Majina ya vinywaji vyetu vya asili

vukani

JF-Expert Member
Dec 30, 2009
245
165
Majina ya pombe zetu za asili:

Dengelua – Hii inapatikana kule upareni
Mbege – Hii ina[patikana kule Moshi uchagani
Ulanzi – Kule Iringa
Ulaka – Nasikia inapatikana Morogoro
Boha – sina uhakiaka inapatikana wapi
Kindi – Hii nayo naomba msaada sijui asili yake ni wapi
Wanzuki – Hii ni new technology nasikia ina gesi kushinda hata Bia
Chimpumu – Hii nayo nasikia inapatikana mikoa ya kusini
Tende – Hii inapatikana wisiwa vya karafuuZanziberi
Gongo – Hii ina majina mengi ajabu, Kachaso, machozi ya Simba, Uzo, Chang’aa, na haijulikani asili yake ni wapi

Nyingine mtajazia……………………..
 
Dengelua – Hii inapatikana kule upareni (ni ya miwa)
Mbege – Hii inapatikana kule Moshi uchagani (ni ndizi+ulezi)
Ulanzi – Kule Iringa (ni ya utomvu wa mianzi)
Wanzuki – Hii ni new technology nasikia ina gesi kushinda hata Bia (maana ya wanzuki ni wa nyuki, kwa asili intumika asali lakini siku hizi inatumika sukari)
Gongo – nadhani teknolojia yake ililetwa wakati wa vita, kumbuka bila pombe hakuna vita (inatengezezwa kwa vitu vyenye sukari nyingi kama sukari, molasesi, mapapai n.k. Hii ni pombe ya mvuke (spirit) tofauti na pombe nyingine za kienyeji)

nyongeza
Mnazi - ni ya watu wa pwani, maarufu kwa harufu yake kali (utomvu wa mnazi)
Busa??
Komoni??
Pingu??
 
Kuna jamaa yangu kanitumia sms akinikumbusha kuwa nimesahau pombee maarufu kama Shamukwale, hii naomba msaada ni pombe gani na inapatikana wapi?
 
Majina ya pombe zetu za asili:

Dengelua – Hii inapatikana kule upareni
Mbege – Hii ina[patikana kule Moshi uchagani
Ulanzi – Kule Iringa
Ulaka – Nasikia inapatikana Morogoro
Boha – sina uhakiaka inapatikana wapi
Kindi – Hii nayo naomba msaada sijui asili yake ni wapi
Wanzuki – Hii ni new technology nasikia ina gesi kushinda hata Bia
Chimpumu – Hii nayo nasikia inapatikana mikoa ya kusini
Tende – Hii inapatikana wisiwa vya karafuuZanziberi
Gongo – Hii ina majina mengi ajabu, Kachaso, machozi ya Simba, Uzo, Chang'aa, na haijulikani asili yake ni wapi

Nyingine mtajazia……………………..

Boha inapatikana kwa kina mgosi 'washambaa'......unakamua miwa then ile juice ndio inatumika kutengeneza ulabu...! Cheki hiyo picha sometime ago nilikuta jamaa wakifanya mambo!
Boha preparation copy.jpg
 
Attachments

  • Boha preparation copy.zip
    471.8 KB · Views: 58
Oyaaa, kuna Matutapu huku Sikonge.

Pia usisahau kwa Pwani kuna Mazishi saa nane.

Kwa watoto kuna Togwa au Matogwa.

ROYA ROY: Uji wa Masasu (maji yanayobaki baada ya kuloweka Mahindi) hivi tunauitaje?
 
ulaka mkuu ni pombe ya mabibo ya korosho na haipatikani morogoro inapatikana mtwara lindi, tunduru, mtwara
 
Comoni inapatikana iringa inatokana na vimelea vya mahindi
kangala-Iringa inatokana na pumba za mahindi
Msabe- Iringa,inatokana na mtama
Sweera-Iringa inatokana na vimelea vya mahindi pamoja na asali
 
Dengelua – Hii inapatikana kule upareni (ni ya miwa)
Mbege – Hii inapatikana kule Moshi uchagani (ni ndizi+ulezi)
Ulanzi – Kule Iringa (ni ya utomvu wa mianzi)
Wanzuki – Hii ni new technology nasikia ina gesi kushinda hata Bia (maana ya wanzuki ni wa nyuki, kwa asili intumika asali lakini siku hizi inatumika sukari)
Gongo – nadhani teknolojia yake ililetwa wakati wa vita, kumbuka bila pombe hakuna vita (inatengezezwa kwa vitu vyenye sukari nyingi kama sukari, molasesi, mapapai n.k. Hii ni pombe ya mvuke (spirit) tofauti na pombe nyingine za kienyeji)

nyongeza
Mnazi - ni ya watu wa pwani, maarufu kwa harufu yake kali (utomvu wa mnazi)
Busa??
Komoni??
Pingu??

