Majini hupenda heshima na ni wakorofi sana

Mkuu Mzimu wa Kolelo angalau uwe unajaribu kutofautisha herufi
"L" na "R" najua zinakutatiza lakini jaribu, mwishowe utazoea.
pamoja sana mkuu nitajitahidi zaidi 7bu hapo mwanzo kabisa ilikuwa shida lakini kadiri muda unavyokwenda kidogo afadhari si unajua wengne uandishi sio fani yetu
ni kweli L na R wengi zinatutatiza
pamoja sana mkuu
Usisite kurekebisha unapoona makosa kwenye uandishi au maelezo au post
najisikia faraja kusahihishwa bila kejeri pale ninapokosea
 
"Wakristo wanasema" ukiunganisha maneno unapoteza maana.
YESU sio Mungu. YESU ni mwana wa MUNGU na ameketi mkono wa kuume wa MUNGU.
Bora Leo umekubali kwamba "YESU NI MWANA WA MUNGU" Na pia hata mimi na wewe ni wana wa Mungu. Kitendo cha MUNGU kutuumba sisi inatosha kabisa kuwa baba yetu. Haijalishi hata kama hajazaa.
BIBLIA INASEMA "SISI NI MIUNGU MIDOGO" tulio tokana na MUNGU
Kuhusu masihi ni sawa kuwa YESU NI MASIHI ALIYEANDIKWA NA MANABII WA KALE KWAMBA ATAKUFA KWA AJILI YA DHAMBI ZA BINADAMU..na ilitimia kama ilivyoandikwa katika TORATI.
Ni MWOKOZI wa maisha YETU Kwa sababu kwa KUPIGWA KWAKE SISI TUMEPONA NA KWA JINA LAKE MAPEPO YATATUTII..
Na ndio maana tunaomba katika UTATU mtakatifu.
MUNGU BABA, NA MWANA NA ROHO MTAKATIFU.
Hii habari ya utatu Umeipata wapi?
Manake hata hili neno UTATU Mtakatifu Kwenye BIBLIA HALIMO!!
 
ni kweli hayo yote nilioleza asilimia kubwa ni ya masimulizi ingawa machache nimeyashuhudia
kilichotokea hapo ni IMANI na kila mtu ana IMANI yake hivyo si lazima watu wote wakubaliane na mimi jinsi ninavyojua au nilivyoeleza
kwa mfano nikisema ni simulizi kwa maana nimejifunza kupitia vitabu mbarimbari QURAN na HADITHI na BIBLIA kidogo ya agano la kale niliipitia nikisema nimeshuhudia kwa maana nimeshazungumza nao(sio live) kutoka kwa wagonjwa waliokuwa nayo mwilini na wengne nilikuwa nao nyumbani (wengine walikuja kibiinadamu)
na pia kufika sehemu ambazo wanazoISHI au Kwenye JABALI kubwa huko mlimani ulipo hasa hao wenyewe
kwa maananilipata bahati ya kuwauliza mambo mengi sana na si haba wanajua mengi ya dunia ndo mana nikiona watu wanabisha kuhusu haya MADUDE huwa naona hadi huruma

hivyo ndugu mshana jr hata mimi pia najifunza vitu pia toka katika baadhi ya mada zako 7bu ulimwengu wa kiroho ni mkubwa sana huwezi kujua yote. nakubali kabisa hatuwezi kwenda sawa kwa kila kitu ila tunapeana zaidi maarifa ila usichoke 7bu lengo lako si kuusambaza uchawi bali watu waufahaamu na kuchukua tahadhari hivyo mimi nipo hivyo pia 7bu naujua na nishaufanyia kazi
hivyo pamoja sana HOJA kwaHOJA
Sasa hata hao majini yaliyosilimu nayo hayataona pepo?maana take mwishoni umesema hata wakitubu ni jehenam
 
Si jina geni kwa kila mmoja wetu hapa jamvini.tumeshavijadili sana hivi viumbe visivyoonekana

