Majimbo 60 Tanzania hayana wawakilishi/wabunge?

Shadow

JF-Expert Member
May 19, 2008
2,897
671
Kulingana na mfumo tuliorithi wa "Chama Kushika Hatamu" na katiba URT-1977[Kama ilivyofanyiwa mabadiliko] inayojivuta kuendena na mbio za mabadiliko Tanzania na dunia yote , watanzania wengi wamejikuta wakipokonywa wawakilishi wao na mamlaka aliyopewa Rais na hiyo Katiba tajwa katika ibara ya 54 na 55.
Kutokana na mfumo huu wabunge hawa 60 ambao ni mawaziri na mananibu mawaziri wamejikuta wakiwa njia panda katika kutekeleza majukumu ya waajiri wao ambao ni wananchi na Rais aliyewapa uwaziri.
Kutokana na haya, kuna msemo unasema ‘huwezi kuwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja bila kujikuta ukielemea zaidi kwa mmoja na katika suala hili mara nyingi inaonyesha wapi mawaziri hawa uangukia.
Ninachotaka kusema ni kwamba pamoja na vita iliyopo katika kupigania utawala wa sheria na vita dhidi ya mafisadi yale yote maovu utaona ya kwamba aliwezi kufanikiwa katika mfumo uliyopo sasa ambapo muhmili mmoja wa dola umeshika atamu zaidi kuliko mihimili miwili iliyobaki.
Ili kuleta usawa na usimamizi wa matumizi na utendaji wa serikali, pendekezo langu ni kwamba katiba ifanyiwe mabadiliko yafuatayo:
Mosi: Kifungu cha kumfanya Rais kuchagua wabunge miongoni mwa wabunge kufutwe na kuwekwa kifungu kitakachomfanya Rais kumteua mtu yoyote (kama ni mbunge basi ajiuzuru ubunge kwanza) kushika wadhifa wa Uwaziri, Ukatibu Mkuu, Ukurugenzi na nafasi zote za juu na kisha baada ya hapo Bunge liweze kuwafanyia ‘vetting’ na kuwapitisha au kuwakataa. Hapa tutaweza kuwaondoa mawaziri bungeni na serkali kuwajibishwa ipasavyo.
Pili: Uhuru wa kupata habari na utendaji wa vyombo vya habari vya ‘umma’ lazima viwajibike kwa bunge[South Africa Model]
Tatu: Wizara zitajwe na kuwekwa kwenye katiba kulinda upendeleo na utengenezaji wizara zisizo na tija[U.S. model]
Nne, Tume Huru ya Uchaguzi[napendekeza hybrid ya South Africa Model ]

 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom