Majina ya waliokuwa wamefaulu katika usaili wa ajira Serikalini, kufutwa.

Babu wa Kambo

JF-Expert Member
May 2, 2016
559
807
Watu wote waliokuwa wamefanya usaili kwa ajili ya ajira serikalini kupitia Sekretarieti ya Ajira ya Utumishi wa Umma kabla ya ajira kusimamishwa, watafutwa ndani ya miezi 6 na kulazimika kuomba upya kipindi ajira hizo zitakapotangazwa tena.

Hilo limebainishwa na sekretarieti hiyo kupitia majibu kwa wadau mbalimbali kwa mwezi Desemba ambao wamekuwa wakiuliza maswali na kujibiwa kila mwezi kupitia tovuti yake, na kubainisha kuwa suala hilo litawahusu wale ambao walifaulu usaili lakini kabla hawajapangiwa vituo vya kazi au kupewa barua na waajiri wao, ajira zikasimamishwa ili kupisha uhakiki wa watumishi hewa.

Taarifa hiyo imesema kuwa huo ni utaratibu wa kawaida wa sekretarieti hiyo, kwamba majina ya waliofaulu huhifadhiwa kwenye kanzi data (Database) kwa muda usiozidi miezi sita, na baada ya hapo majina hayo hufutwa.

"Kwa mujibu wa Taratibu zetu za uendeshaji wa mchakato wa ajira majina ya waombaji kazi waliofaulu lakini hawakupangiwa vituo vya kazi kwa sasa huhifadhiwa kwenye kanzi data kwa muda usiozidi miezi sita" Imesema taarifa hiyo

Swali lingine kutoka kwa mdau na jibu lake liko kama ifuatavyo:-

Kwa kuwa ajira zilisitishwa mwezi Juni, na sasa ni mwezi Desemba, utaratibu huo unamaanisha kuwa wasailiwa wote waliofaulu lakini hawakupangiwa kazi, watalazimika kusubiri upya matangazo ili waombe upya na kufanya usaili upya.
 
Pole yao. Mjiajiri ndiyo wimbo wa sasa lkn kuna viongoz wamekaa madarakan miaka na miaka na wengine hawataki hata kutoka mpaka wanapiga ngumi watu, wanachakachua matokeo, wanatoa rushwa, na wengine kweny compaign zao za uchaguzi zinageuka kuwa Fiesta, lkn hao hao watakuambia mjiajiri. Haya bana ss tumeshika kwenye makali na nyie meshika kweny mpini.
MAISHA LAZIMA YA ENDELEE. UKITEGEMEA SERIKAKI YETU HII, UTAKUFA NA NJAA. TUKUTANE 2020 SIJUI ZILE AHADI ZA MILION 50 KILA KIJIJI NA NCHI YA VIWANDA WATATIMIZA? Au watasema tuwape muda tena miaka 5. Mm wala sijui.
 
Back
Top Bottom