Majimbo 214 kuchota bilioni 15.9 kuchochea maendeleo ya wananchi jimboni mwaka wa fedha 2023/24

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,033
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imetenga jumla ya Shilingi Bilioni 15.99 kwa ajili ya mfuko wa jimbo kwa majimbo 214 ya Tanzania Bara katika Mwaka wa Fedha wa 2023/24.

Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi Bungeni, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Angellah Kairuki, amesema fedha hizo ni kwa ajili ya kuchochea maendeleo katika majimbo yaliyopo Tanzania Bara

Katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Ofisi ya Rais –TAMISEMI iliidhinishiwa Shilingi bilioni 11.00 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Majimbo ya Uchaguzi 214 ya Tanzania Bara ambapo hadi Februari, 2022 fedha zote zilizokuwa zimeiidhinishwa zilikuwa zimetolewa sawa na asilimia 100.

Katika Mwaka wa Fedha wa 2022/23 Ofisi ya Rais –TAMISEMI iliidhinishiwa Shilingi Bilioni 15.99 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Majimbo ya Uchaguzi 214 ya Tanzania Bara. Hadi Februari, 2023 fedha zote zilizoidhinishwa zimetolewa.

Katika miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya mfuko wa jimbo zimetolewa kwa wakati na kwa asilimia 100.
 
Halafu atakuja CAG aseme 15 billion hazionekani.

Na wataambiwa watupishe.
Lakini si umesoma hapo fedha zote kwa miaka miwil zimefikishwa majimboni, au ulitaka tu tujue unamfahamu CAG?
 
Back
Top Bottom