Majimbo yenye wabunge wa chadema

Mfamaji

JF-Expert Member
Nov 6, 2007
6,631
1,926
Wakuu, katika chunguza chunguza yangu nimegundua kuwa majimbo yanayoongozwa na Wabunge wa Chadema yako juu kimaendeleo hasa huduma za jamii. Mfano mzuri ni Moshi mjini na Kigoma .

Ukifika MS mjini utatamani uendelee kuwepo maana kwanza kwa usafi , pili maji kibao, etc
Kule kwa Kabwe hata usiseme . Mambo mengi yametokea kwa miaka mitano tu .

I know it is true and only truth. CHAGUA CHADEMA .
 
Hii haihitaji fedha za kigeni kuona na kuelewa, iko live mno!
Nijuavyo mimi ni kwamba jimbo la upinzani lazima lifanye vizuri kwenye nyanja za huduma ili kukiprove wrong chama tawala!
Long live CHADEMA!
 
Hivi nini siri ya mafanio ya majimbo hayo ya CHADEMA?

fedha zote za miradi zinazoletwa halmashauri zinatumiwa ipasavyo kuleta tija na zaidi ufanisi unaongezeka kwa watumishi ngazi ya halamshauri kuogopa mbunge anaweza kuwalipua wakiboronga mambo.
 
wakuu, katika chunguza chunguza yangu nimegundua kuwa majimbo yanayoongozwa na wabunge wa chadema yako juu kimaendeleo hasa huduma za jamii. Mfano mzuri ni moshi mjini na kigoma .

Ukifika ms mjini utatamani uendelee kuwepo maana kwanza kwa usafi , pili maji kibao, etc
kule kwa kabwe hata usiseme . Mambo mengi yametokea kwa miaka mitano tu .

I know it is true and only truth. Chagua chadema .

uongo mwingine huo!!! Mji wa moshi ni msafi si kwa sababu ndesamburo ni mbunge! Bali manispaa ya moshi ina madiwani zaidi ya asilimia 95 toka ccm na kazi ya usafi inasimamiwa na manispaa sio chadema hivi kweli munazungumzia ushabiki au hali halisi?

Askari wa manispaa ya moshi wakikukamata unatema mate au unatupa taka barabarani faini yake ni sh.50000! Sasa hawa askari wa manispaa ya moshi wanalipwa mshahara na chadema?
Miaka yote ya uongozi wa ndesamburo hakuna alichotufanyia wakazi wa moshi zaidi ya kununua ambulance ya kubeba wagonjwa hewa! Viwanda vyote vilivyokuwepo enzi za uongozi wa marehemu mama lucy lameck na mzee muhidini mfaume kimario wabunge wa ccm wa zamani vimeuwawa ktk uongozi wa chadema! Wananchi wa moshi wamekuwa masikini zaidi kuliko enzi za utawala wa ccm!

Chadema hawajatuletea maendeleo yoyote hivyo musidanganye umma na mwaka huu moshi mjini inarudi ccm kwani chadema wameishindwa moshi na huyu mzee ndesamburo kwa kweli amechoka hana jipya wala hana ubunifu wa kuleta maendeleo! Akapumzike kama mwenzake malecela!
 
hivi nini siri ya mafanio ya majimbo hayo ya chadema?

ni kuacha porojo na ulafi na kufanya kazi kwa bidii.
Kiongozi safi ni yule anayejali awaongozao! Huishi nao hujua matatizo yao na kuyatafutia ufumbuzi.
Viongozi wetu wengi hufanya kazi kwa mazoea na bila malengo na hukosa uzalendo ndiyo maana maendeleo hakuna.
 
Ukweli ukitaka maendeleo katika eneo unaloishi, chagua chama cha upinzani. Hata ikitokea eneo hilo likarudi ccm, nguvu kubwa na ya maksudi huwa inaelekezwa sana hapo. Mfano; Moshi (v), Rombo, Hai nk walijaribu upinzani, sasa lami, umeme, maji mpaka vijijini. Mkiendelea kusema KIDUMU..KIDUMU..., mtaendelea kudumu kwenye lindi la ufukara.
 
