Catarina anna
Member
- Jul 26, 2019
- 14
- 7
Kwa mujibu wa Kifungu 201A cha Sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), Sura 287 na Kifungu cha 87A cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Sura 288 zikisomwa pamoja na Kanuni ya 3 na 6(1) ya Kanuni za Uchaguzi wa Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ngazi ya Vijiji, Vitongoji na Mitaa za mwaka 2019 zilizotolewa kwa Tangazo la Serikali Namba 371,372,373 na 374 ya mwaka 2019.
Kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa za mwaka 2019, mnamo tarehe 09/09/2019 Watumishi wa Umma 184 wameteuliwa kuwa Wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2019.
Wateuliwa wote wataapishwa siku ya Alhamisi tarehe 12/09/2019 katika Mikoa yao. Uongozi wa Mikoa utaratibu zoezi la kuapishwa kwao.
Orodha ya majina ya Watumishi walioteuliwa yanapatikana kwenye kiambatanisho hapo chini