Majina ya wagombea Ubunge jimbo la Kinondoni yatoka, Mgombea wa UKAWA akatwa

you make it sound like it's so simple,,, hata hivyo lazima ujue kuwa hizi sheria ni za muhimu mara elfu zaidi ya huyo mgombea chekibobu mmoja,,

And it is simple. Sioni chochote cha kukwaza hapa. Hujajibu swali lake? Watu wote tunatakiwa tuwajue mahakimu kwa sura? Jibu ni hapana. Tunatakiwa tujue zilipo ofisi na tunadili na ofisi!
 
Ninawasiwasi na hao wagombea wanaokatwa kwa kutokukidhi masharti ya kuteuliwa wengine wanavuta mpunga halafu wanafanya wanavyojua
 
Hivi hizo form za ubunge huwa ni karatasi mia ngapi mpaka wachanganye madesa.

BTW:Hizi kasoro ndogo ndogo busara ingetumika tu na siyo kuenguana.

Ngoja tuone.
Kiapo cha hakimu sio kasoro ndogo,kwa maana hiyo hata Raisi atakiuka katiba ya nchi tutasema kasoro ndogo.
 
Naona umuhimu wa ku negotiate na Zitto ili majimbo yote yenye mizengwe tuwape ACT sababu lengo letu kuu ni kuiondoa CCM na mengine ndio yafuate.
 
Kuna jina lolote umeliona pale.?


Mkuu huoni hapo jina la hakimu na sahihi.Nani kadhibitisha ni karani?
attachment.php
 
Saini imeandikwa SAINI YA HAKIMU............................. nA IMESAINIWA , JE SIO YEYE KIVIPI?
 
CUF ya Lipumba hiyo - Killing softlly.

Mwingine huko Ntwara kazima simu kasepa bila kurudisha form. UKAWA mlitakiwa kuwa makini kwenye makosa madogo madogo kama haya!!

Ngoja tusubiri rufaa.
 
Kuna haja sasa ya kurekebisha kanuni za NEC kutoruhusu mgombea kuondolewa kwa kasoro ambazo zinaweza kurekebishwa otherwise huo unakuwa siyo uchaguzi bali ni mbinu za kupitisha watu kwa mizengwe.

Siku zote wananchi wamekuwa wanalalamika kuwa viongozi wengi huenda wana-sign mikataba bila kujua wanasign nini? hawasomi, na wakisoma hawaonekani kuelewa!

Sasa kama Mbunge yaani mjube katika chombo cha kutunga sheria (Bunge) hawezi hata kutimiza sharti dogo la kisheria kama hilo atawezaji kuchambua miswada?
 
Kumbukeni DC wa Kinondoni ni Paul Makonda.

Huyu anaweza kufanya lolote kuibeba CCM. Chunguzeni vizuri. Saini hiyo ni ya hakimu.
 
Naona umuhimu wa ku negotiate na Zitto ili majimbo yote yenye mizengwe tuwape ACT sababu lengo letu kuu ni kuiondoa CCM na mengine ndio yafuate.

Wewe unacheza na Zitto, kote ambako ccm wamepita bila kupingwa zitto hakuweka wagombea kwa vile ni kwa maswahiba wake! Wacha tu yaende ccm labda tutatia akili! Inakuwaje unapeleka fomu isiyokuwa na jina la Hakimu? Hizo ofisi za chama zinafanya kazi gani? Tanzania elimu yetu ndogo sana!!
 
Nimeona kwenye uchaguzi mwaka huu, wagombea wanaviziana kwa kutafutiana sababu za kutokujaza fomu vizuri, au kujaza kwa na mtu asiyehusika nk
swali ni inakuwaje mtu anatoa kiapo wakati haruhusiwi kisheria? yaani mfanyakazi wa mahakamani asiye hakimu anapokea fomu ya mgombea anagonga na mihuri huku akijua yeye hana mamlaka ya kufanya hivyo? sasa ni muda wa kupigia kelele kwa mtu either kupigwa faini ya kukosea kujaza fomu na sio kuenguliwa maana inapelekea kupata viongozi matangopoli.
 
Hii fomu ya Mgombea Ubunge wa CUF ( UKAWA ) imesainiwa na karani wa mahakama badala ya Hakimu. Ndio maana jina la Hakimu halikuandikwa. Ni kosa kisheria..Na ndiyo sababu ya mgombea huyo wa UKAWA Kuenguliwa.

View attachment 280136

Kutoka kwa Kado Cool

imesainiwa imesainiwa na hakimu na muhur wa hakimu sasa koa lipo wapi ? kama mahakma yenyewe wamefanya khiana nini kosa ?

hili lisiachiwe kupita hivi hivi jimbo litakwenda kwa wasughulikana sembe. ikatwe appeal tume ya uchaguzi ikiwezakana jimbo liwekewe pingamizi . hili jimbo rahisi sana Iddi Azan washamchoka .tusikubali ujinga huu
 
Ukawa kwa hili mkubali kuwa hamko makini! Ilipaswa kwanza kutangaza mwisho was kurudisha fomu kwa ukawa muda ambao ungekuwa ni mapema zaidi ya ule wa tume. Pili fomu ingekaguliwa kwanza na MTU makini aliyeidhinishwa na ukawa kabla ya kuirudisha kwenye tume.
Hayo hayakufanyika, tukubali tumeshafungwa goli la kisigino wala si la mkono katika hili! Ni goli halali! tupende tusipende, hii si bahati mbaya! Kuna mkono wa ccm hapa, huu ni ushindani! Inakera na kuuma sana lakini ukawa tukubali katika hili tumezidiwa mbinu na tumefungwa goli la kisigino!
 
Kwanini kila uchaguzi yanatokea na watu hawajifunzi? Huyo wa IPPT MAENDELEO apigiwe kura za hasira
 
Back
Top Bottom