Ama kweli kazi ya kuelimisha wadanganyika ni nzito mno. At least umeona kitu kwamba Ndesamburo kanunua ambulance. Tukisema wabunge wa CCM pengine uwezo wao wa kutambua matatizo ya wananchi wao ni mdogo sana. Tuanze na JK, kapeleka ambulance ngapi bagamoyo ( kukuonyesha wasivyoijua hata jiografia ya nchi yao, JK kaahidi bajaji 400 ambulance!!!!!!!!!??????). Wataje uwajuao walioleta japo pikipiki za kusaidia wagonjwa majimboni mwao.
Sera ya ubinafsishaji ndugu yetu ilianzishwa na serikali ya CCM, viwanda vyenu Moshi viliuzwa kutokana na sera hiyo. Mbunge hahusiki na ubinafsishaji wa viwanda.
Isitoshe mbunge ni mjumbe katika vikao vya halmashauri, hivyo maamuzi yote halali ya baraza la madiwani mbunge anahusika. Hivyo usafi wa mji una mchango wa mbunge ndugu.
Na ili kukutoa tongotongo usoni, kumbuka kwa asilimia 90 ya majimbo yaliyoongozwa na chadema mafanikio yameonekana dhahiri, angalia vipindi vya tv na vyombo mbalimbali utajionea. Na kama uko mbali navyo just peruuuzi ktk tovuta mbalimbali. See for yourself; Karatu (ni karibu na Moshi tembeleaujionee), fananisha na Babati ambayo imepewa hadhi ya mji kutokana na kuwa makao makuu ya mkoa. Nenda Tarime (waulize wanalipia kiasi gani elimu?). Nenda Kigoma (Uliza matatizo yao ya umeme yametatuliwa ama bado!! Tatizo la barabara ya lami kuwaunganisha na mikoa mingine je?), nenda mpanda jimbo la Arfi waulize wanaongelea nini kuhusu uamuzi wao wa kuichagua chadema? Majimbo manne tu kwa miaka mitano great changes. CCM majimbo 200 ndani ya miaka 50 loooo aibu. Pengine huelewi ndugu, Jaribu kutembelea Tunduru, Tandahimba, Kiteto na kwingineko, utalia. A lot of opportunities, great poverty rate. Mji una mabomba matatu ya maji ya jumuia. Pitia riport za wakaguzi, ubadhirifu wa hali ya kutisha. Hakuna na kuwajibishwa. Hospitali hazina dawa huoni ni tatizo. Je, na hili la kupambana na mbu Muhimbili tunahitaji wafadhili???? Yawezekana unafaidika na ufedhuli huo, lakini think about your brothers and sisters who are dying from cureble diseases bse of luck of medicine, while somebody is bosted thyself "vijisenti" and nobody asking on how he got hivyo vijisenti. People die of diarrhoea because of drinking dirty water.
I call upon you and most of the sleeping partners of yours ma friend, our country is in riddiculous situation, let us dont drive it into dipsomaniac. For the sake of our country and your lovely part CCM, VOTE FOR DR. SLAA. Your VOTE is the liberation of youself, your family, your relatives, your party and the entire community of the peoples of the United Republic of Tanzania.
 
uongo mwingine huo!!! Mji wa moshi ni msafi si kwa sababu ndesamburo ni mbunge! Bali manispaa ya moshi ina madiwani zaidi ya asilimia 95 toka ccm na kazi ya usafi inasimamiwa na manispaa sio chadema hivi kweli munazungumzia ushabiki au hali halisi?

Askari wa manispaa ya moshi wakikukamata unatema mate au unatupa taka barabarani faini yake ni sh.50000! Sasa hawa askari wa manispaa ya moshi wanalipwa mshahara na chadema?
Miaka yote ya uongozi wa ndesamburo hakuna alichotufanyia wakazi wa moshi zaidi ya kununua ambulance ya kubeba wagonjwa hewa! Viwanda vyote vilivyokuwepo enzi za uongozi wa marehemu mama lucy lameck na mzee muhidini mfaume kimario wabunge wa ccm wa zamani vimeuwawa ktk uongozi wa chadema! Wananchi wa moshi wamekuwa masikini zaidi kuliko enzi za utawala wa ccm!

