Majina ya Waliopendekezwa Viti Maalum na hoja za Leticia Musore

Kitila Mkumbo

JF-Expert Member
Feb 25, 2006
3,355
1,952
Tatizo la huyu mama yetu alikariri kwamba yeye lazima ilikuwa awe mbunge wa viti maalumu kwa sababu tu alikuwa mwenyekiti wa BAWACHA kitaifa. Bahati mbaya kwake ni kwamba hatukuwa na kigezo specific cha kumlenga mwenyekiti wa bawacha au kiongozi yeyote mwingine. Katika vigezo tulivyotumia yeye aliangukia kwenye namba 29 kama inavyoonekana katika orodha hapa chini ya first 40 candidates.

Katika safari hii ya mapambano sio abiria wote watakaofika mwisho wa safari; wapo watakaoshukia njia-huyu ni mojawapo!!

Orodha ya wanaopendekezwa kuwa wabunge wa viti maalumu-CHADEMA

Orodha ya wanawake 40 wa juu

1.Lucy Fidelis Owenya
2. Esther Nicholas Matiko
3. Mhonga Said Ruhwanya
4. Anna MaryStella John Mallac
5. Halima James Mdee
6. Paulina Philipo Gekul
7. Conjesta Leos Rwamlaza
8. Susan Kiwanga
9. Grace Sindato Kiwelu
10. Susan Lyimo
11. Regia Mtema
12. Christowaja Mtinda
13. Anna Valerian Komu
14. Mwanamrisho Abama
15. Joyce Mukya
16. Leticia Mageni Nyerere
17. Naomi Kaihula
18. Chiku Abwao
19. Rose Kamil Sukum
20. Christina Lissu Mughiwa
21. Raya Ibrahim Hamisi
22. Philipa Geofrey Mturano
23. Mariam Salum Msabaha
24. Rachel Mashishanga Robert
25. Sabrina Hamza Sungura
26. Rebecca Michael Mngodo
27. Cecilia Daniel Pareso
28. Subira Shabani Waziri
29.
Leticia Gati Musore
30. Helen John Kayanza
31. Rosana Osemu Chapita
32. Mona Shomary Bitakwate
33. Evarim Adrian Mpangama
34. Asha Sudi Kayumba
35. Hija Rashid Wazee
36. Mary James Martin
37. Sophia Hebron Mwakagenda
38. Bupe Odeni Kyambika
39. Magreth Thadei Mangowi
40. Esther Cyprian Daffi
 
MOSHI unaoendelea kufuka ndani ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) unaonekana kuficha moto.

Baada ya uchaguzi mkuu mwaka huu, hali ndani ya chama hicho inaonekana kutokuwa shwari hasa kutokana na mgawanyiko wa wazi unaojitokeza sasa.

Chachu zaidi ilijitokeza hivi karibuni baada ya Katibu Mkuu wa Chama hicho ambaye pia alikuwa mgombea urais, Dk. Willibrod Slaa, kukataa kutambua matokeo yaliyompa ushindi Rais Jakaya Kikwete, aliyekuwa akigombea kwa tiketi ya CCM.

Hali hiyo ndiyo iliyofanya baadhi ya wabunge wa chama hicho kususia pia hotuba ya Rais Kikwete, alipokuwa akizindua Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 18, Dodoma.

Tukio hilo lilitanguliwa na la kutohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kulikofuatiwa usiku na hafla ya kupongeza wabunge, ambapo baadhi ya wabunge wa chama hicho walihudhuria.

Hatua hiyo ilisababisha mgawanyiko wa wazi, kwa baadhi ya wabunge kutoshiriki ususiaji huo na kutoa sababu zao walizoona ni za msingi.

Lakini, kana kwamba hiyo haitoshi, juzi Mwenyekiti wa Chama hicho wa Mkoa wa Mbeya, Sambwee Shitambala akatangaza kujiuzulu wadhifa huo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zilizoelekezwa kwake.

Shitambala aliwambia waandishi wa habari kuwa uongozi wa chama hicho kitaifa unamtuhumu kuhongwa Sh milioni 600 ili ahujumu chama chake na kushindwa kutwaa jimbo la Mbeya Vijijini.

Wakati hayo yanaendelea, huku uongozi wa juu ukikataa kuyazungumzia kuchelea majibizano, jana Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Leticia Musori, alitangaza kukihama chama hicho na kujiunga rasmi na NCCR-Mageuzi. Kiini cha hatua hiyo ni uteuzi wa wabunge wa viti maalumu katika chama hicho.

Musori aliwambia waandishi wa habari jana kuwa hakushirikishwa katika uamuzi wa kuteua wabunge hao na kudai kuwa waliteuliwa kwa kufuata uhusiano na vigogo wa chama hicho.

Akizungumza wakati anakabidhiwa rasmi kadi ya NCCR-Mageuzi na Mwenyekiti wa Chama hicho, James Mbatia, Musori alisema uamuzi wake unatokana na wanawake kukosa haki na mfumo dume kuendekezwa ndani ya chama hicho kwa kutoshirikisha wanawake katika vikao vya uamuzi.

Alisema kitendo cha chama hicho kuendeleza uozo na udikteta katika kufanya uamuzi, huku pia kikiendeshwa kama kampuni ya wakubwa katika kufikia uamuzi mbalimbali.

Musori alisema uchaguzi halali wa Bawacha ulivurugwa na viongozi wa juu wa chama hicho, ili kutoa nafasi kutoa viti maalumu kwa wanaowataka badala ya kuachia vikao vya wanawake wa chama hicho kuamua kama zinavyoelekeza kanuni za Bawacha.

Musori alisema jambo lingine ni kutokubali utumwa wa Mwenyekiti Mbowe ambaye alidai hataki kupingwa katika uamuzi wake.

“Mimi nilikuwa nikipingana na Mbowe katika hoja mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupinga utaratibu wa Chadema ambao Mwenyekiti anakuwa mtia saini ilhali yeye ndiye Mwenyekiti wa vikao vya Kamati Kuu, Baraza Kuu na Mkutano Mkuu, ambavyo kimsingi ndio vyenye mamlaka ya kusimamia Sekretarieti ya chama,” alisema.

Aliongeza kwamba katika uchaguzi wa Bawacha, yeye alishika nafasi ya tano kwa kura zaidi ya 60 za wanawake wa chama hicho huku Suzan Lyimo akipata kura sita, Grace Kiwelo mbili na Halima Mdee saba, lakini hakuteuliwa katika uchaguzi wao wa wabunge 25 jambo ambalo si la kidemokrasia.

Alisema kutokana na uamuzi huo wa vigogo wa Chadema kuwanyima haki wanawake waliochaguliwa na wenzao, wengi watahama chama hicho ambacho alidai kipo kwa ajili ya maslahi ya wachache na hakina demokrasia.

Aliendelea kudai kwamba akiwa na cheo hicho cha Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Mjumbe wa Baraza Kuu la Chadema na Mweka Hazina wa Umoja wa Madiwani wa Chadema na kukidhi vigezo vilivyowekwa na viongozi hao, bado hakuteuliwa kuwa mbunge wa viti maalumu kutokana na kumpinga Mbowe.

Alisema amechukua uamuzi wa kuhamia NCCR - Mageuzi ili aendeleze mageuzi baada ya kufanya utafiti na kuona kuwa chama hicho ndicho kinamfaa na kusisitiza kuwa tatizo si kupata uongozi kwani alikuwa na vyeo vingi ndani ya Chadema.

Akimpokea mwanachama huyo na kumkabidhi kadi, Mbatia alitoa rai kwa wanasiasa kuzingatia haki kwa kila mmoja, kwani bila kutoa haki Taifa haliwezi kwenda vizuri, na alitaka haki ianzie kwenye familia hadi Taifa.

Septemba mwaka jana, kutokana na kilichoonekana ni mchezo mbaya ndani ya Chadema katika kutafuta uongozi wa Baraza la Vijana (Bavicha), kulitokea kutoelewana kambi, moja ikiwa ya Mwenyekiti Freeman Mbowe na nyingine ya Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe.

Mvutano huo ulisababisha uchaguzi kufutwa na Baraza la Wazee na hivyo aliyekuwa akiwania nafasi ya uenyekiti, David Kafulila wa kambi ya Zitto, kuhama chama na kujiunga na NCCR-Mageuzi na sasa ni Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia chama hicho.
 
Habari yenyewe inatoka gazeti la Habari Leo wame base kwenye matukio mawili yasiyo na mshiko wowote ile ya Mwenyekiti wa Mbeya ambaye amesharudishwa na Mwenyekiti wa BAWACHA ambaye ametoka kwa kukosa ubunge wa viti maalum sasa moto uko wapi. Ushauri kwa gazeti kama hamna habari si lazima kuandika habari za Chadema you are losing the direction.
 
