Elections 2010 Majimbo 21 yatakayochukuliwa na CHADEMA kabla ya oct 31

Fuatilia siasa za kule Kigoma kaskazini utagundua nafasi yake. Kuna mambo kadhaa yamemuharibia ikiwemo kuwa nje ya jimbo kwa muda mrefu, kuonyesha nia ya kugombea majimbo mengiine na nguvu ya wagombea wa vyama vingine vya upinzani.

Sina shaka na kiti cha Hai kwa Mbowe lakini tarime yule jamaa aliyehama kutoka Chadema atakuwa na athari mbaya.

Huyo Mtema akikaa na upinzani wa kwenye Keyboard (JF) ubunge atausikia redioni.

Unakumbuka Lyatonga alivyoshinda ubunge Temeke, ilikuwa hakuna kulala wala longo longo kwenye vyombo vya habari. Ni nyumba kwa nyumba, kijiwe kwa kijiwe kila siku. Ni kwa staili hiyo ndio unaweza kuishinda CCM.

Nautakia kila la heri upinzani lakini inabidi watu wafahamishwe uhalisia ulivyo huko majimboni na kama hilo wengine hampendi kulisikia, tuvumiliane.
Uchambuzi ambao sio wa kuvutia kamba kwako kama huu ndio unatakiwa hapa.Haya mambo ya watu kuongeza chumvi baada ya tarehe 31 oct watapiga ukunga hapa.Ukweli unauma lakini ni vizuri kuelewa ili watu waweze kuongeza bidii.

Kwa mfano jimbo la Arusha Mjini kulichukuwa kutoka kwa ccm sio raisi na mara nyingi limekuwa alitabiriki kiraisi hivyo, kueleza ukweli itasaidi kwa wale walioko Arusha ambao wanapenda mageuzi kufanya kampeni kwa bidii.
 
Mwana sheria Tambwe Shitambala wa Jimbo la Mbeya vijijini,kama mambo yatabaki na kwenda hivi hivi yalivyo sasa basi atashinda kwa kura nyingi dhidi ya incumbent Mchungaji Mwanjali
 
Ndg wan JF,
Kulingana na tathimini ya mwenendo mzima wa kampeni za uchaguzi kwa takribani siku 40, wapiga kura wameonyesha dhahiri kuwa CHADEMA itashinda katika majimbo yafuatayo; Hizi sio hisia zangu bali ni hali halisi ya upepo wa kisiasa katika majimbo yafuatayo.

1. Kiteto
2. Karatu
3. Bukombe
4. Iringa mjini
5. Ubungo
6. Kawe
7. Vunjo
8. Kigoma Mjini
9. Kigoma Kaskazini
10. Maswa Mashariki
11. Nyamagana
12. Hai
13. Busanda
14. Mbulu
15. Tarime
16. Arusha Mjini
17. Meatu
18. Ngorongoro
19. Kibaha
20. Singida (jimbo la Tundu Lissu)
21. Bukoba mjini

Ushauri wangu kwa team ya kampeni ya CHADEMA iweke mikakati dhabiti ya kulinda kura katika majimbo haya kwa gharama yoyote maana CCM wanajua hilo na mkizembea sauti ya wananchi itapokonywa na CCM kwa kuiba kura.

Pia Dr. Slaa kama itawezekana apite tena kwa awamu ya pili katika majimbo haya KUKAZIA HUKUMU YA WANANCHI dhidi ya CCM.

Kama kuna watu wamefanya tathimini katika maeneo mengine wanaweza kuongeza katika list hii.

Ningeshauri tutoe tathimini kulingana na hali halisi ya kisiasa katika maeneo husika badala ya ushabiki.

Mbona Handeni hujaweka Kigoda yuko ICU...
 
Nyie jipeni tu moyo na tathimini zenu za kuangali watu wanavyojaa ktk kampeni.
Nakuhakikishieni ccm walisha maliza kazi wakati wa kujiandikisha.
 
Katika hii list ongeza jimbo la msoma mjini. Huyu Mathayo wa CCM ashakubali kushindwa na dogo Nyerere. Alafu dogo anakubalika ile mbaya.
 
Hivi hata Jimbo la Korogwe vijijini mnataka kumwachia mpiga ramli na mchawi? Hawa ndio marafiki wa CCM. ( Waganga wa kienyeji)
 
Zitto asipopita ni sawa tu ili ajue kuwa yeye sio maarufu kuliko chama chake na pia ni vizuri akawa na msimamo. Ameusaliti upinzani. Atakuwa mgeni wa nani?
 