Kuna hawa viumbe majini ambao huwaingia watu mara nyingi ikiwa wanawake na kuanza ukorofi mpaka vipewe vitu fulani fulani na ole wao wasimpe asichotaka pachatimbika

Waganga wanaotumia mizimu wao husema moja kwa moja kuwa ngoja tuwaulize mizimu inasemaje au hiyo kawape mizimu
Hizi ni baadhi tu ya lugha zinazotumika huko kwenye tiba za upande mwingine, ni lugha za heshima na zenye kuvutia zinazomuandaa mteja kujihisi yuko sehemu sahihi

LAKINI anayekwenda kujaribu matibabu haya ya upande wa pili awe makini na waganga feki wa kileo hata kama atatumia maneno ya waungwana na mizimu mara elfu moja

Waungwana hawana bei bali kile utoacho ni alama tu ya kuonyesha ushirikiano na commitment

Waungwana hawana masharti magumu Waungwana hushukuriwa mwishoni baada ya kufanikiwa mambo yako Ukikutana na mganga akawaita waungwana kisha akasema waungwana wanataka laki jua unapigwa live bila chenga
 
Kweli tuwaheshimu waalimu wetu... nimekwambia Mungu HAKUUMBA MAJINNI bali Malaika hivyo walivyoasi wakaitwa Ibilisi, mashetwain, mapepo n.k Mungu aliumba Malaika...hivyo unapokuwa unazungumzia uumbaji wa Mungu sema aliumba Malaika ambao waliasi lakini usiseme aliumba Majinni... kusema aliumba majinni maana yake hakuumba malaika hapo awali bali majinni jambo ambalo ni upotoshaji...
Leo ukizaa mtoto ukamlea vyema mpaka akajitambua akawa jambazi muuaji utasema umezaa jambazi au jina la ujambazi lilikuja baadae?! Jiongeze kidogo basi
Malaika hawezi kuasi, ila hutekeleza maamrisho ya Mungu. Wenye hiyari ya kuasi au kutii maamrisho ya Mungu ni sisi binadamu na majinni pia.
 
= yakikiri

Unayoyaona mengi kanisani ni mchezo wa kuigiza na au majinni ya kufugwa na hao hao wanaojifanya wachungaji. Wengi wa hao wachungaji ni mashetani na hushirikiana na mashetani wa kijinni kuwajaza watu ujinga.

Wajinga Ndiyo Waliwao.

Faizafoxy sijakuelewa, ulivyosema
"usichanganye kuhusu mashetani na majinni. Majinni ni viumbe, mashetani ni sifa ya viumbe wakiwemo binaadamu na majinni.

Halafu unasema tena

Wengi wa hao wachungaji ni mashetani na hushirikiana na mashetani wa kijinni kuwajaza watu ujinga.
 
Malaika hawezi kuasi, ila hutekeleza maamrisho ya Mungu. Wenye hiyari ya kuasi au kutii maamrisho ya Mungu ni sisi binadamu na majinni pia.
Labda imani yenu inawaambia Mungu aliumba 'Majinni' ila kwetu hamna hilo swala kabisa. Malaika anaasi according to my faith hivyo hata ukibisha utalazimisha niamini unachokiamini jambo ambalo haliwezi kutokea na pia nitaishia kukushawishi na haitawezekana hivyo basi baki na imani yako kwamba Mungu aliumba Majinni' ndugu na kila la kheri katika imani yako
 
Shukran sana.
Najua tatizo hatuna common understanding juu ya neno jinni. Hiyo ni sababu tosha ya mimi na wewe kutokukubaliana.

Kila la kheri.
 
