Majina ya vituo vya kuchimba dawa kwa abiria wawapo safarini. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majina ya vituo vya kuchimba dawa kwa abiria wawapo safarini.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Twilumba, Sep 1, 2012.

 1. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,142
  Likes Received: 869
  Trophy Points: 280
  Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) ilifanya kikao na wasafirishaji na kuweka mikakati ya utekelezaji wa agizo la Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe katika Mkutano wa Nane wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2012 uliomalizika hivi karibuni mjini Dodoma, alipotangaza kukataza tabia ya abiria ya kushuka maporini na kujisaidia ‘kuchimba dawa' ifikapo leo.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyopo kwenye tangazo la SUMATRA kwa vyombo vya habari, itawalazimu abiria kuwa na kiasi cha fedha cha ziada kwa ajili ya kulipia huduma ya maliwato. Hata hivyo, taarifa hiyo haikusema lolote kuhusu watoto na wale ambao wana matatizo ya kupata haja ndogo kila baada ya muda mfupi.

  Kwa mujibu wa tangazo la SUMATRA vituo vilivyoainishwa katika barabara kuu tano ni:

  Dar es Salaam - Mbeya

  Vituo vilivyoainishwa ni mikoa ya Pwani, Morogoro, Iringa na Njombe. Vituo hivyo ni Ruvu iliko hoteli inayotoa huduma hiyo bure, Chalinze kuna hoteli inahudumia kwa Sh 200; stendi kuu ya mabasi ya Msamvu huduma inatolewa kwa Sh 200 na Ruaha Mbuyuni Hoteli ya Al Jazeera inatoa huduma bure. Kitonga, Hoteli ya Confort inahudumia bure, stendi ya Ipogoro malipo ni kati ya Sh 100 na 200, Mafinga abiria watalazimika kulipia kiasi kama hicho na Makambako malipo yatakuwa kati ya Sh 200 na 300.

  Dar es Salaam - Mwanza

  Magari yanapitia mikoa ya Pwani, Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora na Shinyanga, ‘dawa itachimbwa' Msamvu, Gairo kuna hoteli ambayo inahudumia bure, Badueli umbali wa kilometa tatu kutoka Dodoma mjini pia huduma ni ya bure. Singida mjini iliko stendi ya mabasi huduma hiyo pia itapatikana kwa malipo ya Sh 200, kituo cha mabasi Nzega mjini huduma italipiwa Sh 200 na katika stendi kuu mjini Tabora malipo ni Sh 200 pia.

  Katika stendi kuu ya mabasi Shinyanga mjini, huduma hiyo italipiwa Sh 200 na kwa waendao Kagera kupitia Kahama huduma itapatikana stendi kuu ya mabasi kwa kati ya Sh 200 na 300 huku Mwanza mjini katika stendi kuu ya mabasi pia huduma italipiwa Sh 200. Kwa waendao Kagera baada ya kutoka Kahama, huduma zitapatikana Ushirombo kwa Sh 100 na Sh 500 ambapo pia watapata fursa ya kuoga, Chato Sh 200, Muleba Sh 200 na Bukoba Sh 200. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kwa abiria watokao Kigoma kabla ya kufika Kahama watahudumiwa Kasulu kwa Sh 200, Kibondo kwa Sh 200 na Runzewe kwa Sh 200 pia.

  Dar es Salaam - Tanga

  Abiria watahudumiwa katika kituo cha mizani Msata bila gharama yoyote sawa na Segera.

  Dar es Salaam - Moshi, Arusha na Manyara

  Huduma zitapatikana Korogwe katika hoteli mbili bila malipo na Mombo ambako pia kuna hoteli isiyotoza malipo. Lakini Same, Mwanga, Himo, Moshi Mjini na Boma Ng'ombe, huduma itatolewa kwa Sh 200 na Arusha huduma itapatikana stendi kuu kwa Sh 200 sawa na ilivyo kwa Manyara.

  Dar es Salaam-Lindi-Mtwara

  Eneo la Nangurukuru kuna hoteli iitwayo StarCom ambayo itatoa huduma bila malipo, ambapo Lindi huduma hiyo haitalipiwa huku Mtwara ikilipiwa Sh 200 ingawa haitoshelezi mahitaji.

  Source: Pambana na Climate Change

   
 2. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  Miradi Bubu ya Wazalendo
   
 3. KATATANAMA

  KATATANAMA Member

  #3
  Sep 1, 2012
  Joined: Feb 15, 2012
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ujinga mtupu. Miundo mbinu ya mjini imewashinda sembuse ya porini.
   
 4. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,142
  Likes Received: 869
  Trophy Points: 280
  inawezekana kuna jamaa amepeleka wazo na ahadi kem kem za kuwashawishi wamiliki wa hz hotel juu ya kutoa 10% na deal ikaingia line!. Chezea bongo wewe?
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Sep 1, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Mtu akishikwa na haja ya ghafla porini itakuwaje?
   
Loading...