Majina ya Waliopendekezwa Viti Maalum na hoja za Leticia Musore

Acheni kumlaumu huyo mama rather is high time to real think about this very country!

wanachadema hamna hata haja ya kumzungumzia, maana vidole vingine vinawanyooshea wenyewe!

Slaa alihama CCM for likely reasons! unataka niseme nini juuu ya Mpendazoe, Marando, Shibuda......

If she is right then chadema must act on it accordingly is not a first time we hear the same accusations, we have been hearing this for years now, since late Wangwe, come to Kafulila and many more............................However..it is common you should know politics.. even csame NCCR people are running away!

why waste time to blame her? you may fail to defend your chama simply....remember Slaa....

Leave her, wabunge wa kuteuliwa ndani ya chadema bado kuna ugomvi mwingi na tuhuma nyingi sana, however, those are politics..

lets think of new katiba and NEC

Yeah. I support your opinion.

These gossips are a best suit for CCM.
 
Tuwe makini sana na watu wa aina hii, bado ussm unawasumbua! Si wanamageuzi wa kweli. Kwa heshima zake mama kama yule huwezi kuamini anakimbia eti kakosa viti maalumu! CHADEMA isigeuzwe ssm, kuna vigezo vya kugombea ubunge na kuteuliwa viti maalum. Hata kama huyu mama alikuwa amevifikisha, nadhani hakustahili kabisa kupewa kwa jinsi ambavyo ameonyesha udhaifu wake! You show, you perfom then you deserve! nothing will come out of that unless you are in ssm green jacket where sleeping in the parliament and punishing tables is rewarded!
 
M'kiti Wanawake Chadema atimkia NCCR-Mageuzi
Monday, 22 November 2010 20:34

Patricia Kimelemeta na Fidelis Butahe

MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake wa Chadema, Leticia Musori amehamia chama cha NCCR-Mageuzi huku akikiponda chama chake cha zamani kwa madai kuwa kimejaa udini, ukabila na ubinafsi. Musori amedai kuwa amechukua uamuzi huo baada ya kutofautiana na viongozi wa juu wa chama hicho, akiwemo mwenyekiti Freeman Mbowe, katibu mkuu Dk Willibrod Slaa na Tundu Lissu kuhusu uteuzi wa wabunge wa viti maalum, akisema kuwa baadhi ya watu wenye sifa walienguliwa.

Suala la viti maalum lilikuwa na utata mkubwa ndani ya Chadema kabla ya uchaguzi mkuu na kusababisha viongozi watofautiane, lakini mwishoni uongozi wa juu walikubaliana kumtafuta mtaalamu ambaye alitengeneza vigezo na sifa ambazo zilitumika kupata wabunge wa viti maalum, kikiwemo kigezo muhimu cha elimu, uzoefu na kuthubutu kugombea ubunge majimboni. Kwa mujibu wa mchanganuo huo wa kupata wabunge wa viti maalum, Musori alikuwa amepata alama za chini ambazo zingeweza kumpa ubunge tu iwapo Chadema ingefanya vizuri zaidi kwenye uchaguzi mkuu.

Lakini idadi ya kura za urais ya asilimia 26.2 na idadi ya wabunge 24 walioingia bungeni imemfanya mwenyekiti huyo wa wanawake kushindwa kupata nafasi. Lakini Dk Slaa alijibu tuhuma hizo jana akisema kuwa Musori ameondoka kwenye chama hicho baada ya kukosa nafasi ya ubunge wa viti maalum. Alisema mara nyingi watu wanakwenda kwenye vyama wakiwa na maslahi yao binafsi, wasipopata kile walichofuata huanza kunyea kambi, jambo ambalo Dk Slaa alisema linawafanya wazunguke kila chama kwa ajili ya kutetea maslahi yao binafsi. “Ninamshangaa sana Mama Musoril; baada ya kushindwa kupitishwa kwenye nafasi ya viti maalum ameanza kunyea kambi. Mwache aondoke; narudia tena, kama kuna mtu mwingine naye amefuata uongozi ndani ya chama aondoke.

