Elections 2010 Majimbo ya Dar kipimo cha nani kashinda Uraisi...Dr.Slaa vs. JK.

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Mkuu wa MKoa wa Dar-Es-Salaam wa enzi zile aitwaye Chipungahelo au "Mama Chips" aliwahi kusema kwa kutamba.........."where Dar goes the nation goes......"

Kwa majigambo hayo hayo ni dhahiri Chadema imeshinda majimbo matano ya Dar na CCM kuambulia mawili tu..........

Katika hali hii JK anawezaje kutangazwa kuwa Raisi kama siyo uchakachuaji ulipo huko mikoani ukisimamiwa na kuratibiwa kwa ukaribu na wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo ambao wameahidiwa vyeo serikalini au halmashauri zenye neema?

Dar haki imetendeka kwa vile wajanja ni wengi na wameweza kufuatilia kwa karibu na kukwamisha zoezi chafu la CCM la kuchakachua matokeo lakini mikoani ni baadhi ya maeneo ya mijini Chadema imeweza kufanikisha hilo zoezi..............
 
Walikuwa wanasema watu wengi wa Dar (mijini) huwa hawaendi kupiga kura matokeo haya yana prove wrong, Jiji kuu limekwenda Chadema kama lilivyokwenda jiji la Nairobi mwaka 2002 kwa upinzani kabla ya wapinzani kuchukua serikali 2007. Pamoja na matokeo yote haya mimi naona ushindi wa Jiji la Dar na majiji mengine ni mtaji mkubwa kwa wapinzani watakaoutumia 2015.
 
Nawapongeza sana Mods wa JF kwa kazi nzuri mnayofanya. Hii posti inafaa kuunganishwa na kuwa chini ya ile inayosema CCM imepoteza majimbo yote muhimu, Arusha, Mwanza, Ubongo n.k. Mantiki yake ni moja inaonyesha kuwa Dr. Slaa ndiye rais wa Tanzania na Watanzania.
 
Lililotangwazwa Mpaka sasa ni Ubungo tu Mkuu, hayo mengine manne ni yapi?
 
Mengine ni kwa Mdee na Mpendazoe na ndo maana wanachelewesha matokeo...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom