Majina ya watumishi wa Umma walioteuliwa kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa-2019

Catarina anna

Member
Jul 26, 2019
14
7
Kwa mujibu wa Kifungu 201A cha Sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), Sura 287 na Kifungu cha 87A cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Sura 288 zikisomwa pamoja na Kanuni ya 3 na 6(1) ya Kanuni za Uchaguzi wa Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ngazi ya Vijiji, Vitongoji na Mitaa za mwaka 2019 zilizotolewa kwa Tangazo la Serikali Namba 371,372,373 na 374 ya mwaka 2019.

Kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa za mwaka 2019, mnamo tarehe 09/09/2019 Watumishi wa Umma 184 wameteuliwa kuwa Wasimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2019.

Wateuliwa wote wataapishwa siku ya Alhamisi tarehe 12/09/2019 katika Mikoa yao. Uongozi wa Mikoa utaratibu zoezi la kuapishwa kwao.

Orodha ya majina ya Watumishi walioteuliwa yanapatikana kwenye kiambatanisho hapo chini
 
Attachments

  • Wasimamizi UTEUZI.pdf
    213.9 KB · Views: 52
Kwa mamlaka ninayojipa mwenyewe namteua Tundu Lisu kuwa msimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa ubelgiji
 
Watumishi wa Umma 184 watasimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu kutoka kada mbalimbali wakiwamo Wakuu wa Idara ya Elimu za Msingi, Kitengo cha Sheria, Takwimu na Ufuatiliaji na Kitengo cha Uchaguzi.

Taarifa iliyotolewa na Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), watumishi hao kutoka idara hizo zinazosimamiwa na Ofisi za Wakuu wa Wilaya kutoka mikoa mbalimbali nchini, wataapishwa kesho Alhamisi Septemba 12 ambapo uongozi wa mikoa utaratibu shughuli ya kuapishwa kwao.
 
ok,kwa hiyo uchaguzi huu hausimamiwi na this so called NEC??,why NEC wasipewe madaraka ya kuajiri watumishi wao kuanzia taifani hadi ngazi ya mtaa na kuwa ndio wasimamizi wa chaguzi hizi?but never mind nimeshiriki uchaguzi mmoja tu na will never again vote,and after all hakuna uchaguzi may be tusubirie beyond 2025(kama nitakuwa hai itakuwa ni bonsai kubwa from MWENYEZI MUNGU)
 
Nitakuja huko kupiga kura 2020. Nataka wapate tabu kuiba kura yangu.
 
Wameteuliwa na mtawala wa CCM kusimamia maslahi ya ccm. Hakuna chama cha siasa kitashiriki uchaguzi huo, watakuwa wajinga bora waendelee kuvijenga vyama vyao wasubiri zama nyingine, hii itakuwa kujipotezea muda.
Nitasikitika nikiona PONA, TPP, DP, UMD, UDP, CUF na TADEA, kama vitashiriki.
 
Watumishi wa Umma 184 watasimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu kutoka kada mbalimbali wakiwamo Wakuu wa Idara ya Elimu za Msingi, Kitengo cha Sheria, Takwimu na Ufuatiliaji na Kitengo cha Uchaguzi.

Taarifa iliyotolewa na Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), watumishi hao kutoka idara hizo zinazosimamiwa na Ofisi za Wakuu wa Wilaya kutoka mikoa mbalimbali nchini, wataapishwa kesho Alhamisi Septemba 12 ambapo uongozi wa mikoa utaratibu shughuli ya kuapishwa kwao.
Kwahiyo tamisemi ndo NEC ujinga kweli hivi Tanzania kuna wasomi kweli?

Alafu utashangaa vijana machizi wanakuja humu jf kujaza saver tu hapa na utumbo wao mara ooh Lissu, Nape, Kinana shame on you Tanzanians
 
Si mlisema wakurugenzi wasisimamie uchaguzi,sasa ombi lenu limetekelezwa mnapiga kelele tena, sasa mnataka iweje kwa mfano !!
 
Suala siyo tu kuteuliwa kusimamia uchaguzi, isipokuwa wasiwasi upo endapo wanaamika kubeba jukumu hilo. Iseje kuwa wote ni makada tena kuna maelekezo ya ziada wamepewa mpaka wakakubalika kubeba dhamana hiyo.
 
Back
Top Bottom