Hakuna huruma katika hilo,” alisema Dk Slaa. Aliongeza kuwa mchakato wa kutafuta wagombea wa viti maalum ulianzia ngazi ya wilaya ambako mama huyo alishindwa kwa kupata kura moja. Baada ya kuona hivyo akaamua kuomba msaada, lakini walishindwa kutokana na majina hayo kufikishwa Tume ya Uchaguzi (Nec) kwa ajili ya kuyathibitisha. Alidai kuwa kutokana na hali hiyo mama huyo alikosa nafasi na ndio maana ameamua kuhama chama. Alisema jambo hilo linaonyesha wazi kuwa alifuata ubunge ndani ya Chadema.

Alikanusha madai ya ukabila akisema kilichopo ni maadili ndani ya chama na kwamba ikiwa mtu ameshindwa, anapaswa kuondoka na kujiunga na vyama vingine. “Kwanza mimi hata dini yake siijui... tatizo lililopo ni kwamba hakuteuliwa kwenye ubunge wa viti maalum ndio maana amehama,” alidai Dk Slaa. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Musori alisema kuwa kutokana na maamuzi ya wabunge wa viti maalum kufanywa na wanaume bila ya kulishirikisha Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), ameamua kujiengua chama hicho. “Chadema inaongozwa kwa misingi ya udhalilishaji wa kijinsia, ukabila, undugu na mambo mengine ambayo si mazuri," alidai Musori. "Jambo hilo limesababisha viongozi wakuu kuchagua majina mengi ya wabunge wa viti maalum ambao hawana uwezo,” alisema Musori.

Alidai kuwa mwenyekiti wa Chadema ndio mwenye maamuzi ya mwisho ndani ya chama na anafanya hivyo bila ya kushirikisha wanachama wake katika kutoa maamuzi hayo, jambo ambalo alidai linasababisha kuwepo kwa mpasuko ndani ya chama. Alisema kutokana na hali hiyo, Chadema inakabiliwa na mpasuko mkubwa ambao utasababisha wanachama wengine kuhama kutokana na maamuzi aliyoyaita ya kiubabe yanayofanywa na viongozi hao katika shughuli za chama bila ya kujali utu wa mtu, wala nafasi yake na hivyo kusababisha kuibuka kwa mgogoro. “Mgogoro uliopo ndani ya chama ni mkubwa.

Mpaka sasa umesababisha wanachama wengine kuhama, hii inatokana na maamuzi ya kiubabe yanayofanywa na Mbowe bila ya kuangalia utu wa mtu, jambo ambalo limesababisha kuwepo kwa udhalilishaji wa kijinsia... tumesikitishwa sana,” alisema Musori Alidai kuwa kuondoka kwake ni mwanzo, lakini kuna wanachama wengi ambao mpaka sasa wameanza kurudisha kadi huku wengine wakiendelea kutafakari uamuzi wa kukihama chama hicho. “Iweje mwenyekiti awe signatory (mtia saini) wa kila kitu, hapo kuna tatizo... haiwezekani kiongozi kuwa na maamuzi yako huku wanachama wanataka vile... kutokana na hali hiyo nataka kujenga heshima yangu na familia; nimeamua kuihama Chadema na kujiuzulu uongozi wowote ndani ya chama hicho na sasa najiunga na NCCR,” alisema. Musori alikuwa mwenyekiti wa umoja huo wa wanawake wa Chadema, mjumbe wa kamati Kuu, mjumbe wa Bawacha na Mweka hazina wa Umoja wa Madiwani wa Chadema).

Mwenyekiti wa NCCR –Mageuzi, James Mbatia alisema suala la maamuzi ndani ya chama linapaswa kufanya na viongozi wa aina zote bila ya kujali jinsia ya mtu au cheo chake na kwamba jambo hilo linaweza kusaidia chama kusonga mbele. “Tunachpaswa kufanya ni kuthamini utu wa mtu,” alisema Mbatia ambaye aligombea ubunge wa Jimbo la Kawe bila ya mafanikio. Huwezi kudai mabadiliko ya katiba wakati katiba ya chama chako inakusuta, kutokana na hali hiyo viongozi wa vyama wanapaswa kujiangalia kwanza kabla ya kutetea kile wanachokitaka. Uamuzi wa Musori umefanyika siku moja baada ya mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Mbeya, Smabwe Shitambala kutangaza kujivua wadhifa wake ili kupisha uchunguzi dhidi yake kufanyika kwa uhuru.

Shitambala, ambaye aligombea ubunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini na kushindwa na mgombea wa CCM, anadaiwa kupewa fedha na maofisa wa chama hicho tawala ili akihujumu. Shitambala aliwahi kugombea ubunge wa jimbo hilo katika uchaguzi mdogo uliofanyika mwaka 2008, lakini alienguliwa na Tume ya Uchaguzi baada ya kubaini kasoro kwenye hati yake ya kiapo. Chadema, ambayo imeibukia kuwa chama kikuuu cha upinzani Tanzania Bara, pia kilipoteza wanachama wake kabla ya uchaguzi mkuu baada ya David Kafulila kukihama mapema mwaka huu na kujiunga na NCCR Mageuzi ambayo ilimsimamisha kuwania ubunge wa Kigoma Kusini na kushinda. Pia ilimpoteza Felix Mkosamali (Muhambwe) na Moses Machali (Kasulu Mjini).

CHANZO: GAZETI LA MWANANCHI
M'kiti Wanawake Chadema atimkia NCCR-Mageuzi
 
Mambo kutokuwa shwari ni mazingira yasiyoepukika ndani ya chama cha siasa ambacho umaarufu wake mbele ya jamii unakua kwa kasi kama chadema. Hiyo ni changamoto kama zilivyo changamoto zingine. Muhimu hapa, ni namna viongozi wake wanavyoweza kutuliza akili na kutumia hekima na busara kukabiliana na changamoto hiyo. Makifanikio ya kuikabili changamoto hiyo, yanakisogeza mbele chama na kuwa imara zaidi.

Kwa hiyo, kwangu mimi hali kutokuwa shwari ninaichukulia kuwa ni fursa ya chama kujikomaza au kujipima namna kinavyoweza kukabiliana na changamoto. Vile vile, hali hiyo pia inaweza kuwa ni fursa kwa chama kusafisha uchafu uliomo ndani ya chama unaoweza kuwa umeletwa na 'rivals' wa chama kama vile ccm ambao hawachelewi kupandikiza mamluki wao ndani ya chama kinachoonekana kuwa ni tishio kwao. Viongozi wa chadema lazima watambue kuwa pigo walilowapatia ccm la kuchukua majimbo yote muhimu kwenye uchaguzi lilikuwa ni 'direct punch' ya usoni kwa ccm. Kwa hiyo, ccm inahaha na kutokana na hilo sitashangaa kamwe chadema itakapokumbana na migogoro mingi zaidi, ikilinganishwa na nyakati zingine zilizopita. Kama nilivyosema, muhimu ni viongozi wa chadema kutuliza akili na kutumia hekima na busara katika kukabiliana na changamoto hizo.

Well said, huwa wanakosea issue ni kubadilika hapa, maana tuhuma hizi zimekuwepo kitambo sana, sidhani kamani tatizo kubwa, ila ukweli uangaliwe bila ushabiki

Uteuzi wa Zakhia Meghiji kuwa mbunge alishirikishwa nani?

So nao wanafanya kama CCM sio? LMAO!!!!!!!!!
 
Slaa alihama CCM lini? I think alihama zamani sana, hata kabla ya ubunge. Nisahihisheni kama nimekosea
 
amehamia nccr mageuzi kwa sasa baada ya kukosa viti maalumu ndani ya chadema huku akitoa shutuma za udini,ukabila na kila aina ya ubaguzi ambao anadai upo ndani ya chadema.
kwa umri wake hakupaswa kusema hayo yote,hivi muda wote wa utumishi wake ndani ya chadema hakuyaona hayo anayoshutumu kwa sasa?
Amejikwaa,amepotea njia,amekuwa mfa maji na sasa anatapatapa,akumbuke utu uzima dawa,akae kimya kama amegundua kuna uozo chadema na aelekee kule anakokuona kwake ni sahihi.chadema si yeye bali ni taasisi ya watu wenye mapenzi mema,wapenda mabadiliko,wazalendo na wanaharakkati wa kweli

Mnategemea nini kama Ubunge Viti Maalum, anaachwa mwenyekiti wa Bawacha Taifa na badala yake wanachaguliwa mabinti, wake na vimada wa viongozi wa juu wa Chama.
Kama mnataka imani ya watanzania kama chama mbadala, hamna budi kuyafanyia kazi haya na kujikosoa vinginevyo 2015 mtaachwa mbali sana.
Kumbuka kwa asilimia kubwa sehemu mlizoshinda ilikuwa chuki dhidi ya ubovu wa chama tawala na wala sio uwezo au uzuri wenu kama chama.
 
Chadema wameshaanza kujichanganya na mpaka 2015 hawatakuwa na nguvu waliyonayo
Kweli ukabila umo na ushemeji
Hata Hayati Chacha Wangwe alisema haya
Na wengine wameyaona
Mbio za sakafuni
 
Mheshimiwa Kitila Mkumbo,

Habari za asubuhi.

Kabla ya yote napenda kukupa pole kwa majukumu ya kila siku ya kichama na kitaifa. Umekuwa ni mtu muhimu katika ukuaji wa demokrasia ndani ya nchi yetu yenye kila hila kuona demokrasia inapindishwa. Ama baada ya salamu nina maswali yangu machache ningeomba unijibu wewe mwenyewe binafsi. Sitategemea mtu mwingine aingilie na kuanza kutoa kashfa. Maana imezoeleka humu ndani unapofanya kitu watu wanakushambulia hata kama kitu hicho ni cha kujenga demokrasi.

Swali ni kuwa chini nimequote sababu zilizopelekea aliekuwa mwenyekiti wa wanawake Chadema Leticia Musori kutochaguliwa katika nafasi za kuingia bungeni kwa viti maalumu. Katika list uliyoitoa kuna majina mapya ya walioingia kwenye Chadema muda si mrefu na wamefanikiwa kuingia kwenye ubunge kupitia viti vya "upendeleo" mfano mzuri ni Mama Kaihula huyu mama alikuwa mwalimu wangu pale CBE sijawahi kumsikia kushiriki siasa mpaka hivi karibuni mwaka huu na licha ya kugombea na kushindwa ameweza kupita kwenye hivyo viti vya "upendeleo" wa pili ni mzazi mwenzake Dr W. P. Slaa Mhe Rose Kamili yeye alikuwa CCM amehama chama akasimama kugombea hakufanikiwa lakini amepitishwa kwa njia ya viti vya "upendeleo"

Sasa ikiwa hawa wameingia kwenye chama karibuni na walio serve muda mrefu hawakupewa fursa je ni sababu zipi ulikuwa unaangalia ili mtu kuweza kupata fursa hiyo? nakuuliza wewe kwa kuwa mchakato mzima ulikabidhiwa wewe ku rank nani awe wa mwanzo na nani awe wa mwisho. Sitakosea nikisema wewe ulikuwa "consultant" kwenye hili na nina amini ni wewe pekee mwenye majibu stahiki kwa hili. Na haitakuwa vibaya ikiwa utaelezea kwanini wewe peke yako ulipewa jukumu hilo? kwanini hamkutumia demokrasia kama ya upigaji kura? na kwanini na je nini faida ya mtu mmoja kuchagua wabunge wa viti maalumu na nini hasara ya demokrasia kuchukua mkondo wake kwenye suala hilo?


Nategemea majibu mazuri kutoka kwako natanguliza shukrani za dhati.





quote_icon.png
Originally Posted by Kitila Mkumbo
Tatizo la huyu mama yetu alikariri kwamba yeye lazima ilikuwa awe mbunge wa viti maalumu kwa sababu tu alikuwa mwenyekiti wa BAWACHA kitaifa. Bahati mbaya kwake ni kwamba hatukuwa na kigezo specific cha kumlenga mwenyekiti wa bawacha au kiongozi yeyote mwingine. Katika vigezo tulivyotumia yeye aliangukia kwenye namba 29 kama inavyoonekana katika orodha hapa chini ya first 40 candidates.