Chadema hawajatuletea maendeleo yoyote hivyo musidanganye umma na mwaka huu moshi mjini inarudi ccm kwani chadema wameishindwa moshi na huyu mzee ndesamburo kwa kweli amechoka hana jipya wala hana ubunifu wa kuleta maendeleo! Akapumzike kama mwenzake malecela!

Hiyo Avator yako inasema vyote. Uliza uambiwe mchango wa Ndesa katika kuendeleza Moshi kila nyanja. Nenda Karatu uone kinachozungumzwa hapa.Sio ukurupuke tuu kama umeamka usingizini.Kama unataka maendeleo achana na hao mafisadi broo. Twende zetu kwenye utawala halisi sio wa kibongo flavor na ujambazi.
 
ushabiki mwengine bana....
na kule Pemba jee!? 100% ni wabunge wa upinzani mbona hatujaona kitu?
Yaliopo yote (bara bara,,umeme...) ni kazi ya Karume...
nyinyi kazi yenu kulia lia tu
 
wakuu kuna mtu ana list ya majmbo CHADEMA waliyo simamisha wagombea tafadhali sana mwenye list hiyo anisaidie nataka fanya tarhmini wapi tuongeze nguvu ya ili kuhakikisha ushindi
 
Wakuu, katika chunguza chunguza yangu nimegundua kuwa majimbo yanayoongozwa na Wabunge wa Chadema yako juu kimaendeleo hasa huduma za jamii. Mfano mzuri ni Moshi mjini na Kigoma .

Ukifika MS mjini utatamani uendelee kuwepo maana kwanza kwa usafi , pili maji kibao, etc
Kule kwa Kabwe hata usiseme . Mambo mengi yametokea kwa miaka mitano tu .

I know it is true and only truth. CHAGUA CHADEMA .

hii analysis yako sidhani kama ni sahihi kwani usafi unategemea na wenyeji wa sehemu hiyo pia si mbunge tu ndugu yangu
miji iliyopewa tuzo ya usafi ni mingi hebu ifuatilie na utaona kuna factors nyingi tu.
 
soma hapa pia
JIJI LA MWANZA LAONGOZA KWA USAFI
PMORALG - Information Centre - News
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Celina Kombani (MB) amesema kuwa Wizara yake haitaivumilia halmashauri au Manispaa ambayo mji wake hauzingatii hali ya usafi.
Mheshimiwa Kombani ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya mikakati ya wizara yake mwaka huu katika kuhakikisha kuwa miji na majiji nchini inazingatia usafi wa mazingira.
Pamoja na kulipongeza jiji la Mwanza na Manispaa ya Moshi kwa kuwa vinara wa usafi nchini, Waziri Kombani pia alisifu jitihada za usafi zinazofanywa na baadhi ya manispaa nchini kama vile Arusha, Iringa, Morogoro, Kibaha na halmashauri ya mji wa Kongwa iliyopo Mkoani Dodoma kwa kuwa Mstari wa mbele katika usafi wa mazingira.
Licha ya mkakati wa kitaifa ambao ni endelevu wa kuhakikisha kuwa majiji, manispaa, na miji mikubwa na midogo nchini inakuwa safi, Waziri Kombani alisisitiza kuwa Wizara yake mwaka huu itaipa kipaumbele mashindano ya kila mwaka ya usafi baina ya halmashauri, miji, manispaa na majiji nchini ili kubaini miji ambayo iko nyuma katika suala zima la usafi wa Mazingira.
Alisema kuwa Wizara yake haitaivumilia halmashauri au manispaa ambayo mji wake ni mchafu ndani ama pembezoni mwa mji huo.
Hata hivyo Waziri Kombani alikemea tabia iliyojengeka miongoni mwa wakazi hasa wa mijini wa kutupa ovyo taka taka kwani mtindo huo unachangia mno kurudisha nyuma jitihada za manispaa na majiji za kuboresha usafi.
Alisema pamoja na jitihada zinazofanywa na manispaa na majiji nchini za kuboresha miundombinu, kama wananchi hawatahamasika na kuanza kujijengea utamaduni wa kuwa na mazingira safi jitihada hizo hazitasaidia.
Alitolea mfano wa eneo la Manzese katika jiji la Dar es salaam ambalo ndilo linaloongoza kwa uchafu nchini Mheshimiwa Kombani alisema kuwa pamoja na jitihada za Manispaa ya Kinondoni kujenga mifereji mizuri kwa ajili ya kupitishia maji taka lakini mifereji hiyo sasa imekuwa ikitumika kwa ajili ya kutupia takataka.
"Pale Manzese, pamoja na manispaa kujenga mifereji mizuri, lakini nenda sasa mifereji ile mizuri ndo imekuwa dampo, watu wanatupa chupa, majivu na takataka za kila aina kwenye mifereji hiyo," alisema
Wakati huo huo Waziri huyo wa Tamisemi ametoa ufafanuzi juu ya uamuzi wa Serikali wa kumhamisha aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala John Lubuva kwenda kwenye halmashauri ya Shinyanga.
Alisema kwa vile uchunguzi ulionyesha kuwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Ilala hakuhusika moja kwa moja katika uzembe uliosababisha bomoa bomoa ya Tabata Dampo, Serikali iliamua kumpa adhabu ya kuteremshwa ngazi ya mshahara wake.
"Na kwa vile tulimpa adhabu hiyo, pia ilibidi aende kwenye halmashauri ndogo ambayo inalingana na ngazi ya mshahara wake," alisema Waziri Kombani na kusisitiza kuwa adhabu hiyo ni kulingana na kanuni za utumishi namba 42 ya mwaka 2003
 
