Kwanini maeneo haya yalipewa majina ya hivi?

Namuona Kyachakiche naomba atupe maana ya maeneo haya uko Arusha
Ngulelo
Kimandolu
Arusha Mjini
Philips
Ngarenaro
Mbauda
Ngaramtoni
Tengeru
USA River
King'ori
Kikatiti
Sokoni II
Arumeru
Loita
Bangata
Midawe
Ulong'a
Njiro
Sakina
Sing'isi
Matejoo
Unga Limited
Sinoni
na mengineyo

mengineyo
Illboru
Kijenge ya juu
Kijenge mwanama
Njiro nane nane,njiro contena (container)
Massai camp
Sekei
 
Sinza kwa remy- maeneo hayo alikuwa anaishi Dr remy mwimbaji wa nyimbo za dance.
Ubungo maziwa-maeneo hayo kulikuwa na kiwanda cha maziwa.
Mabibo-maeneo hayo kulikuwa na mikorosho mingi sana na ilikuwa inatoa mabibo(matunda ya mikorosho) matamu sana tulikuwa tunaenda kula miaka ya 80.
Philips-Hapa kulikuwa na kiwanda cha radio za philips Arusha.
Sakina-hapa alikuwepo mama mmoja anaitwa sakina alikuwa anapika chakula so watu walikuwa wanasema wanaenda kwa sakina.
Singisi-hapa ni maeneo ya jamii ya wasingisi ni jamii ndani ya jamii ya wameru wa arusha.ni wakorofi hao
Unga ltd-hii ilitokana na kiwanda cha unga na ni maeneo ya NMC.national milling cooperation.- Arusha.
njiro nanenane-kuna uwanja wa maonyesho ya sikukuu ya nanenane.Njiro. kontena hapa ni eneo lililopo njiro jamaa waliweka kontena la kuuza vifaa vya ujenzi hapo watu wakaanza kusema nishushe kontena.

masai camp-hili ni jina la biashara jamaa alinunua eneo akatengeneza campsite kwa ajili ya watalii na club ndani basi eneo likabatizwa jina masai camp.
NB.Abiria ktk vyombo vya usafiri ndio chazo kikubwa cha majina ya maeneo.ikisaidiwa na matukio flani yasiyo sahaulika.mlima.mito na feature nyingine.
 
Vipi
1. Kiwalani
2. Bom Bom
3. Vingunguti
4. Kiembembuzi
5. Kigilagila
6. Chang'ombe
7. Yombo
8. Changanyikeni
9. Tandika
10. Dovya
11. Buza
12.Vijibweni
13.Tumbi

Kiwalani linatokana na neno la kizaramo kiwala-eneo lenye msitu wa wastani na lillilo kavu-halina rutuba nyingi. Kipindi hicho mashamba yenye rutuba nyingi yalikuwa Buguruni na Tabata kwa waliokosa maeneo hayo waliambiwa waende huko mbali msituni (kiwalani).

Kuhusu Tandika, ukiacha Temeke wailesi (Wire Less) kutokana na mitambo ya simu ya upepo pale ili Miburani Sekondari kwa sasa maeneo yote yaliyobaki yalikuwa na mapori yaliokuwa na miti ya mikorosho(Temeke Mikoroshini), miembe na mikole/mkole (miti ambayo ngoma za asili za wazaramo zinafanyika). Hivyo kulikuwa na eneo maarufu lililokuwa na huo mkole kwa ajili ya kufundia wali wa kizaramo. Kabla ya kuelekea huko, ni lazima papwe pametandikwa vizuri. Ndivyo jina Tandika lilivyoanza.
 
Tabata Matumbi; Kanisa la KKKT limekataa kutumia jina hilo, wana msuguano na doyasisi. Eti lina maana za mizimu. na mapepo Matumbi ni Manyani makubwa na inawezekana kuna imani za kichawi haliashirii UPAKO, mema, maendeleo au bahati. Jina la Tabata Ubaya Ubaya bnalo noma!
 
Tabata Matumbi; Kanisa la KKKT limekataa kutumia jina hilo, wana msuguano na doyasisi. Eti lina maana za mizimu. na mapepo Matumbi ni Manyani makubwa na inawezekana kuna imani za kichawi haliashirii mema, maendeleo au bahati. Jina la Tabata Ubaya Ubaya bnalo noma!

hata njombe kuna sehemu inaitwa NYUMBA NITU- MEANS NYUMBA YA GIZA pana msitu wa mapepo, kanisa la kkkt walikataa kutumia hilo jina wanatumia jina la Mtaa wa Amani,usharika wa Amani
 
Vipi
1. Kiwalani
2. Bom Bom
3. Vingunguti
4. Kiembembuzi
5. Kigilagila
6. Chang'ombe
7. Yombo
8. Changanyikeni
9. Tandika
10. Dovya
11. Buza
12.Vijibweni
13.Tumbi

Zamani huku vingunguti kulikuwa na soko kubwa sana la mbuzi ambalo bado linaendelea mpaka sasa, mbuzi hao walikuwa wanapumzishwa chini ya miti ya miembe mikubwa ambayo ilikuwa kandokando ya barabara.

kutoka wakati huo mpaka Leo kumeendelea kuitwa Vingunguti kiembembuzi sababu ikiwa ni hiyo miembe japo siku hizi haipo baada ya ujenzi wa barabara, na hilo soko la mbuzi.
 
banana
kulikuwa na baa moja ya mchaga mmoja alikuwa kapteni wa ndege za jeshi pale airwing alikwenda moshi akapakia mgomba akaja kupanda pale banana sasa hivi kuna petrostasheni ya gapco kwa sasa

Si sahihi hii stori. Ukweli ni kwamba kulikua na baa ikiitwa banana mwenyewe akiitwa kimati, marehemu sasa. Hakuwahi kuwa mwanajeshi wala rubani, ila baa yake ilipendwa na wanajeshi. Baadae aliivunja na kujenga kituo cha mafuta kinachoitwa banana service station. Jina rasmi la eneo lile japo si maarufu sana ni minazi mirefu
 
mengineyo
Illboru
Kijenge ya juu
Kijenge mwanama
Njiro nane nane,njiro contena (container)
Massai camp
Sekei

Pale Mtwara: Mtwara, mikindani, chikongola,Ligula(A,B,C) magomeni(A,B,C),Tandika, Kisutu, Shangani(east, west),mangoela, lilungu,naliendele, mangamba, rahaleo,Chipuputa, Kilimahewa, mji mwema, ufukoni, chikongola, railway, chuno, mbezi n.k. Na kwa nini majina ya mitaa au vitongoji unakuta kuna majengo moshi, majengo mtwara, shangani zanzibar, shangani mtwara, magomeni, kisutu na tandika ni dar na mtwara hivyo hivyo, hii inasababishwa na nini?
 
Nawaunga mkono asilimia 100, majina mengine yanaambatana na mabalaa bana
Tabata Matumbi; Kanisa la KKKT limekataa kutumia jina hilo, wana msuguano na doyasisi. Eti lina maana za mizimu. na mapepo Matumbi ni Manyani makubwa na inawezekana kuna imani za kichawi haliashirii UPAKO, mema, maendeleo au bahati. Jina la Tabata Ubaya Ubaya bnalo noma!
 
Back
Top Bottom