Uteuzi wa VICKY KAMATA na kubadilishiwa makazi toka Msimbazi Centre Ilala, miezi michache kabla ya Uchaguzi Mkuu 2010, nao ulimshirikisha nani au kwa maslahi ipi hasa wakubwa???? Jibu swali hili hapa tafadhali au uombe THREAD kusitishwa hapa hapa.

Hivi umeseha habari yenyewe SOURCE yake ni wapi vile ... eti toka gazeti la 'Habari Leo'? Kama kama source ndio hiyo basi wala hamna haja ya kuendelea zaidi na mjadala hapa.
 
Vyama vingi vya siasa Tanzania Bara vilianza kugawanyika baada ya uchaguzi. Walianza NCCR-Mageuzi, na sasa hivi Chadema.
 
Habari leo Big Up!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Huyo kakosa Ubunge kakimbia acheni Majungu Habari leo mnalipwa Kodi za watanzaniaaaaa
 
Habari leo Big Up!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Huyo kakosa Ubunge kakimbia acheni Majungu Habari leo mnalipwa Kodi za watanzaniaaaaa

Eleweka sasa! Maana mwelekeo wako sijakupata mkuu. Unawapa shavu habari leo au vipi yaani?
 
Mambo kutokuwa shwari ni mazingira yasiyoepukika ndani ya chama cha siasa ambacho umaarufu wake mbele ya jamii unakua kwa kasi kama chadema. Hiyo ni changamoto kama zilivyo changamoto zingine. Muhimu hapa, ni namna viongozi wake wanavyoweza kutuliza akili na kutumia hekima na busara kukabiliana na changamoto hiyo. Makifanikio ya kuikabili changamoto hiyo, yanakisogeza mbele chama na kuwa imara zaidi.

Kwa hiyo, kwangu mimi hali kutokuwa shwari ninaichukulia kuwa ni fursa ya chama kujikomaza au kujipima namna kinavyoweza kukabiliana na changamoto. Vile vile, hali hiyo pia inaweza kuwa ni fursa kwa chama kusafisha uchafu uliomo ndani ya chama unaoweza kuwa umeletwa na 'rivals' wa chama kama vile ccm ambao hawachelewi kupandikiza mamluki wao ndani ya chama kinachoonekana kuwa ni tishio kwao. Viongozi wa chadema lazima watambue kuwa pigo walilowapatia ccm la kuchukua majimbo yote muhimu kwenye uchaguzi lilikuwa ni 'direct punch' ya usoni kwa ccm. Kwa hiyo, ccm inahaha na kutokana na hilo sitashangaa kamwe chadema itakapokumbana na migogoro mingi zaidi, ikilinganishwa na nyakati zingine zilizopita. Kama nilivyosema, muhimu ni viongozi wa chadema kutuliza akili na kutumia hekima na busara katika kukabiliana na changamoto hizo.
 
Kuchukua majiji ya Tanzania siyo kazi rahisi, lazima kuwe na mapandikizi wa ccm ambao hata hivyo hawatapata chochote, badala yake wataipa chama nguvu zaidi.
 
Wanaipa umaarufu ili mpaka vijijini waijue.
tatizo siyo chadema,ila kwamba inapendwa mno.ccm wamehamisha watendaji wangapi ambao wameshindwa kwenye maeneo yao.kumuengua sita uspika ni jambo dogo? Wale waliofunga ofisi rukwa? Walioandamana arusha, waliofukuzwa bkb? Nk.ukweli ni kuwa hakuna anayejali habari za mzoga ccm.lakini habari ya keki chadema inapendwa na kila mtu hata ccm yenyewe na vibaraka wao kama habarileo,taifa huru na ,cufnccrudptlpccm,
 
Kila siku CHADEMA CHADEMA CHADEMA HII IKOJE,MAANA YAKE NINI?HAYA NI MAELEZO MAFUPI;

  • Ni chama mbadala wa ccm
  • Ni chama kilichokuwa na wabunge wengi zaidi wa upinzani katikati bunge la JMT
  • Ni chama kilichoshika kasi ya aina yake kwa ukuaji wa Democrasia Tanzania
  • Ni chama chenye msimamo kisichoyumba mpaka sasa
  • Ni chama kinachoongozwa kwa mujibu wa katiba na sheria za Nchi
  • Ni chama chenye itikadi ya kisiasa
  • Ni chama kilichoenea sehemu zote Tanzania pamoja na mapungufu ya bajeti yake
  • Ni chama pekee kilichodiriki kuyakataa matokeo ya urais waziwazi bila kuficha
  • Ni chama kilichodhihirisha ulimwengu kuwa rais aliyeingia madarakani kaingia kwa wizi wa kura kwa kutoka nje ya bunge wakati alipotaka kuanza kuhutubia bunge.
  • Ni chama kitakachosimamia uundaji wa katiba mpya mpaka sasa.
  • Ni chama kilichoonesha UPINZANI wa kweli ndani na nje ya bunge.
 
amehamia nccr mageuzi kwa sasa baada ya kukosa viti maalumu ndani ya chadema huku akitoa shutuma za udini,ukabila na kila aina ya ubaguzi ambao anadai upo ndani ya chadema.
kwa umri wake hakupaswa kusema hayo yote,hivi muda wote wa utumishi wake ndani ya chadema hakuyaona hayo anayoshutumu kwa sasa?
Amejikwaa,amepotea njia,amekuwa mfa maji na sasa anatapatapa,akumbuke utu uzima dawa,akae kimya kama amegundua kuna uozo chadema na aelekee kule anakokuona kwake ni sahihi.chadema si yeye bali ni taasisi ya watu wenye mapenzi mema,wapenda mabadiliko,wazalendo na wanaharakkati wa kweli
 
Kila siku CHADEMA CHADEMA CHADEMA HII IKOJE,MAANA YAKE NINI?HAYA NI MAELEZO MAFUPI;

  • Ni chama mbadala wa ccm
  • Ni chama kilichokuwa na wabunge wengi zaidi wa upinzani katikati bunge la JMT
  • Ni chama kilichoshika kasi ya aina yake kwa ukuaji wa Democrasia Tanzania
  • Ni chama chenye msimamo kisichoyumba mpaka sasa
  • Ni chama kinachoongozwa kwa mujibu wa katiba na sheria za Nchi
  • Ni chama chenye itikadi ya kisiasa
  • Ni chama kilichoenea sehemu zote Tanzania pamoja na mapungufu ya bajeti yake
  • Ni chama pekee kilichodiriki kuyakataa matokeo ya urais waziwazi bila kuficha
  • Ni chama kilichodhihirisha ulimwengu kuwa rais aliyeingia madarakani kaingia kwa wizi wa kura kwa kutoka nje ya bunge wakati alipotaka kuanza kuhutubia bunge.
  • Ni chama kitakachosimamia uundaji wa katiba mpya mpaka sasa.
  • Ni chama kilichoonesha UPINZANI wa kweli ndani na nje ya bunge.

Ni chama pekee cha UPINZANI hapa nchini,vingine vyoooooote ni mapandikizi ya Chama cha Mafisadi(CCM)
 
amehamia nccr mageuzi kwa sasa baada ya kukosa viti maalumu ndani ya chadema huku akitoa shutuma za udini,ukabila na kila aina ya ubaguzi ambao anadai upo ndani ya chadema.
kwa umri wake hakupaswa kusema hayo yote,hivi muda wote wa utumishi wake ndani ya chadema hakuyaona hayo anayoshutumu kwa sasa?
Amejikwaa,amepotea njia,amekuwa mfa maji na sasa anatapatapa,akumbuke utu uzima dawa,akae kimya kama amegundua kuna uozo chadema na aelekee kule anakokuona kwake ni sahihi.chadema si yeye bali ni taasisi ya watu wenye mapenzi mema,wapenda mabadiliko,wazalendo na wanaharakkati wa kweli

Sizitaki mbichi hizi, njaa inamsumbua, na alipoenda njaa ni kali zaidi
 
Acheni kumlaumu huyo mama rather is high time to real think about this very country!

wanachadema hamna hata haja ya kumzungumzia, maana vidole vingine vinawanyooshea wenyewe!

Slaa alihama CCM for likely reasons! unataka niseme nini juuu ya Mpendazoe, Marando, Shibuda......

If she is right then chadema must act on it accordingly is not a first time we hear the same accusations, we have been hearing this for years now, since late Wangwe, come to Kafulila and many more............................However..it is common you should know politics.. even csame NCCR people are running away!

why waste time to blame her? you may fail to defend your chama simply....remember Slaa....

Leave her, wabunge wa kuteuliwa ndani ya chadema bado kuna ugomvi mwingi na tuhuma nyingi sana, however, those are politics..

lets think of new katiba and NEC
 
Back
Top Bottom