikuwa daima anapigana vita vizuri vya imani, isijetokea kwamba anawapeleka wengine Mbinguni na yeye anabaki.

Kiti moto unakula na kisha unavitoa ****** kama uchafu au porini kama mbolea ya nyasi. Kimwingiacho mtu sio najisi bali kimtokacho. Moyo wa mtu ndio store ya unajisi machoni pa Mungu. Acha tule kiti moto, Bwana alipokiumba akakiona na tazama, kimekuwa safi. Agano la Kale lilikuwa kiboko cha wagumu wa mioyo, lakini Mungu alipoona wateule wake wengi wanakwamishwa kumfikia kwa sababu ya sheria za Torati, akaamua kuleta sheria mpya kuhuisha uwezekano wa watu wengi zaidi kuingia Mbinguni angalau through a moderate pass mark - aliruhusu sheria ya Upendo kutawala, ndiyo sheria kuu kumpenda bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa akili zako zote na kwa mwili wako wote. Ya pili inayofanana na hiyo, ni kumpenda jirani yako kama nafsi yako. Aliipiga muhuri amri kuu hiyo Bwana Yesu mwenyewe kwa mhuri wa damu yake mwenyewe, maana kwa kupigwa kwake SISI SOTE TUMEPONA. Hakuna cha Myahudi wala mnyalukolo wala Nshomile au Msokile.
 
Mkuu jioni nitafute. Una mzigo wako wa kilo moja na ndizi mbili. Vipi unapendelea rosti au ikaushwe? Kachumbari iwekwe pilipili? Hebu kagua senksi niliyokugongea hapo afu utabasamu kidogo!~

Chrispin, ni kwa nini mara nyingi lazima tumle mkuu wa meza na ndizi?
 
Aksante Leka kwa kunifunulia sikuwa na ufahamu huu kuwa ni agano la kale ndilo lililokataza na jipya linaruhusu. Uvivu hii wa kusoma bibilia -Shame on me!!

Sawa sasa nimeelewa kwa upande wa kikristo.

Swali langu sasa ni je ni kweli kuwa nguruwe na majini/maruhani havipatani? Kama ni kweli basi naomba ndugu zangu waislamu wanieleweshe zaidi hapa juu ya hili

nina swali kwa ndugu zangu waislamu (Tafadhali naomba msinielewe vibaya ) Nahitaji kuelimishwa juu ya hili.

Kitabu kitukufu cha dini ya kiislamu kinakataza wao kula huyu mkuu wa meza, kama havipatani na majini na maruhani hawaoni kama ni njia nzuri ya kufukuza majini ambayo yanawatesa wengi katika jamii zetu?-

mwanajamiione naona sasa unaanza kukosa adabu, Nani kakwambia waislamu hawali? ni kitabu tu kinakataza lakini wao wanakula kwenda mbele, wanadai mkuu wa meza ni tiba ya nanihino. Kama unabisha pitie bucha za kitimoto kabla na wakati wa mwezi wa ramadhani uone mauzo yanavyoshuka wakati wa ramadhani.

Halafu inamaana waislamu na majini/maruhani ni dugu moya? kama siyo kwa nini umehusianisha?
 
Hata mimi nashangaa........... sijui kwa nini hatuli na TAMBI

na huwa nasikia pilau ya mbuzi, kuku, ng'ombe. Lakini sijasikia ya Mkuu wa Meza. This is not fair. au pilau ya Mkuu wa Meza ni ghali sana ni wachache sana mnaoweza kuimudu? Wapemba tu na vibakhresa vichache !!!!!!!!!!tehe tehe tehe heheheeee
 
Dr.isaack ndodi kayajibu yote hayo jumanne kwa kunakiri marco 3(11) na kuhitimisha kuwa kama majini yamesomba nguruwe wakiwa hai hadi mtoni watashindwa vipi kuingia sehemu ambayo nguruwe wameshakufa?tena kasema bado ile zawadi ya nissan ipo palepale kwa atakayemtolea andiko katika biblia kuwa nguruwe karuhusiwa kuliwa.huyu ndodi ni mchungaji wa kondoo za bwana aliye hai.
 
Hoja haijajibiwa na kwa vile sina authority kwenye hili, nafuatilia tu kwa ukaribu.

By the way huyo Ndodi alizungumziaje kisa cha Petro alivokuwa na njaa, akaambiwa ale wote wenye miguu MINNE< na watambaao, na ndege?

Pili, wale mapepo waliowaingia nguruwe, nikiangaliwa ki mkuktadha ni kwam vile hao nguruwe walikuwa pale wakati huo, ingewezekana ikawa kondoo, mbuzi, ng'ombe etc, je na wenyewe tungewajengea hoja hiyo? Huyo kasoma theolojia ya wapi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom