Majina ya Wabunge Viti Maalum hadharani: CCM-64, CHADEMA-36, CUF-10

yule dada alijiondoa jimboni na akaapa mahakani na hakupiga kampen..NEC wakarudisha jina lake..hiyo kesi ukawa watashinda saa moja asubuhi, uchaguzi unarudiwa pale...so hana kosa kabisaaa
Upo sahihi Mkuu, Segerea kuna uhakika wa kurudia soon.
 
Wasiompenda kaja... Kelele za Ester Bulaya, Ester Matiko, Halima Mdee, Zimepata dawa

kuna tofauti ya nafasi za fadhila na nafasi za kugombaniwa.
huwezi mlinganisha shonza na mdee au bulaya.
ni kichaa tu anayeweza kuwalingani hao. mwingine atakuwa anakisemea chama ili kiendelee kumteua na mwingine anawasemea wananchi. kuna utofauti mkubwa sana
 
Wewe Ben hawajafikiria kukupa viti maalum? By the way Juliana aliongoza kwenye mkoa wake wa Songwe. Na waliochukuliwa ni wale walioongoza kwenye mchujo
mkuu Lizaboni utani mwingine sio mzuri ujue, Ben anapewaje viti maalum.. the teh
 
Last edited by a moderator:
Hivi nyie Chadema waislam wamewakosea nini nafasi zote hizo waislam hawazidi kumi?

Ulitaka waende mtaani kuwatafuta!! CUF wakitoa list yao mtakuja na lingine. Typical Tanzania. Divide and Rule is working well in this country!!
 
Huyo mtoto wa lubuva ameingiaje , atolewe mana baba yake alituhujumu UKAWA

Huku watu wanamagufulika, kummbe wewe bado unalowa! mambo hayo yalishaisha kipindi na watu wameanza kazi, si umeona jana hazina, fanya kazi muda ni mali
 
Hivi CHADEMA wameshatangaza hayo majina?

Maana haya yaliyoko humu sidhani kama ni rasmi...

BTW, Napenda sana huyu dada aingie Bungeni...
1609773_744424918923608_95056372242560335_n.jpg
 
Ila jamani hawa watu vipI...UMMY MWALIMU..SOFIA SIMBA...ANGELA KAIRUKI... si wagombee majimbo na wao vikongwe lkn wanataka kubebwa wathubutu mbona kina ester wameweza...mnatuangusha bana mnaonyesha udhaifu mtapewa pewa mpk lini...kutokujuamin
 
Ficha ujinga wako kama alikuwa hakubaliki na huyo ana ndio anakubalika mtatiro alipataje kura elfo 70 na huyo Dada yako elfu 40? wewe unakaa segerea ya wapi? kama huyu Dada akipitishwa viti maalumu bila ya maelezo ya kutosha nitajitoa, tumeumizwa sana kukosa jimbo kizembe.
Umeandika kwa hasira sana ndugu yangu. Je huyo binti alipata kura hizo elfu 40 baada ya kufanya kampeni au ni kweli kwamba hakufanya kama mwandishi unayemjibu alivyosema? Binafsi nafikiri mfumo wa kuachiana majimbo waliufanya karibu sana na uchaguzi na kuwachanganya wapiga kura. Wangetoa muda wa kuwaeleza wapiga kura na wale washindani wangeshirikiana katika kampeni baada ya kupatanishwa na 'kuponya madonda' ya kuenguliwa. Lakini sasa huyu binti wa watu mnamuandama bure kwa sababu naye alishawekeza na alikuwa na wafuasi (elfu 40)waliokuwa wakimtaka agombee na kama mwanasiasa si rahisi yeye kufanya maamuzi ya kuwaudhi kwa manufaa ya siku za usoni.
 
Haswa kwa vyama vya upinzani inakuwaje jimbo lina mbunge wa kuchaguliwa tayari alafu bado linaongezewa mbunge wa viti maalum? Kwanini nafasi hizo zisiwe kwa majimbo ambayo hayana upinzani?

Niko tayari kukosolewa
 
Back
Top Bottom