Red: Wanzuki, hii kitu nzuri sana but kwasababu ya haya makampuni ya bia kutaka kuiua kimarket ndo mana cku hizi haisikiki

Nyongeza
Rubisi: ni ya watu wa kagera, maarufu kwa utengenezaji wake kwa kutumia nyenzo za miguu kuchanganya ndizi na mtama
 
Comoni inapatikana iringa inatokana na vimelea vya mahindi
kangala-Iringa inatokana na pumba za mahindi
Msabe- Iringa,inatokana na mtama
Sweera-Iringa inatokana na vimelea vya mahindi pamoja na asali
Zote hizi zinapatikana sehemu moja?
Kuna watu wanatakiwa kuja kutoa maelezo hapa.
 
Majina ya pombe zetu za asili:

Dengelua – Hii inapatikana kule upareni
Mbege – Hii ina[patikana kule Moshi uchagani
Ulanzi – Kule Iringa
Ulaka – Nasikia inapatikana Morogoro
Boha – sina uhakiaka inapatikana wapi
Kindi – Hii nayo naomba msaada sijui asili yake ni wapi
Wanzuki – Hii ni new technology nasikia ina gesi kushinda hata Bia
Chimpumu – Hii nayo nasikia inapatikana mikoa ya kusini
Tende – Hii inapatikana wisiwa vya karafuuZanziberi
Gongo – Hii ina majina mengi ajabu, Kachaso, machozi ya Simba, Uzo, Chang’aa, na haijulikani asili yake ni wapi

Nyingine mtajazia……………………..
Gongo asili yake ni Germany ilifika hapa kwa mara ya kwanza WW1 baada ya waheshimiwa kukosa whisky ndipo wakaamua kuitengeneza.
NI KITU KIZURI SANA MIMI HUWA NAITUMIA.
PROBLEM HAPA NI ALCOHOLIC VOLUME INA FLACTUATE ...
NINGESHAURI SERIKALI IRUHUSU HII KITU THEN SIDO WAWE WANANUNUA NA KUCHUJA NA KU PACK NA KU CONTROL ALCOHOLIC VOLUME (IWE STANDARD) ....ITAWAPATIA AJIRA WA TZ WENGI....
HII UGANDA WANAITA WARAGI NA MALAWI NI POWER NAMBA 1....HAPA BONGO NI FITNA TUUU ETI HARAM.....
 
Dengelua – Hii inapatikana kule upareni (ni ya miwa)
Mbege – Hii inapatikana kule Moshi uchagani (ni ndizi+ulezi)
Ulanzi – Kule Iringa (ni ya utomvu wa mianzi)
Wanzuki – Hii ni new technology nasikia ina gesi kushinda hata Bia (maana ya wanzuki ni wa nyuki, kwa asili intumika asali lakini siku hizi inatumika sukari)
Gongo – nadhani teknolojia yake ililetwa wakati wa vita, kumbuka bila pombe hakuna vita (inatengezezwa kwa vitu vyenye sukari nyingi kama sukari, molasesi, mapapai n.k. Hii ni pombe ya mvuke (spirit) tofauti na pombe nyingine za kienyeji)

nyongeza
Mnazi - ni ya watu wa pwani, maarufu kwa harufu yake kali (utomvu wa mnazi)
Busa??
Komoni??
Pingu??

Matutapu huku Sikonge.
Pwani kuna Mazishi saa nane.
Togwa au Matogwa.
ROYA ROY: Uji wa Masasu (maji yanayobaki baada ya kuloweka Mahindi) hivi tunauitaje?
Comoni inapatikana iringa inatokana na vimelea vya mahindi
kangala-Iringa inatokana na pumba za mahindi
Msabe- Iringa,inatokana na mtama
Sweera-Iringa inatokana na vimelea vya mahindi pamoja na asali

Chibuku = Ubungo Mathiwa hapo!.
Kindi= Iringa/ Nyanda za Juu Kusini (mapumba ya mahindi+mbolea ya UREA+Chloroquine).
 
Wakuu kule kwetu mpitimbi songea kuna kilaji babu kubwa kinaitwa myakaya, inatengenezwa kwa mihogo haha, kuna msabe hii inapatikana iringa vijijini, pyua au gongo bin chang'aa inatokana na sehemu na sehemu, wakati naishi maeneo ya shamsi pale arusha kuna washkaji zangu wa matejoo waliniambia pyua ya pale inamchanganyiko wa hatari, kuna molases humo, mapapai, vidonge vya klorokwini yaani noma tupu
 
Kuna myakaya wa NAMATUHI bana.....mbele ya mpitimbi kama unakwenda Muhukulu, kile kijiji cha mzee Msongela we acha tuuuuu
 
We ngalikihinja mwana wa yani? ummanyile na msongela? ah pale namatuhi ndo pa bomani bwana, ummanyile na mbema?
 
Chang'aa - asili yake ni Kenya! Ni pombe inayotengenezwa baada ya kuzimua 'kinyesi' cha binadamu!

Bhusara - ni kinywaji laini ila ikichacha inakuwa pombe na watengenezaji ni wakurya, wajita (kanda ya ziwa)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom