figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,890
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) leo imetangaza idadi ya wabunge wa viti maalumu ambao vyama vya CCM, CHADEMA na CUF vimepata baada ya kupata angalau asilimia 5 ya kura zote halali za wabunge nchi nzima.
Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema chama cha CCM ambacho kilipata jumla ya kura milioni 8.3 kimepata wabunge 64 wakati chama cha CHADEMA ambacho kilipata kura milioni 4.7 kimepata wabunge 36
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), leo imetangaza idadi ya Wabunge wa Viti Maalum, ambao vyama vya CCM, Chadema na CUF vimewapata baada ya kupata asilimia zote halali za wabunge nchini.
Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu, Damian Lubuva, amekaririwa na FikraPevu akisema Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho kilipata jumla ya kura milioni 8.3 kimepata wabunge 64, wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambacho kilipata kura milioni 4.7 na sasa kimepata wabunge 36, huku Chama Cha Wananchi (CUF) kilichopata kura milioni 1.2 kikipata wabunge 10.
Aidha, amebainisha kuwa wabuge wa viti maalumu vya ubunge ni viti 113, wakati viti 5 vitatoka baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Jaji Mstaafu Lubuva, ameeleza kuwa majina ya wabunge hao yatapatikana kwenye Ofisi za vyama husika.
Hata hivyo, amesema kutokana na kuwepo kwa majimbo 8 ambayo hayakufanya uchaguzi, mgawanyo wa viti maalumu, kwa sasa ni 110 ambapo viti 3 vilivyobaki vitagawanywa baada ya kufanyika kwa uchaguzi katika majimbo hayo.
Soma zaidi => Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) yatangaza idadi ya Wabunge wa Viti Maalum