Majiji 5 kwa Uzuri Tanzania

Hii hapa ni orodha ya Miji mizuri Tanzania.
1-Dar es Salaam (Mzizima)
Eneo la mkoa ni jiji la Dar es Salaam ambalo ndilo kitovu cha shughuli za biashara (na za utawala, kwa kiasi fulani) nchini Tanzania, na ni kati ya majiji yanayokua haraka zaidi duniani.

Ni km² 1,800 pamoja na visiwa vidogo 8 na eneo la bahari kati ya pwani na visiwa hivi. Eneo la nchi kavu pekee ni km² 1,393.

Kuna wilaya tano: Kinondoni (wakazi 1,775,049), Ilala (wakazi 1,220,611) na Temeke (wakazi 1,368,881) ambazo zimeongezewa Kigamboni na Ubungo. Kila moja inaangaliwa kama mji. Takwimu hizi ni za mwaka 2012, kwa ujumla idadi ya wakazi ilikuwa 4,364,541.

Wakazi asili wa eneo la mkoa walikuwa Wazaramo pamoja na makabila madogo kama vile Wandengereko na Wakwere. Kutokana na kukua na kupanuka kwa jiji kuna makabila yote ya Tanzania.

2-Mwanza (Rocky city)
Jiji la Mwanza ni mji nchini Tanzania ambao ni makao makuu ya Mkoa wa Mwanza. Mji upo kando la ziwa Viktoria Nyanza Kulingana na sensa ya mwaka 2002 idadi ya wakazi wake ilihesabiwa kuwa 378,327 (ukijumlisha wakazi wa Wilaya ya Nyamagana na sehemu za Wilaya ya Ilemela).

3-Arusha (A city)
Arusha ni jiji la kaskazini mwa Tanzania na makao makuu ya Mkoa wa Arusha. Kiutawala eneo la jiji la Arusha ni sawa na eneo la Wilaya ya Arusha Mjini. Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 416,442

4-Dodoma (Idodomya)
Ilitangazwa kuwa mji mkuu wa Tanzania mwaka 1973, lakini mnamo tarehe 26 Aprili 2018 katika maadhimisho ya miaka 54 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya tano John Magufuli aliupandisha hadhi na kutangaza rasmi kuwa Dodoma ni Jiji. Serikali ya awamu ya tano ilihamia rasmi jijini Dodoma mwaka 2016.

Jiji hili pia ni makao makuu ya Mkoa wa Dodoma na eneo lake linahesabiwa kama Wilaya ya Dodoma .

Eneo la mji liko mita 1135 juu ya usawa wa bahari UB. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, mji wa Dodoma ulikuwa na wakazi wapatao 410,956 waishio humo.

5-Mbeya (Green city)
Mbeya ni mji wa nne kwa ukubwa nchini Tanzania. Idadi ya wakazi imehesabiwa kuwa 385,279 katika sensa ya mwaka 2012. Wengine 300,000 hivi wanaishi katika mazingira karibu na Mbeya mjini.

Kiasili Mbeya ilikuwa eneo la Wasafwa. Siku hizi sehemu kubwa ya wakazi wanaweza kuwa mchanganyiko wa Wasafwa pamoja na makabila ya Wanyakyusa kutoka wilaya za Rungwe na Kyela, Wanyiha kutoka Mbozi, Wandali kutoka Ileje na Wakinga kutoka Makete.

Tazama zaidi video ya mandhari ya majiji hayo.

Shida ya jiji la mbeya halipendezi katikati ya mjini nyumba zimejengwa Kwa tofali mbichi halafu hazijapigwa plasta. Katika miji mingi niliyotembea Tanzania mbeya ndio jiji pekee tatikati ya mji nyumba zimejengwa Kwa tope
 
Ninachomaanisha,Majiji yenye Bandari za Bahari,Port City,ndio ziwe namba moja.Kwasababu majiji yote yanategemea haya majiji yenye Bandari za Bahari,kukuza uchumi wao,kwa kusafirisha bidhaa na kupokea bidhaa.Kwa mfano mafuta ya magari,yana umuhimu wa kwanza,bila kupitia Bandari za Bahari,ingekuwa shida kubwa,na vile vile kupokea bidhaa na kusafirisha mazao kwenye masoko ya kimataifa ingekuwa tabu.

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
Huyu naye anachekesha kwel na bandari ya tanga dah 😀😀😀
Basi mtwara na lindi zipandishwe hadhi yawe majiji
 
View attachment 1817471

Mbeya City
View attachment 1817472


Mount Loleza - Unaosifia eti kivutio

View attachment 1817474


HIzi ndizo mandhari za Mbeya, nitakuja niwwaambie kwa nini Mbeya patabaki na ujima wake ukipewa Ceremonial Title. Watu wa Mbeya noma sana. Hawataki mawazo ya watu wasiokuwa wa kwao kama vile watu wasio wa Mbeya wanavyopata tabu kuwaongoza hawa watu. Ubishi wa kishamba, ubinafsi na ukablia ndiko mahala pake. Maendeleo yanahitaji kuchanganya fahamu na maarifa. Kaeni na mlima loleza wenu eti ndio kivutio cha jiji. Duh!.
Nilichogundua wewe jamaa una chuki kali sana,kama una uwezo wa kujipima pia una ukabila sana,sasa shida umeanzaje kuwashambulia Mbeya kwa ukabila,huu umeanzishwa kama mjadala tu,lakini maneno ni makali mno kuhusu Mbeya tu,wamekukosea nini mzee,hata vigezo vya mji kupandishwa hadhi huvijui kwa vigezo vyako ni makabila,najua utakuwa povu pole sana
 
Bandari,inaizidi Arusha,Port City,ndio mafuta ya magari na ya mitambo,na Bidhaa kutoka nje,zinashuka hapo Port City.Arusha na majiji yasio na Bandari,lazima yazidiwe na majiji yenye Bandari(Port City).

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
Kwa muktadha huo Tanga imeendelea kuliko Arusha na Dodoma?

Mombasa imeendelea kuliko Nairobi? Japo ni off topic but kuwa tuu na bandari hakukufanyi uendelee automatic
 
Back
Top Bottom