Uchaguzi 2020 Majimbo zaidi ya 11 ya mikoa ya Lindi na Mtwara hatarini kupotea

Kinambeu

JF-Expert Member
Nov 2, 2014
906
454
Taarifa zilizo rasmi za kiutafiti katika mikoa ya LINDI na Mtwara yapo majimbo takriban 11 ambayo yapo hatarini kupotea. Majimbo hayo ni kama ifuatavyo,

1. Kilwa Kaskazini
2. Kilwa Kusini
3.Nachingwea
4. Lindi Mjini
5. Liawale

Kwa upande wa Mkoa wa Mtwara ni,
1. Mtwara Mjini
2. Tandahimba
3. Newala Mjini
4. Masasi Mjini
5. Newala Vijijini

Lakini mengine bado utafiti wake unaendelea ambayo yatatolewa report zake kamili ndani ya siku 3. Majimbo ambayo utafiti unaendelea ni Mtwara Vijijini, Nanyamba, Nanyumbu, Mchinga na Ndanda.

Chanzo kikuu cha mambo kwenda mrama ni kusimamisha wagombea wasiokubalika, waliochoka na wasio na mvuto. Chama cha Mapinduzi turufu iliyobakia ni kuja kwa Mukulu lakini baada ya kusema hatokuja mikoa ya Kusini Hali ndio imekuwa Ngumu na wapinzani wakishangilia.

Kwa mfano jimbo la Kilwa Kusini Mgombea aliyeongozwa alikatwa na kuteuliwa wa nne aliyepata kura 12 tu, Liwale pia hivyo hivyo, Kilwa Kaskazini nako ni hivyo hivyo. Mtwara Mjini nako mgombea aliyeshinda alikatwa, Tandahimba nako alikatwa, Newala Vijijini pia alikatwa.

Bwege wa Kilwa Kusini tayari mguu mmoja upo bungeni maana kazi kwake ni rahisi mnoo.

Naomba kuwasilisha.
 
Tunaomba Rais atumie hata chopa kunusuru hayo majimbo. Maana sauti ya baba ina faraja kubwa kuliko sauti nyingine.

Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, tafadhali tumia busara zako, kwenye siku 10, zilizobaki tumia siku 3 (tatu) kwenda kwenye mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma ili angalau wakuone kuwa una wathamini kuliko kutokwenda kabisa.
 
Tunaomba Rais atumie hata chopa kunusuru hayo majimbo. Maana sauti ya baba ina faraja kubwa kuliko sauti nyingine. Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, tafadhali tumia busara zako, kwenye siku 10, zilizobaki tumia siku 3 (tatu) kwenda kwenye mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma ili angalau wakuone kuwa una wathamini kuliko kutokwenda kabisa.
Kwi kwi kwiiiii. Huyu dikteta uchwara aliyenyang'anya korosho kwa kutumia jeshi akija ndo ataharibu kabisaa!!
 
Tunaomba Rais atumie hata chopa kunusuru hayo majimbo. Maana sauti ya baba ina faraja kubwa kuliko sauti nyingine. Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, tafadhali tumia busara zako, kwenye siku 10, zilizobaki tumia siku 3 (tatu) kwenda kwenye mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma ili angalau wakuone kuwa una wathamini kuliko kutokwenda kabisa.
Ohoooo!!! unazikumbuka korosho ?
 
Huko si aliondokaga ghafla tena akaenda kusiko julikana?
 
Back
Top Bottom