Majiji ya Tanzania yapangiliwe vyema kimakazi

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
4,491
9,691
Maisha ya kawaida katika majiji yetu, ni yenye kuwakutanisha watu mbalimbali katika shughuli zao za kila siku za kibiashara, kidini, starehe na hata burudani. Shughuli hizo nyingi hufanyika katika makazi ya watu pasipo kujali makwazo, kero na hata athari zenye kuambatana nazo.

Mathalani, katika makazi ya watu tunashuhudia uwepo wa wingi wa nyumba za ibada za madhehebu ya Kikristo ama misikiti pasipo kujali uwepo wa watu wenye imani tofauti. Tatizo linaanzia pale mawaidha yanapotolewa tena kwa nia njema kabisa, ama ikiwa ni ndani ama nje ktk viwanja vya wazi, mara kwa mara tumeshuhudia ujumbe ulikusudiwa kuwajenga wengine kidini, unakuwa ni mwiba na tena ukiwakwaza wengine wenye imani iliyokuwa tofauti.

Aidha, kuna hili kundi la wadau wa kilevi ama huduma za mahaba ya "short time". Nao sehemu za baa na nyumba za kulala wageni zinaonekana zinazidi kuchanganya ktk makazi ya watu. Kutokana kuenea kwa huduma hizi kila kona za majiji yetu, na kila mtu ni shahidi, maumizi yake yapo dhahiri machoni petu wote, hata iwe wakati wa Kwarezima ama Mfungo wa Ramadhani. Kwa kweli zinawakwaza wazazi na viongozi wengi wa kidini.

Mimi nashauri, uwepo mpangilio mzuri wa kutolewa huduma hizi muhimu kwa wadau wake ndani ya makazi ya watu. Pengine nijielekeze zaidi ndani ya hoja ninajyojaribu kuijenga kupitia maeneo hayo mawili. Mathalani, yawepo maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kuendesha shughuli za ibada na kupeana mawaidha ya kidini tu. Mfano ktk hili uwe mpangilio mzuri uliopo ktk madhehebu makubwa ya Kikristo kama vile Wakatoliki na Walutheri.

Kuna hili kundi lingine la huduma za starehe na burudani, ni kweli linachangia kodi nyingi mno serikalini. Lkn pia lina adha na makwazo yake ndani ya makazi ya watu, hasa kwa viongozi wa kidini na wazazi wenye kupenda kusafunda vyema kimaadili watoto wao. Hili lingetengewa "Red Light Streets" zake ili huko kusiwe kabisa na makazi ya watu. Huko mtu anakwenda kupata huduma za vilevi, mahaba, bange, kujidunga madawa bila bughudha yoyote ile ama kubughudhi wanakondoo wasiohitaji kunajisiwa pasipo kuwa na sababu za msingi.

Hapo nimeuza tu wazo, haijalishi litaanza kufanyiwa kazi lini, ama wapi na hata nani afanye nini. Natambua kabisa ktk baadhi ya nchi haya hufanyika na kuzingaitwa, sasa ni vyema wataalamu husika wakaanza kuufanyia kazi ushauri huu.
 
Mipango miji ipo...

Tatizo linakuja pale mtu anapoamua kuuza enea lake, na huyo mnunuzi akapabadilisha tofauti na eneo la makazi...

Mifano ipo, unakuta nyumba inauzwa, ila mnunuzi anavunja na kujenga either, Lodge, frame za biashara, au hata Bar...


Cc: mahondaw
 
Ni kweli kabisa wakuu, uwepo wa mipango mingi mizuri pasipo utekelezaje wake, hiyo nayo ni changamoto nyingine pia. Nategemea jiji jipya la Dodoma, wataalamu wetu watajifunza kupitia makosa yaliyopo ktk majiji mengine. Natamani liwe la mfano wa kuigwa hapa nchini.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom