Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,695
- 40,721
Praying Mantis
Hivi anaitwaje kwa Kiswahili?
Hivi anaitwaje kwa Kiswahili?
Last edited by a moderator:
Jama, na 'dragonfly' wanaitwa nini kwa kiswahili?
Najua jina la Kisukuma ni 'shilondela', direct translation is pursuer or chaser.
SteveD.
Hivi anaitwaje kwa Kiswahili?
Dragonfly wanaitwa 'Kereng'ende' kwa kiswahili
Jioni njema.
Je, Koboko ndiyo king-cobra?!
Hivyo Tanzania wapo Cobra? Halafu yule ndege anaitwa Dudumizi analo jina la kiingereza?
Halafu kuna vile vindege vidogo hupenda kuruka kwa makundi (siyo mbayuwayu) yaani ni vidogo kweli sijui vinaitwaje, nimekuwa nikitafuta jina lake kwa muda mrefu sasa.
Ngao, Take 5!! Yaani umenikumbusha mbali sana... ni kama vile tumekua pamoja toka utotoni. Hizo tales kuhusu jinsi ya kuua koboko ni sawa sawa kabisa na zile nilizosimuliwa mimi. Yaani ni kubeba uji wa moto kwenye chungu na kata nzito, uji uliomzito sana... ili akijilengesha tu na kudonyoa kichwani anajikuta kazamisha kichwa chake chenye ('usunzu'- in sukuma au 'cock-crown' kwa waingereza nadhani) ushungi kwenye uji.SteveD,
Kuhusu koboko na king cobra nadhani ni nyoka wawili tofauti kwa sababu:
Koboko (japo sijawahi kumuona kwa macho)nafahamu anapatikana sana maeneo ya msitu ya miombo hususan kule Kigoma na Tabora.Habari zinaeleza kuwa ana ushungi kama wa jogoo!! Kama umesikia juu ya nyoka anayevizia watu kwa kujificha kwenye matawi ya miti na kuwadonoa wapitapo chini. Pale Bulombora JKT tulipata sana habari kama hizi. Na namna ya kumtega na kumuua ni kwa wanawake kubeba mitungi yenye uji wa moto na kupita eneo aliloko huyu koboko, ambapo atajitumbukiza kichwa kichwa kwenye uji wa moto!
Cobra kwa upande mwingine, habari zinaeleza kuwa anapatikana zaidi Asia, hususan India na ana umbile la mashavu(?) makubwa ambayo hujivimbisha anapoghadhabika.
Hebu tupate maoni ya wengine wajuao zaidi labda.
Ngao you are right kwa koboko si King Cobra ila ni Black mamba ambaye rangi yake si mweusi ila kijani hafifu ila ndani ya mdomo ndiyo mweusi.King cobra wapo wa Asia na wa Misri wote wana vimbisha mashavu.
Hivyo Tanzania wapo Cobra? Halafu yule ndege anaitwa Dudumizi analo jina la kiingereza?
Halafu kuna vile vindege vidogo hupenda kuruka kwa makundi (siyo mbayuwayu) yaani ni vidogo kweli sijui vinaitwaje, nimekuwa nikitafuta jina lake kwa muda mrefu sasa.
T-1!Nadhani Cobra kwa Kiswahili anaitwa KIFUTU
Nadhani Tanzania wapo Cobra. Nakumbuka nimeshawahi kumuona mtoto wa Cobra miaka mingi iliyopita. Labda macho yangu yawe yalindanganya akuwamdgo sana.
Kuna ndege wadogo warukao kwa makundi. Wana kelele sana, na vidari vyao ni vya njano. Wanaitwa USIGI. Sijui km ni hao uwazungumziao.
Nadhani sehemu za pwani wanaitwa kumbi-kumbindiyo kuna senene, panzi, halafu wale wanaoliwa wako kama mchwa wanaitwaje, hasa kule kwenye "bomba hii, nyumba hii" wana mafuta hao!!
T-1!
Za siku ndugu?!... hapa sina hakika kwa kweli, inawezekana you are right, lakini nadhani kifutu ni tofauti... kifutu kwa jinsi ninavyojua mimi ana rangi nyingi nyingi (kama za chatu hivi), na ni mfupi sana ila mnene. Sumu yake kwa wenye bahati mbaya ya kung'atwa naye nikuwa ina ozesha miguu au kiungo. Kwa hisia zangu mimi nafikiri kifutu ni rattle snake kama wale wa kule America. Kifutu hana hasira kama cobra.
Cobra ni mweusi na kule kanda ya ziwa tuna mwita Swila. Nadhani ulishawahi sikia hili. Na kama nilivyosema mwanzoni kabisa nadhani hili jina linaweza kunyambulishwa na kuwa neno la kiswahili. Jina swila linatokana na kutema mate, kama unavyojua, cobra are notorious kwa kutema mate, hence jina swila.
SteveD.
ndiyo kuna senene, panzi, halafu wale wanaoliwa wako kama mchwa wanaitwaje, hasa kule kwenye "bomba hii, nyumba hii" wana mafuta hao!!
Hivyo Tanzania wapo Cobra? Halafu yule ndege anaitwa Dudumizi analo jina la kiingereza?
Halafu kuna vile vindege vidogo hupenda kuruka kwa makundi (siyo mbayuwayu) yaani ni vidogo kweli sijui vinaitwaje, nimekuwa nikitafuta jina lake kwa muda mrefu sasa.
SteveD,
Tupo, ndugu yangu! Hilo jina T-1 nimelipenda sana! Ni fupi na limetulia. I wish I could adapt it; need your advice.
Nimemkumbuka Kifutu baada ya kunitajia maumbile yake. I think I was wrong. Vilevile, niliwahi kusikia hilo jina "Swila" somewhere. Sikumbuki km muongeaji alikuwa mwenyeji wa kanda ya ziwa. What I want to say ni kwamba baadhi ya maneno ya Kiswahili yanaazimwa kutoka ktk lugha za makabila; hivyo, inawezekana hata hilo jina Swila likawa limeazimwa kutoka huko kanda ya ziwa, na kukubalika ktk Kiswahili. I'm not sure.
Nakumbuka kuwa rattle snake ni mrefu; kiasi cha kuweza kujivingirisha na sehemu ya mkia wake kuwa juu. Akiwa ktk hali hii, anauchezesha huo mkia ambao hutoa rattling sound (and hence the name) na kuwaonya viumbe wengine, hasa binadamu, kuwa "nipo hapa, angalia usinikanyage kwani nina sumu kali sana".
SteveD, hivi wale mijusi yenye rangi nyingi wanapatikana Mwanza tu? Au kanda ya ziwa tu? Wanaitwaje?
T-1
SWILA NI NYOKA MWEUSI na anatema mate(spitting cobra)KIFUTU NI NYOKA MFUPI NA MNENE ana rangi kama za chatu na ni mpole labda umkanyage ndiyo anauma. Ni kweli anaozesha muscles. Koboko ni kweli si wa kijani kabisa ila ni kati ya kijivu na kijani( Black mamba) black ina refer to the colour of its mouth. It is the fastest snake in the world and also the most poisonous.(3 minutes if not given aid you die) Njia ingine ya kumkamata au kumuua ni kupambana naye kwa kumtupia majani mabichi ya mkonge. Akiyauma yanakuka. So you throw mengi mpaka poison ina isha na jani kubakia bichi na la kijani.Kumbikumbi ni mchwa na kwetu tunawaita "NSWA" tulikua tuna export Zambia siku zileeeee.