Majina ya wanaowania uenyekiti uvccm hadi sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majina ya wanaowania uenyekiti uvccm hadi sasa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by engmtolera, May 19, 2011.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  May 19, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Hivi karibuni, Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Tanzania ulitangaza fursa ya watu kuwania kiti cha Uenyekiti wa umoja huo.

  Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela, hadi sasa kati ya waliojitokeza kuwania nafasi hiyo ni wanawake watano na wanaume saba.

  Majina yao yakiwa ni:

  -Thabiti Jecha Kombo
  -Bakar Bakar
  -Innocent Melleck Shirima
  -Omar Mwadi Mwarabu
  -Asha Suleiman Shibu
  -Shinuna Kombo Juma
  -Mwanawewe Usi Yahya
  -Laila Burhan Ngozi
  -Sadifa Juma Khamis (Mbunge wa Donge)
  -Khadija Nassor Abdi (Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM)
  -Jamal Kassim Ali (kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM-Zanzibar)
  -Hamidu Bilal Gharib (mtoto wa kaka'ke Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal)

  Kwa mujibu wa Katiba ya UVCCM, mwenyekiti wa umoja huo akitokea upande mmoja wa muungano, lazima makamu wake atoke upande mwingine. Kwa sasa, Makamu Mwenyekiti wa umoja huo ni Benno Malisa hivyo mwenyekiti wake analazimika kutokea Zanzibar.
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  May 19, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Wacha wapambane labda wataiokoa CCM kupitia UVCCM. Ila hayo majina ni yaleyale.
   
 3. e

  erneus kyambo Member

  #3
  May 19, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyie wote mnaogombea ni zero! Najua dhamira iliyowasukuma kugombea nafasi hizo ni ili muweze kula kwani mmeona 'wakubwa zenu ndani ya chukua chako mapema(ccm) wamekula wakashiba na sasa wamevimbiwa na sasa ni wakati wenu kugombea kula kama wao'-si maneno yangu,mliwahi kusema hivyo. Nimeona lista yenu wote, naamini kabisa dhamira zenu zote ni sawa ; Hivyo wote mnagombea kuwa wawakilishi wa wala nchi na sio wawakilishi wa wananchi!
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  May 19, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Chama cha kiislam hiki Mwanakijiji 2011. Kama ukweli hivi
   
 5. mpiganiahaki

  mpiganiahaki Senior Member

  #5
  May 19, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Duh! Nimejua na kuamini leo, chukua chako mapema(ccm) ni chama cha WAISLAM ,wana jf angalieni hiyo list vizuri, kati ya wagombeaji 12, wote ni WAISLAM isipokuwa moja tu! Asanten kwa kunifungua macho.
   
 6. Freestyler

  Freestyler Senior Member

  #6
  May 19, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sasa jamani mgombea wa nafasi ya uenyekiti anatakiwa kutokea Zanzibar (kikanuni) bado mnategemea nusu wawe wakristo? Sitashangaa mkitaka na sehemu za kuuza kitimoto Zanzibar zilingane na Bara!!
   
Loading...