Majina ya watoto (Vikembe) wa wanyama/viumbe

Asamwa

JF-Expert Member
Apr 13, 2012
3,578
2,261
Kuna ripoti fulani nilikuwa nasoma nikakutana na neno "vifaranga" ikimaanisha samaki wachanga. Ni sawa samaki wachanga kuitwa vifaranga?

Majina mengine ya watoto (vikembe) wa wanyama mbalimbali ni kama ifuatavyo:

Ng'ombe......Ndama
Nzige...kimatu/maige/tunutu/matumatu/funutu
Ndege....Kinda
Kipepeo/nondo....kiwavi
Nzi......Buu
Farasi....Kitekli
Mamba...... Kigwena
Nyangumi..... Kinyangunya
Fisi.... Kikuto/bakaya
Ngamia..... Nirigi/nirihi
Paka.......kinyaunyau/kipusi
Ndovu.... Kidanga
Mbweha.... Nyamawa
Nyani...... Kigunge
Kondoo..... Kibebe/katama
Mbuzi.....Kibui/kibuli/kimeme
Farasi na punda.... Nyumbu
Punda.... Kiongwe/kihongwe
Mbu....kiluwiluwi
Chura.... kiluwiluwi
Kuku..... Kifaranga
Papa.... Kinengwe
Nyuki.... Jana
Simba..... Shibli
Sungura.....Kitungule
Kwanga/wibari.... " "
Samaki.... Chengo/kichengo
Chui.... Chongole/kisui
Mbwa..... Kilebu/kidue/kibwa
Nyoka...... Kinyemere
Njiwa..... Kipura
Wazazi wenye rangi tofauti.... Chotara/suriama

Naomba michango yenu mingine.
 
Kuna ripoti fulani nilikuwa nasoma nikakutana na neno "vifaranga" ikimaanisha samaki wachanga. Ni sawa samaki wachanga kuitwa vifaranga? Naomba michango yenu.
Ndio lugha inayotumika- vifaranga. Kwa kiingereza wanaita fish fingerlings or seed kwa samaki hawa wa kawaida. Ikiwa prawns watasema postlarvae na itabadilika kutokana na aina ya samaki.
 
Kuna ripoti fulani nilikuwa nasoma nikakutana na neno "vifaranga" ikimaanisha samaki wachanga. Ni sawa samaki wachanga kuitwa vifaranga? Naomba michango yenu.

samaki mchanga kule kwetu ina maana nyingine so jiandae kwa majibu usiyotarajia
 
Kifaranga ni mtoto wa kuku/bata/ndege kwa ufupi viumbe jamii ya ndege watoto wao wanaitwa vifanga, vinaanguliwa kutoka kwenye mayai.

Ndama ni mtoto wa ngo'mbe
Mtoto wa samaki anaitwa mtoto wa samaki
Mtoto wa mbwa anaitwa mtoto wa mbwa
Mtoto wa binadamu anaitwa mtoto wa binadamu
Hicho ndio kiswahili
 
Kifaranga ni mtoto wa kuku/bata/ndege kwa ufupi viumbe jamii ya ndege watoto wao wanaitwa vifanga,vinaanguliwa kutoka kwenye mayai.

Ndama ni mtoto wa ngo'mbe
Mtoto wa samaki anaitwa mtoto wa samaki
Mtoto wa mbwa anaitwa mtoto wa mbwa
Mtoto wa binadamu anaitwa mtoto wa binadamu
Hicho ndio kiswahili

Na kinda utaelezeaje?

Sent from my GT-P7500 using Tapatalk HD
 
Ndio lugha inayotumika- vifaranga. Kwa kiingereza wanaita fish fingerlings or seed kwa samaki hawa wa kawaida. Ikiwa prawns watasema postlarvae na itabadilika kutokana na aina ya samaki.

Mkuu mtoto wa kibua anaitwaje?
 
Dagaa anapotaga mayai, mayai yanatotoa dagaa, dagaa ni samaki mdogo hakui mkubwa hata akiwa amepea
 
Mkuu mtoto wa kibua anaitwaje?

Kibua ni jamii ya samaki
mtoto wa kibua anaitwa kibua
mtoto wa tasi anaitwa tasi
mtoto wa nguru anaitwa nguru
mtoto wa pweza......
mtoto wa jodari.....
mtoto wa ngisi......
mtoto wa mkundaji.....
mtoto wa koana....
mtoto wa changu.....
mtoto wa nduwaro....
mtoto wa kasa.....
mtoto wa taa......
mtoto wa kolekole....
mtoto wa sumbururu.....
kaka unawajua hao samaki ;)
 
Kifaranga ni mtoto wa kuku/bata/ndege kwa ufupi viumbe jamii ya ndege watoto wao wanaitwa vifanga,vinaanguliwa kutoka kwenye mayai.

Ndama ni mtoto wa ngo'mbe
Mtoto wa samaki anaitwa mtoto wa samaki
Mtoto wa mbwa anaitwa mtoto wa mbwa
Mtoto wa binadamu anaitwa mtoto wa binadamu
Hicho ndio kiswahili

Mtoto wa mbwa anaitwa mtoto wa mbwa-kijibwa
Mtoto wa binadamu anaitwa mtoto wa binadamu-mwana/kichanga
 
Kinda la ndege
mtoto wa ndege anaitwa kinda
asante kaka
Kinda ni hatua ya pili ya kifaranga katika ukuaji,hapa some how ana uwezo wa kujitambua/nakujisaidia sio helpless kama alipokuwa kifaranga.
 
Kinda ni hatua ya pili ya kifaranga katika ukuaji,hapa some how ana uwezo wa kujitambua/nakujisaidia sio helpless kama alipokuwa kifaranga.

Usifananishe kiswahili na lugha nyingine, watu wengi wanafananisha grama ya kiswahili na Kingereza kuwezi kumwita mtoto wa kuku kinda la kuku wala huwezi kumwita kinda la ndege kifaranga cha ndege. Hicho kitakuwa sio kiswahili itakuwa lugha iliyofanana na kiswahili lakini watu watakufahamu nini umekusudia.
 
Dagaa ni samaki mbilikimo bwana sio mtoto.....

Hehehehe samaki mbilikimo:yo:, uko sawa madameX dagaa hakuwi umbo lake ndio hilo hilo,baba wa dagaa umbo lake liko hivyo mama wa dagaa umbo lake liko hivyo
 
Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom