Majina ya Mikoa, Wilaya, sehemu ndani ya Tanzania pia na maana yake

Mto_Ngono

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
686
589
Tanzania ipo mikoa, wilaya na sehemu tofauti tofauti na majina yake. Lakini huwa najiuliza haya majina yametokana na nini au ni kwa sababu gani waliita hivyo?

Kwa mfano Msasani nasikia ilitokana na mmakonde flani kushindwa kutamka Musa Hassan na kwa sababu walikuwa wanakaa wamakonde wengi basi wakaamua kupaita Musa-sani ile ' Ha' walishindwa kutamka na huyu mtu alikuwa maarufu. Hapo ndo msasani ikaanza kutumika.

Kilimanjaro-hii ninkutokana na mlima ulipo. Nafahamu Kilima ni Mlima, Sasa Njaro sijui yatokea wapi...

Je wewe wajua jina gani na historia yake!!! Twende pamoja sasa tueleweshane tuwe na kumbukumbu sahihi...
 
1. Kibororoni nasikia ilitokana na wenyeji wa eneo hilo kushindwa kutamka kibao cha alama barabarani kilichoandikwa Kibo Road. Kwahiyo wao wakawa wanatamka Kibororoni!

2. Chekeleni huko Moshi. Hii ilitokana na wenyeji wa eneo hilo kushindwa kutamka vema kibao cha angalizo la njia ya Treini cha Check Train. Kwahiyo wao wakawa wanatamka Chekeleni!
 
Koromije, Mzungu alikua akiishi hapo Anaitwa Jonathan ,alikua nakisima cha maji sasa wasukuma wanamuamsha kila siku kuchota maji na wanalikosea jina lake, akawaambia "just call me J" wasukuma wanasema "Mzungu Kasema kwamba colu mi jei" hivyo wakamuita columijei ndo ikawa Koromije
 
1. Kibororoni nasikia ilitokana na wenyeji wa eneo hilo kushindwa kutamka kibao cha alama barabarani kilichoandikwa Kibo Road. Kwahiyo wao wakawa wanatamka Kibororoni!

2. Chekeleni huko Moshi. Hii ilitokana na wenyeji wa eneo hilo kushindwa kutamka vema kibao cha angalizo la njia ya Treini cha Check Train. Kwahiyo wao wakawa wanatamka Chekeleni!
Sio kibo road ni sehemu ambapo unaweza ona kilelele kimoja cha kibo so pakaitw kibo alone wenyejk wakashindwa tamka ndio wakapiga pask ndefu na kuwa kibororoni.
 
Tanganyika ilitokana na memo Tanga ki-Bondei ni shamba. Wajerumani wakiwa na wapagazi wao walikuta watoto wanacheza wakawauliza wazazi wenu wako wapi walijibu 'waita tanga' ikimaanisha 'wamekwenda shamba' WalipofikaTanga waluwakuta wazazi wanalima ndiyo ukawa mawazo wa neno Tanga. Walikuwa baada ya Tanga ni nyika wala unga likawa Tanganyika
 
KIBOROLONI ni baada ya wachaga kushindwa kusema KIBO ALONE. maana yake kilele cha kibo kilionekana chenyewe. mawenzi haikuonekana

TARAKEA ipo rombo. Wazungu waliwaambia wachaga TAKE CARE kwa sababu waliona wako karibu na mlima volcano wasije lipukiwa.

KILIMANJARO ni mzungu alishindwa kuelewa maana ya maneno haya KILIMA-KYARO ikimaanianisha mlima wa Mungu akasikia ni kama wamesema kilimanjaro
 
Back
Top Bottom