wakuu kuna mtu ana list ya majmbo chadema waliyo simamisha wagombea tafadhali sana mwenye list hiyo anisaidie nataka fanya tarhmini wapi tuongeze nguvu ya ili kuhakikisha ushindi

brother, listi yenu inazidi kupungua kwani huko kagera kuna mgombea wenu mmoja wa chadema kajitoa sasa sijui nini kapewa any way watu kama hawa ndio wanataka kupewa ridhaa ya kuongoza ni hatari sana kwani yaliyowakuta wa zambia mwaka 1991 bado hawajayasahau baada ya kumtupa kenneth kaunda na kumpa madaraka mlokole chiluba! Matokeo yake kila mtu anayajuwa! Mlokole aliifilisi nchi na sasa kesi yake bado inaendelea!

Chadema wacheni kuhadaa wananchi uwezo uwezo na nia ya kuongoza hamna labda sababu na hiyo haitoshi kama hamna uwezo na nia ya dhati!
 
Wewe umeoa na una watoto wanaosoma shule? Je una wazee wanaohitaji matibabu? Je kuna jirani zako au ndugu zako ambao wameshindwa kuwapeleka watoto shule kwa sababu ya gharama? Je wewe umeshiriki kwenye ufisadi uliondeshwa na CCM? Je kipato chako au ndugu zako ni shiling ngapi? Je umeajiriwa au ni mmchinga? Kama umeajiriwa ni kiasi gani cha kodi ya PAYE unalipa? Je unafahamu maana ya kuishi chini ya dola moja?

Kama kuna watu waliopo kwenye huu ukumbi ambao bado wanashabikia hawa mafisadi kama Kadogoo ni wa kuhurumiwa tu maana hawajui wawazalo au watendalo. Msamehewe bure, japo muda wa kubadilika kifikra bado upo hadi 31 Oct. 2010
 
uongo mwingine huo!!! Mji wa moshi ni msafi si kwa sababu ndesamburo ni mbunge! Bali manispaa ya moshi ina madiwani zaidi ya asilimia 95 toka ccm na kazi ya usafi inasimamiwa na manispaa sio chadema hivi kweli munazungumzia ushabiki au hali halisi?

Askari wa manispaa ya moshi wakikukamata unatema mate au unatupa taka barabarani faini yake ni sh.50000! Sasa hawa askari wa manispaa ya moshi wanalipwa mshahara na chadema?
Miaka yote ya uongozi wa ndesamburo hakuna alichotufanyia wakazi wa moshi zaidi ya kununua ambulance ya kubeba wagonjwa hewa! Viwanda vyote vilivyokuwepo enzi za uongozi wa marehemu mama lucy lameck na mzee muhidini mfaume kimario wabunge wa ccm wa zamani vimeuwawa ktk uongozi wa chadema! Wananchi wa moshi wamekuwa masikini zaidi kuliko enzi za utawala wa ccm!

Chadema hawajatuletea maendeleo yoyote hivyo musidanganye umma na mwaka huu moshi mjini inarudi ccm kwani chadema wameishindwa moshi na huyu mzee ndesamburo kwa kweli amechoka hana jipya wala hana ubunifu wa kuleta maendeleo! Akapumzike kama mwenzake malecela!

Upo sahihi usafi wa mji wa Moshi si sababu ya Ndesamburo, CCM inaongoza halmashauri ya Moshi lakini inapata changamoto nyingi sana kutoka kwa madiwani wa CHADEMA.
Tukiweka ushabiki pembeni CCM mwaka huu haiwezi kumng'oa Ndesamburo Moshi Mjini uzembe uliofanywa na NEC ya CCM kurudisha jina la Salakana mtu ambaye hana makazi hapa Moshi Mjini unawagharimu sana... Salakana hafahamiki kabisa hapa Moshi kwa hiyo hawezi kumsumbua Ndesamburo.... (katika moja ya mikutano yake Ndesamburo ametoa ofa atakae onesha nyumbani kwa Salakana ndani ya jimbo la Moshi Mjini atampa 2M)
Pili mama Nsilo Swai ndiye chanzo cha CCM kushindwa hapa Moshi amechochea sana Makundi si Moshi Mjini tuu nenda Vunjo, Hai, Mwanga nk

kwa kifupi: Moshi Mjin Ndesamburo atashinda tena kwa kishindo kikubwa (kata karibu zote atapata asilimia kubwa dhidi ya pandikizi Salakana)
 
mbona nasikia ruzuku wanakula viongozi wa chadema? inakuwaje wanafanikiwa kiasi hicho?...kwa hiyo tuhuma hizo ni unafiki wa ccm?...........chagua chadema watutumikie.....
 
Upo sahihi usafi wa mji wa Moshi si sababu ya Ndesamburo, CCM inaongoza halmashauri ya Moshi lakini inapata changamoto nyingi sana kutoka kwa madiwani wa CHADEMA.
Tukiweka ushabiki pembeni CCM mwaka huu haiwezi kumng'oa Ndesamburo Moshi Mjini uzembe uliofanywa na NEC ya CCM kurudisha jina la Salakana mtu ambaye hana makazi hapa Moshi Mjini unawagharimu sana... Salakana hafahamiki kabisa hapa Moshi kwa hiyo hawezi kumsumbua Ndesamburo.... (katika moja ya mikutano yake Ndesamburo ametoa ofa atakae onesha nyumbani kwa Salakana ndani ya jimbo la Moshi Mjini atampa 2M)
Pili mama Nsilo Swai ndiye chanzo cha CCM kushindwa hapa Moshi amechochea sana Makundi si Moshi Mjini tuu nenda Vunjo, Hai, Mwanga nk

kwa kifupi: Moshi Mjin Ndesamburo atashinda tena kwa kishindo kikubwa (kata karibu zote atapata asilimia kubwa dhidi ya pandikizi Salakana)

Mwaka huu tena CCM itapoteza majimbo mengi sana ya Mkoa wa Kilimanjaro.... kwa uhakika (anayebisha baada ya 31st Oct ataelewa)

Vunjo inakwenda kwa Agustino Mrema kule CCM ni ya tatu Meela hana ubavu wa kupambana na Agustino anayetoka nae Kilema na Mrema wa CHADEMA ana nguvu kidogo maeneo ya Mwika tuu.
Moshi Mjini Ni CHADEMA (mbunge Ndesamburo)
Hai ni CHADEMA (Mbunge ni Mbowe, Kimbita hana nguvu maeneo ya watu wengi hasa machame na kikubwa alipokuwa mbunge hana alichofanya)

Mwanga anachukua Maghembe wa CCM though anapata upinzani toka kwa Pandikizi la Mzee Msuya na Kisumo

Same zote ni CCM (ile ya Mashariki kitakachomwokoa Anna Kilango ni kile kiwanda cha Tangawizi)

Moshi Vijijini Na Rombo hapo ni 50% CHADEMA au CCM inategemea kivumbi hiki cha Dr Silaa kitampitia vipi Mramba na ndugu yangu Chami...
 
Back
Top Bottom