Katika safari hii ya mapambano sio abiria wote watakaofika mwisho wa safari; wapo watakaoshukia njia-huyu ni mojawapo!!


Orodha ya wanaopendekezwa kuwa wabunge wa viti maalumu-CHADEMA

Orodha ya wanawake 40 wa juu




1.Lucy Fidelis Owenya
2. Esther Nicholas Matiko
3. Mhonga Said Ruhwanya
4. Anna MaryStella John Mallac
5. Halima James Mdee
6. Paulina Philipo Gekul
7. Conjesta Leos Rwamlaza
8. Susan Kiwanga
9. Grace Sindato Kiwelu
10. Susan Lyimo
11. Regia Mtema
12. Christowaja Mtinda
13. Anna Valerian Komu
14. Mwanamrisho Abama
15. Joyce Mukya
16. Leticia Mageni Nyerere
17. Naomi Kaihula
18. Chiku Abwao
19. Rose Kamil Sukum
20. Christina Lissu Mughiwa
21. Raya Ibrahim Hamisi
22. Philipa Geofrey Mturano
23. Mariam Salum Msabaha
24. Rachel Mashishanga Robert
25. Sabrina Hamza Sungura
26. Rebecca Michael Mngodo
27. Cecilia Daniel Pareso
28. Subira Shabani Waziri
29. Leticia Gati Musore
30. Helen John Kayanza
31. Rosana Osemu Chapita
32. Mona Shomary Bitakwate
33. Evarim Adrian Mpangama
34. Asha Sudi Kayumba
35. Hija Rashid Wazee
36. Mary James Martin
37. Sophia Hebron Mwakagenda
38. Bupe Odeni Kyambika
39. Magreth Thadei Mangowi
40. Esther Cyprian Daffi

 
Chadema Imeanza kuoza
Na wanaanza kutuonyesha kuwa hata Dk W. Slaa alikuwa ni chambo tuu kwenye kugombania urais
Hakika kama wangepata basi baada ya miaka mitano wangemtoa na kumsimamisha mmoja wao kati ya wana ndugu na mashemeji
Hii imenipa wasiawai sanaaa
Naimani hata Zitto Atang'atuka Chadema ifikapo au ikaribiapo 2015
Chadema siyo Chaguo la MUNGU
 
Vipi huyu mama alikuwa ameandaa mavazi ya kuingia kwenye mjengo au? Maana anavyotetea kama vile mtoto alishafanyiwa maandalizi yote kwa ajili ya ubarikio ghafla mchungaji akasema hakufaulu mtihani. Angevumilia si bado Chadema wana nafasi mbili hazijateuliwa?
 
Mh!rafiki yangu mbona una inferiarity complex kwa kiasi kikubwa?kwa nini unaongopa kujibiwa na wana JF wengine zaidi ya DR Kitila Mkumbwa?Usiogope kukosolewa hii ni kawaida katika maisha ya binadamu!Huyu siyo mheshimiwa,mheshimiwa ni Jakaya Kikwete.Huyu anaitwa Dr Kitila Mkubwa,naomba umpe heshima yake!!!
 
Mi najiuliza, mtu kukaa kwenye chama kwa muda nrefu ndio kigezo cha kupewa ubunge/uongozi?

Kama ni hivyo, Kingunge Ngombale Mwiru angekuwa rais wa nchi hii badala ya JK.
 
Mimi kwenye fani yangu ni marufuku kutaja jina la mshindani wangu kibiashara ninapokuwa na majadiliano na wateja wangu. Maana yangu jinsi jina la CHADEMA linavyotajwa kwa uzuri au ubaya ndivyo CHADEMA inavyozidi kujulikana
 
Mkuu hii habari iko hapa tangu juzi, next time check kama kuna stori inayofanana na ile unayotaka kupost kabla hujaposti ya kwako kuturahisishia na sisi wachangiaji na wasomaji.
 
Hivi ni lazima kila kiongozi ni lazima awe mbunge? Huyu mama ameonyesha wazi kwamba kilichomuingiza kwenye harakati ni ubunge ambao hata hivyo laikuwa hastahili kwa nafasi aliyokuwamo katika mchakato huo wa viti maalum.
 
Back
Top Bottom