Majina yangu ni kiswahili cha wapi?

Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
14,769
10,645
Wakuu, kumekuwa na tabia ya jamii kutumia sentensi "kwa majina naitwa" au "majina yangu ni" kila kunapofanyika utambulisho. Naomba kujuzwa kama hii ni sahihi ama la. Tena hata kwenye vyombo vya habari hili limekuwa jambo la kawaida kabisa ingawa binafsi sikuwahi kufjndishwa hivyo.

Mimi nina jina moja na jinhine la baba yangu na kama nitakwenda mbele zaidi kuna jina la babu. Ni kama anwani ya makazi. Naomba ufahamu wenu wakuu

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Majina yangu ni A B C umekua Msanii wa kizazi kipya mwenye AKA Sabini!??
Au umekua Attendance wewe mpaka uwe na Majina

Jina ni moja tu, Naitwa Aa Baa Chaa
Toshaa...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kiswahili cha Kenya.

Wapo sahihi nafikiri kwakua ukisema "Majina yangu ni Mchanga Wingu Juu" utakua umemaanisha yale majina yote 3 ni yako na kwakua wingi ni pale kitu kikizidi kimoja basi ni sawa kutamka hivyo.

Ukisema "Jina langu ni Mchanga Wingu Juu" upo sahihi pia. Kwa sababu hapa Mchanga Wingu Juu unakua ni utambulisho ambao unatendewa kama vile hauna wingi.

Ni kama vile tuseme utambulisho wako ni kirai (Natumaini nip sahihi) na kirai hakina wingi.

Haya ni mawazo yangu.
 
Wakuu, kumekuwa na tabia ya jamii kutumia sentensi "kwa majina naitwa" au "majina yangu ni" kila kunapofanyika utambulisho. Naomba kujuzwa kama hii ni sahihi ama la. Tena hata kwenye vyombo vya habari hili limekuwa jambo la kawaida kabisa ingawa binafsi sikuwahi kufjndishwa hivyo.

Mimi nina jina moja na jinhine la baba yangu na kama nitakwenda mbele zaidi kuna jina la babu. Ni kama anwani ya makazi. Naomba ufahamu wenu wakuu

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
Kenya wanatumia sana hii. Ninadhani wapo sahihi. Kama unajiona una jina moja, mbona unataja majina zaidi ya moja ukijitambulisha? Wao wanaona unataja zaidi ya jina moja, hivyo, wingi unahusika.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom