Majina ya walio na wasioteuliwa kugombea Ubunge wa Afrika Mashariki

i pad3

JF-Expert Member
Mar 16, 2012
1,518
378
Majina ya walio na wasioteuliwa kugombea Ubunge wa Afrika Mashariki 14/04/2012

1.0 Tarehe 9 Machi, 2012 nilitoa Tangazo kwa vyombo vya habari na gazeti la Serikali juu ya kuwepo kwa nafasi Tisa wazi za Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki kufuatia kufikia ukomo wa maisha ya Bunge la sasa hapo 04 Juni, 2012. Katika Tangazo hilo niliwaomba wananchi wenye sifa za kugombea nafasi hizo wafanye mchakato wa kugombea kupitia vyama vyao vya Siasa na fomu za wagombea waliopendekezwa zirejeshwe Ofisi ya Bunge kabla ya saa 10.00 jioni tarehe 10 Aprili, 2012 ambayo ndiyo siku ya uteuzi. Jumla ya Wagombea 34 kutoka Vyama vya Siasa vya CCM, CHADEMA, CUF, NCCR-MAGEUZI, TLP, UDP na TADEA wamerudisha Fomu.

2.0 Zoezi la uteuzi limekamilika, Wajumbe 33 wametimiza masharti ya uchaguzi kwa mujibu wa Mkataba wa kuanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kanuni za Bunge, hivyo, wameteuliwa kugombea nafasi hizo. Aidha, Mgombea mmoja hakutimiza masharti ya uchaguzi ya kuthibitisha uraia wake na kulipa ada ya uchaguzi kwa mujibu wa Kanuni 5(3) na 6 ya Nyongeza ya Tatu ya Kanuni za Bunge, hivyo hakuteuliwa kugombea.

Ifuatayo ni Orodha ya Wagombea walioteuliwa na wasioteuliwa kugombea nafasi za Ubunge wa Afrika Mashariki:-
1. WAGOMBEA WALIOTEULIWA
KUNDI A: WAGOMBEA WANAWAKE
S/NO.
JINA
CHAMA
1.
Nd. Angela Charles Kizigha
CCM
2.
Nd. Fancy Haji Nkuhi
CCM
3.
Dkt. Godbertha Kokubanza Kinyondo
CCM
4.
Nd. Janet Deo Mmari
CCM
5.
Nd. Janet Zebedayo Mbene
CCM
6.
Nd. Maryam Ussi Yahya
CCM
7.
Nd. Rose Daudi Mwalusamba
CUF
8.
Nd. Sebtuu Mohamed Nassor
CCM
9.
Nd. Shy-Rose Sadruddin Bhanji
CCM
10.
Nd. Sofia Ali Rijaal
CCM

KUNDI B: WAGOMBEA WA ZANZIBAR

S/NO.
JINA
CHAMA
1.
Nd. Abdullah Ali Hassan Mwinyi
CCM
2.
Dkt. Ahmada Hamad Khatib
CCM
3.
Dkt. Haji Mwita Haji
CCM
4.
Nd. Khamis Jabir Makame
CCM
5.
Dkt. Said Gharib Bilal
CCM
6.
Nd. Zubeir Ali Maulid
CCM

KUNDI C: WAGOMBEA WA VYAMA VYA UPINZANI

S/NO.
JINA
CHAMA
1.
Nd. Antony Calist Komu
CHADEMA
2.
Dkt. Fortunatus Lwanyantika Masha
UDP
4.
Nd. Juju Martin Danda
NCCR-MAGEUZI
5.
Nd. Micah Elifuraha Mrindoko
TLP
6.
Nd. Mwaiseje S. Polisya
NCCR-MAGEUZI
7.
Nd. Nderakindo Perpetua Kessy
NCCR- MAGEUZI
8.
Nd. Twaha Issa Taslima
CUF

KUNDI D: WAGOMBEA WA TANZANIA BARA

S/NO.
JINA
CHAMA
1.
Nd. Adam Omar Kimbisa
CCM
2.
Nd. Bernard Musomi Murunya
CCM
3.
Nd. Charles Makongoro Nyerere
CCM
4.
Dkt. Edmund Bernard Mndolwa
CCM
5.
Nd. Elibariki Immanuel Kingu
CCM
6.
Dkt. Evans Mujuni Rweikiza
CCM
7.
Nd. John Dunstan Lifa-Chipaka
TADEA
8.
Nd. Mrisho Mashaka Gambo
CCM
9.
Nd. Siraju Juma Kaboyonga
CCM
10.
Nd. William John Malecela
CCM

2. MGOMBEA AMBAYE HAKUTEULIWA

S/NO.
JINA
CHAMA
1.
Nd. Mohamed Abdulrahman Dedes
CUF

3.1 Hivyo, bila ya kuathiri shughuli nyingine zitakazopangwa na Bunge, tarehe 17 Aprili, 2012 saa Nne na nusu asubuhi au muda mfupi baada ya hapo nitawasilisha majina ya Wagombea kwa wapiga kura.

Napenda kutoa shukrani kwa Wagombea wote kwa ushirikiano wao katika kukamilisha zoezi hili la uteuzi. Aidha, tunawaomba wapiga kura, wakati utakapofika, wazingatie matakwa ya Sheria na Kanuni zinazotawala chaguzi hizi.

Imetolewa na:

Dkt. Thomas D. Kashililah

KATIBU WA BUNGE NA MSIMAMIZI WAUCHAGUZI
BUNGENI DODOMA

14 APRILI, 2012

Source: Majina ya walio na wasioteuliwa kugombea Ubunge wa Afrika Mashariki - wavuti.com 
 
Duu,naona kuna hadi mtoto wa makamu wa rais aitwae Said Gharib Bilal,na pia kuna mtoto wa Malechela,kwa staili hii ya kurithishana vyeo hatofika yaani utafikiri hakuna hakuna watanzania wengine wenye uwezo wa kugombea kupitia CCM wakati wapo kibao tu.
 
Kuna familia ambazo watoto hufuata nyayo za wazazi wao,kama walimu,madaktari,askari n.k.Ndivyo ilivyo kwa wanasiasa. Hata hivyo jaribu na wewe kugombea kama una sifa na uwezo kuliko kulialia tu.
 
Haya haya @Le Mutuz naona ukuu unabisha hodi taratiiibu. Haya bana, hongera zako ingawa haibadilishi msimamo wangu kwamba bado hujafaa kutuwakilisha E.Africa, labda ya miaka mitano.
 
Kuna familia ambazo watoto hufuata nyayo za wazazi wao,kama walimu,madaktari,askari n.k.Ndivyo ilivyo kwa wanasiasa. Hata hivyo jaribu na wewe kugombea kama una sifa na uwezo kuliko kulialia tu.

Si vibaya mtoto akirithi taaluma ya mzazi wake wala hilo halina shida endapo mtoto atataka kuwa daktari ,mwalimu au mhandisi kama baba/mama yake. hoja ya msingi ni kulithishana vyeo vya kisiasa ambavyo havihusiani na taaluma! hilo halikubaliki na inapaswa likemewe na wapenda haki wote.watoto wengi wa maskini lakini wana uwezo mzuri tu wa kiungozi wanapigwa zengwe lakini watoto wa vigogo wanapeta! nasema hili halikubaliki hata kidogo hii ni nchi yetu sote. maskini na matajiri na mtu achaguliwe kwa sifa kupitia ushindani ulio sawa.
 
Wabunge wetu nao sasa have come of age naamini watakula hela za wale waliozoea kuhomga lakini katika kuchagua, hizo hongo hazitakuwa na nafasi ya kuinfluence uamuzi wao makini na mwisho wa yote watatuchagulia watu wenye weledi, wazalendo wenye afya safi ambao watakuwa tayari kuwatumikia wananchi.
 
Si vibaya mtoto akirithi taaluma ya mzazi wake wala hilo halina shida endapo mtoto atataka kuwa daktari ,mwalimu au mhandisi kama baba/mama yake. hoja ya msingi ni kulithishana vyeo vya kisiasa ambavyo havihusiani na taaluma! hilo halikubaliki na inapaswa likemewe na wapenda haki wote.watoto wengi wa maskini lakini wana uwezo mzuri tu wa kiungozi wanapigwa zengwe lakini watoto wa vigogo wanapeta! nasema hili halikubaliki hata kidogo hii ni nchi yetu sote. maskini na matajiri na mtu achaguliwe kwa sifa kupitia ushindani ulio sawa.

Mhunzi huzaa Mhunzi!

Nafasi za kisiasa zinashindaniwa, jitokeze...usisubiri viti maalum!

Kwa case hiyo ya EALA mgombea ambaye hakupitishwa ni mmoja tu, na huenda kuna sababu nzito. Tujitokeze, ili kuondoa dhana ya nafasi hizo kuwa za urithi.
 
Baada ya miaka 3 CCM ikiendelea kuongoza, asilimia hamsini ya baraza la mawaziri. itakuwa ni Watoto wa viongozi.
 
Kwa CCM ni sawa kila mtu alikuwa na haki ya kugombea hakuzuiliwa mtu kwa kule zanzibar wanaume waliongombea walikuwa 8 wawili wakatolewa na kura zilizopigwa na wabunge wa CCM na kuna kila sababu ya kutolewa la kwanza uzowefu mmoja ndio kwanza amemaliza shule mwaka jana postgraduate na miaka yake 32 wa pili hata sifa hana na huyo Dkt said gharib ni ndugu yake na siyo mwanawe na ni mzowefu na hii itakuwa awamu yake ya pili akipitiswa ana phd kutoka kule marekani miaka kumi na sita iliyopita na wengine wakiobakia sita kwa kuwa chama cha CCM ni makini na imejiamini wote wamepelekwa wakapigiwe kura na wabunge wote kutokana na watavyouza sera na ufahamu wao kwenye mbuge hilo la EAC
 
Back
Top Bottom