Majina yako nani au Jina lako nani?

MZIMU

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
4,057
1,371
BAKITA, hivi kwanini mmelala hivyo. Kiswahili kinachafuliwa sana. Kiswahili fasaha ni Jina lako nani?. Sio Majina yako nani?.

Ukiulizwa jina lako nani, hapo utayataja yote hatakama yanafika kumi. Unamkuta kiongozi mkubwa tu wa Serekalini anasema, kwa majina naitwa Tumaini Kazinyingi, kwa Mfano. Wakati hicho sio kiswahili fasaha. Angesema tu Jina langu naitwa Tumaini Kazinyingi.

BAKITA mnafanya kazi gani?
 
Mzimu uko sahihi kabisa. Jina ni utambulisho kamili wa mtu. Kwa hiyo kama utambulisho wako unakamilishwa na maneno ishirini basi maneno hayo ishirini ndiyo jina lako. Mfano Waziri Mkuu wa Tanzania jina lake ni: Mizengo Kayanza Peter Pinda na aliyekuwa Raisi wa Zaire Kabla ya Lawrence Kabila jina lake ni Mobutu Seseseko Kuku Ngbendu Wazabanga.
Nawaomba waandishi wa vyombo mbalimbali wawe macho na wawasahihishe wateja wao pindi wakoseapo kiswahili. Wasiwaache wakosee na waondoke bila kurekebishwa. Wenzetu wa Rwanda wametunga sheria inayomtia hatiani yeyote anayepotosha Kinywarwanda. Sisi hatuna sheria sawia ya kulinda Kiswahili japo tunavyo vyombo lukuki visivyokuwa na meno.
 
Mkuu ni kweli. Hii nchi kila jambo ni holela na hovyohovyo tu.
 
Halafu mwingine anasema "sefuria lipo kwa jiko" na ni mswahili naye.

Hihihihahhahahaa! Ni hatari Mkuu. Yaani wale wasio jua kiswahili ndio wamekua watangazaji wa redio na Televisheni na Washereheshaji kwenye Masherehe.
 
BAKITA, hivi kwanini mmelala hivyo. Kiswahili kinachafuliwa sana. Kiswahili fasaha ni Jina lako nani?. Sio Majina yako nani?.

Ukiulizwa jina lako nani, hapo utayataja yote hatakama yanafika kumi. Unamkuta kiongozi mkubwa tu wa Serekalini anasema, kwa majina naitwa Tumaini Kazinyingi, kwa Mfano. Wakati hicho sio kiswahili fasaha. Angesema tu Jina langu naitwa Tumaini Kazinyingi.

BAKITA mnafanya kazi gani?

Mkuu upo sahihi katika Kiswahili. Lakini usiwalaumu sana BAKITA kwa hapo ulipogundua japo kuna mengine isiwe sababu ya kuwalaumu. Binafsi nawafuatilia BAKITA na wanajitahidi sana kurekebisha pale ambapo wanaona kuna makosa.
 
Mkuu BAKITA ni BARAZA LA KISWAHILI TANZANIA. Sasa uwepo wao unamaana gani?
 
Sidhani kama wana uwezo wa kumfuata kila mtamzania na kumpatia elimu ya Kiswahili ila wao wanatumia vyombo vya habari kama TBC, Radio One na ladhalika. Ni jukumu letu sisi kufuatilia na kujifunza.
 
Sasa hivi Bakita ndio watakuwa polisi wa lugha? Hilo haliwezekani jamani. Ni vizuri kuwaelimisha watu, na hilo silo jukumu la Bakita bali ni jukumu la shule za Tanzania.

Hata hivyo mtu husema, Jina Langu ni Sospeter. Lakini pia waweza kusema Majina yangu ni Sospeter, Simba Mpenda Nyasi, na Jogoo wa Mjini. Haya yote matatu ni majina yako.
 
Na watu wengine wanataka waongee kama mtangazaji Fulani.

Kitu kingine ni pale wanapotamka bila waga kila penye herufi ya ''L'' wanaweka ''R''. Mfano utamsikia mtu anatangaza redioni,

Pare pare Uanjani

Reo Asubuhi

Ushauli wao Urifatwa

etc.
 
BAKITA, hivi kwanini mmelala hivyo. Kiswahili kinachafuliwa sana. Kiswahili fasaha ni Jina lako nani?. Sio Majina yako nani?.

Ukiulizwa jina lako nani, hapo utayataja yote hatakama yanafika kumi. Unamkuta kiongozi mkubwa tu wa Serekalini anasema, kwa majina naitwa Tumaini Kazinyingi, kwa Mfano. Wakati hicho sio kiswahili fasaha. Angesema tu Jina langu naitwa Tumaini Kazinyingi.

BAKITA mnafanya kazi gani?

Huu ni mwingiliano uliopo kwenye shirikisho la Africa Mashariki. Wenzetu Wakenya husema Majina yangu ni:.......
Tanzania : Jina langu ni: .....
Ikiwa ni tafsiri kutoka kiingereza (my names are ...Kenya )
(My name is. ... Tanzania )
 
!
!
anatakiwa arejee mzee kifimbo cheza akiwadhibiti wachafuzi wa lugha.....lakini nae alikutana na dhoruba fulani hivi ile ya "na kata funua ndio hi" loh
 
Back
Top Bottom