That the perfect way of becoming great thinkers....hoja bila matusi wala kashfa
 
Labda imani yenu inawaambia Mungu aliumba 'Majinni' ila kwetu hamna hilo swala kabisa. Malaika anaasi according to my faith hivyo hata ukibisha utalazimisha niamini unachokiamini jambo ambalo haliwezi kutokea na pia nitaishia kukushawishi na haitawezekana hivyo basi baki na imani yako kwamba Mungu aliumba Majinni' ndugu na kila la kheri katika imani yako
Unaelewa maana Ya Kiumbe Kuitwa MALAIKA? au unaandika kwa jazba zisizo na maana hapa?

Ktk IMANI YOYOTE Hakuna Malaika mwenye CHOICE ya Kufanya mambo anavyotaka yeye.
Ndio maana akaitwa MALAIKA.

Someni imani zenu kwanza kabla ya kuandika mambo ya ajabu hapa.
 
MAJINI KATIKA DINI YA KIISLAM ( Q 72:1-14 )

Katika lugha ya kiarabu, neno Jini linamaanisha kitu kilichofichwa au kisichoonekana QURAN 1:71 Neno hili hutumiwa na Waarabu kwa ajili ya kutaja jina fulani. Kwa Waarabu, Jini anayevaa sura ya kike humwita Jinivya, hivyo majini Ghul/Ghilan, nao hujifunua kwa sura ya kike.

Katika imani ya Kiislamu, wao huamni kwamba Majini hutofautiana na Mashetani. Majini waliosilimu wao huitwa majini mazuri na hawa wakiwa katika hali kujionyesha kwa wanadamu, hao huitwa AJINU na wale walioacha kusilimu mwaka 610 AD (Baada ya Kristo) katika safari ya mtume Muhamad alipotoka Taif , wao wanaitwa Mashetani . Hivyo, wao wanapokuwa katika hali ya kutoonekana huitwa ALBAHATWA lakini pia Majini wote wanapokuwa katika hali ya kutoonekana waweza kuitwa ALBAHATWA, yaani PEPO.

Muislamu huamini kwamba kuna majini ya kike na kiume. Lakini pia , huamini kuwa Majini huoana na kuzaliana QURAN 55:56 na kuwa Majini huzaa sana kuliko binadamu na kwamba, Jini mmoja anaweza kuzaa watoto 300, na kuwa Jini huzaa watoto 3 hadi 4 kwa mkupuo. Somo QURAN 55:26-28 na kuwa Majini wanaweza kuishi miaka 400-1,000 kisha wanaweza kufa. Tofauti yao na binadamu ni kwamba wao wanaishi miaka mingi kuliko binadamu. Lakini pia, huamini kuwa wapo Majini wanaokula, wanaomeza, wanaokunywa, ila tofauti yao na wanadamu ni kwamba wao hula kwa kutumia mkono wa kushoto. Pia hiamini kuwa Majini wana uwezo wa kuzaa na Wanadamu. Soma QURAN 17:64. Waislamu huamini kwamba mtu anauwezo wa kuoa au kuolewa na Jini bila kujua, na mwanadamu anauwezo wa kumuua Jini. Soma QURAN 57:14-15

SURATULJINN

Ndani ya QURAN pia imo sura inayoitwa Suratuljinn ( QURAN 72 ). Sura hiyo huitwa hivyo kwa sababu ni sura ya Majini (Mapepo).

Kwa nini wanatajwa Majini katika imani ya Kiislamu?

Majini wanatajwa sana katika dini ya Kiislamu kwa kuwa ni waislam kwa kusilimu, kwa kuiamini Quran tukufu aliyopewa mtume Muhamad.. Majini walisilimu na kuwa Waislamu mwaka 610 AD(Baada ya Yesu) SOMA 72:1-14 QURAN. Hivyo basi, unapotumia neon jinni maana yake unatumia lugha ya Kiarabu ukimaanisha Pepo mchafu. Ni kama Spoon/kijiko, vyote ni kitu kimoja. Ndani ya Quran, neon “PEPO” limetumika kama Paradiso, mbinguni. Lakini pia, tunapata neon jingine liitwalo AKHERA ila neno hilo halimaanishi PARADISO, bali kwa lugha ya Kiarabu neno hili “AKHERA” lina maana ya KUZIMU. Lakini pia ukiangalia ndani ya SURALJINN ( QURAN 72:1-2, 8-9, 12 ) Mapepo hawa wanajieleza waziwazi kabisa kuwa mwanzo waliishi Mbinguni, walipogeuka kwa kuasi, walitegwa na Mungu. Linganisha na maandiko haya katika Biblia ( UFUNUO WA YOHANA 12:7-9; YUDA 1:6-8; UFUNUO 20:10; UFUNUO 21:8 ). Kwa mujibu wa dini ya Kiislamu, hawa majini ( Mapepo ) waliotegwa na Mungu Mbinguni wakiwa Malaika huko na kutupwa Duniani baada ya kuasi huko, sasa, wakati wa mtume Muhamad katika safari yake ya kurudi Taif mwaka 620 AD (baada ya Yesu) wapo walioamini na kuona kuwa Quran ni ya ajabu ya kuwatangazia neema ya kuabudu.

Katika vol 8-9, husema , wanapojaribu kwenda Mbinguni ( walikotoka zamani ), hukuta ile Mbingu imezungushiwa vimondo vya moto. Hivyo, hudai kuwa mbingu yao iko Akhera, yaani Kuzimu, maana Mbingu ya juu ina moto na hawana uwezo wa kwenda huko. SOMA ( QURAN 72:9 ), Mbingu ina utisho wa moto ila Akhera ( kuzimu ) hakuna shida kwao .

Hivyo basi, kulingana na jinsi Allah asemavyo ndani ya Quran kuwa nimeumba binadamu na majini ili muniabudu ( QURAN 57:58 ; 51:56) na kuwa , mbinguni mwao Majini wanaabudu (Majini waliosilimu mwaka 620 AD) ,SOMA QURAN 72:14, ambao ni wema wanaosafiri na kurithi uzima wa milele upatikanao Akhera ( Kuzimu ). Lengo kubwa la Shetani ni kufanya urafiki na wanadamu wengi ili kwa wingi huo apate watu wengi wa kwenda nao JEHANAMU ( QURAN 6:128 ). Jambo la muhimu kujua hapa ni kwamba moto wa milele hakuwekewa Mwanadamu bali ni Shetani na malaika zake wote ( Majini au mapepo ). Hawa, hawana nafasi tena ya kuungama au kutubu.
Duuh!!jamaa muongo wewe
 
Hivi unawezaje kuthibitisha uwepo wa majini? Je huwa yakimwingia mtu yeye atagundua kivipi...au ni lazima mtu mwingine mwenye ujuzi ndo atajua na huo ujuzi unapatikana je mkuu...
 
Hivi unawezaje kuthibitisha uwepo wa majini? Je huwa yakimwingia mtu yeye atagundua kivipi...au ni lazima mtu mwingine mwenye ujuzi ndo atajua na huo ujuzi unapatikana je mkuu...
Kwanza majini huwa hayawaingii watu hovyo tuu bali huchagua wa kuwaingia kulingana na 'conducive environment' na wenyewe hujikuta tu wanajifahamu aidha kwa kuambiwa au kutokana na matukio
 
Kwanza majini huwa hayawaingii watu hovyo tuu bali huchagua wa kuwaingia kulingana na 'conducive environment' na wenyewe hujikuta tu wanajifahamu aidha kwa kuambiwa au kutokana na matukio
Vipi kuhusu hao ambao tunasikia wanatumwa kwa watu kwa ajili ya kuwafanya jambo flani, je haya ni kweli na kama pia huweza kukataa kuwaingia watu kadhaa, pengine nao huwa ni waoga au ujasiri wao upoje!
 
Kila kitu kina mfumo wake kwahiyo hata ishu za majini ni za kimfumo zaidi ndio maana utakuta kuna kaliba ya watu kutokana na mfumo wa kiimani basi majini kwao ni kitu cha kawaida
 
Back
Top Bottom