Nimekuwa nikiona kama huyu ameondoka upinzani na bado hajaweza kujionyesha wazi. Ni wa kuangalia.
 
Haya si ndio mambo ambayo Kaimu Mkurugenzi wa Daily News, Nd. Mkumbwa aliandika kuhusu matokeo ya urais akashutumiwa na kila mpenda demokrasia nchini? Hatujafika tarehe 31 October tayari Fanfa anatangaza matokeo ya uchaguzi majimboni. Let us be realistic.

kwani tumefika hiyo 31 hadi huyo mhariri aropoke kuwa dk slaa si rais wa 5 wa tz? Na wewe utumie fikra
 
Haya si ndio mambo ambayo Kaimu Mkurugenzi wa Daily News, Nd. Mkumbwa aliandika kuhusu matokeo ya urais akashutumiwa na kila mpenda demokrasia nchini? Hatujafika tarehe 31 October tayari Fanfa anatangaza matokeo ya uchaguzi majimboni. Let us be realistic.

Afadhali angetabiri majimbo yatakayochukuliwa na CHADEMA baada ya uchaguzi, tungejua anamuunga mkono Sheikh Yahya katika fani.

Yeye anakwambia "Majimbo 21 yatakayochukuliwa na CHADEMA kabla ya oct 31" sasa sijui ana maan majimbo yatachukuliwa kwa process gani ikiwa uchaguzi wenyewe ni Oct 31 na majimbo yatachukuliwa kabla ya Oct 31.
 
jimbo la chalinze,bagamoyo,muheza,handeni, monduli,bagamoyo,lushoto,mwanga, same mashariki&magharibi,chamwino,dodoma mjini,simanjiro,rungwe mashariki&magharibi,kyela aaaaaaahhh jamani mbona yapo mengi mmeshindwa kuyataja?
na hii ni kwa mujibu wa utafiti makini wa SYNOVATE..

CHADEMA HOYYYY........EEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE
hapo kwenye red aisee sijaona upinzani zaidi ya sisiem kwa kweli, bado upinza hauna kasi kama sehemu nyingine wakuu
 
Ndg wan JF,
Kulingana na tathimini ya mwenendo mzima wa kampeni za uchaguzi kwa takribani siku 40, wapiga kura wameonyesha dhahiri kuwa CHADEMA itashinda katika majimbo yafuatayo; Hizi sio hisia zangu bali ni hali halisi ya upepo wa kisiasa katika majimbo yafuatayo.

1. Kiteto
2. Karatu
3. Bukombe
4. Iringa mjini
5. Ubungo
6. Kawe
7. Vunjo
8. Kigoma Mjini
9. Kigoma Kaskazini
10. Maswa Mashariki
11. Nyamagana
12. Hai
13. Busanda
14. Mbulu
15. Tarime
16. Arusha Mjini
17. Meatu
18. Ngorongoro
19. Kibaha
20. Singida (jimbo la Tundu Lissu)
21. Bukoba mjini

Ushauri wangu kwa team ya kampeni ya CHADEMA iweke mikakati dhabiti ya kulinda kura katika majimbo haya kwa gharama yoyote maana CCM wanajua hilo na mkizembea sauti ya wananchi itapokonywa na CCM kwa kuiba kura.

Pia Dr. Slaa kama itawezekana apite tena kwa awamu ya pili katika majimbo haya KUKAZIA HUKUMU YA WANANCHI dhidi ya CCM.

Kama kuna watu wamefanya tathimini katika maeneo mengine wanaweza kuongeza katika list hii.

Ningeshauri tutoe tathimini kulingana na hali halisi ya kisiasa katika maeneo husika badala ya ushabiki.

Haya mambo yanataka basis au vigezo. Labda mimi nikusaidie kuwa basis yako ni kuzomewa kwa wagombea ubunge wa CCM, si ndiyo? Na kushangiliwa wale wa CCM walioenguliwa kwenye kura za maoni!
 
Kweli mkuu hili jimbo kalisahau hali ya CCM kule Mbeya ni ya kukatisha tamaa maana Chadema wanakunywa mpaka uji wa mgonjwa
Niko mlandizi naelekea Mbeya, Riport kamili ya majimbo ya Mbeya mjini,Vijijini,Rungwe Mashariiki,Kyera ntawapa bila kuchakachu! Leo ntakutana na Mr 2!
 
Back
Top Bottom