Majibu yangu kwa Baba Askofu Stephen Munga kuhusu Bandiko lenye kichwa cha habari kisemacho "CHADEMA JITAFAKARINI"

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Nimesoma andiko la Baba Askofu Stephen Munga lenye kichwa kisemacho "CHADEMA JITAFAKARINI"

Naomba nijibu binafsi maoni haya ambayo anaiandikia CHADEMA huku yakiandikwa kwa umma wote, mimi kama sehemu ya umma huo nitajibu kwa namna hii niipendayo, izingatiwe majibu yangu sio majibu ya CHADEMA.

Katika andiko lake nimeona kuna hoja kama tano au sita hivi za msingi, na kwakuwa Chadema ni chama cha kisiasa ambacho hujibu hoja bila kuzipiga rungu hoja hizo.

Naomba mimi kama sehemu ya umma hoja zake nizigawanye katika aya sita kama ifuatavyo,

Hoja ya Kwanza ya Askofu Munga:

"Mimi ni miongoni mwa watu waliowaangaliza CHADEMA kuwa waonyeshe na kuurihidhishia umma wa Watanzania kwamba wao ni Chama cha Siasa kinachozingatia misingi ya kidemokrasia. Nilifanya hivyo kwa nia njema japo niliishia matusi. Nilifanya hivyo kwa ajili ya maslahi mapana ya kitaifa na kwa sababu ni mwana taaluma katika masuala ya maadili ya siasa".

Majibu yangu:

Ni kweli Chadema bado ni chama kinachoonyesha na kuridhisha umma wa Watanzania kwamba ni Chama cha Kisiasa kinachozingatia misingi ya kidemokrasia, Hili linadhihirika sio kwa hisia bali kwa vitendo, kwanza ni uwingi wa kitakwimu wa umma unaoiunga mkono Chadema hadi leo hii 27/2/2020 ambapo kwa takwimu za chadema ni msingi Chama kimeshaandikisha wanachama zaidi ya milioni nane na nusu.

Ushahidi wa pili ni takwimu za ushiriki wa chama katika uchaguzi wa serikali za mitaa ambao mchakato wake uliporwa na CCM ambayo Dr Munga umekiri wazi kwamba wewe ni mwanachama wake na unaipenda sana (Rejea hoja ya 6 hapo chini), Mfano: Mwaka 2014 CHADEMA iliweka wagombea mitaa 22 kati ya mitaa 67 ya Wilaya ya Kigamboni, lakini 2019 Chadema iliweka wagombea katika mitaa 64 kati ya 67. Hili ni ongezeko la zaidi ya 97%. Hapo jaza mwenyewe Dr Munga CHADEMA kinaaminiwa na umma au kimepotea?

Katika hoja hii pia umetaja Demokrsia, hii ni propaganda iliyoimbwa na akina polepole na wenzake wengi waliopita katika nafasi hiyo, ninashangaa Daktari msomi wa filosofia kama Munga nawe umeshika beti hizi na kuziima. Ushahidi mmoja ambao umewazima akina Polepole na wenzao ni kwamba CHADEMA kina practice Demokrasia kwa vitendo, mchakato wa kupata viongozi wake umekuwa ukitendeka kidemokrasia, mfano mzuri ni uchaguzi wa mwezi December 2019 ambapo chini ya uangalizi wa msajili wa vyama vya siasa, chama kilitoa nafasi ya kila mwanachama kushiriki uchaguzi kwa ngazi ya chini ta msingi hadi taifa, na kukudhihirishia hilo, nafasi ya mwenyekiti iligombewa na wanachama watatu ambao ni Fredrick Sumaye, Cecil Mwambe na Freeman Mbowe, Hapo ni demokrasia ilitawala, Sumaye lijivua uanachama na kukosa sifa za kugombea, mchuano ukabaki kwa Mwambe na Mbowe, ambapo Mbowe akashinda chini ya jicho la Msajili wa vyama vya siasa na hajawahi kutoa taarifa kuwa hakuna demokrasia bali alipongeza utaratibu mzima wa chama.

Kwa msingi huu hoja yako ya kwanza inakosa mashiko, na inabaki kuwa ni hoja ya hisia zaidi inayokosa weledi kwa mtu wa kaliba yako Daktari Munga, zaidi inaonyesha hasira na hisia zaidi.

Hoja ya Pili ya Dr Munga:

"Kwa kawaida hakuna nchi iwezayo kupiga hatua za kimaendeleo pasipokuwa na siasa pinzani zenye nguvu. Tumepita kipindi cha kina Durkheim za uthibiti wa kiuchumi (economic determinism) na kujidumbukiza katika kipindi cha uthibiti wa kisiasa ( political determinism). Katika uthibiti huo mpya unahitaji ushindani wa kisiasa. Hapo ndipo inapohitatajika kuimarishwa dhana ya utawala wa demokrasia na utawala wa sheria. Utawala wa jinsi hiyo lazima udhihirike katika nyanja zote za miunganiko ya kijamii vikiwema vyama vya kisiasa".

Majibu yangu:

Hoja hii ni nyepesi, Daktari Munga unafahamu vema kwamba Rais Magufuli ambae ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi alivunja katiba na sheria kwa kuzuia shughuli halali za vyama vya siasa, hivyo unaposema hakuna nchi inayoweza kupiga hatua za kimaendeleo bila vyama vya siasa, hoja hii ulitakiwa kuifikisha kwa mwenyekiti wako wa CCM kwamba kubinya vyama vya siasa ni kudidimiza maendeleo ya nchi. Kimsingi hoja hii ni nzuri lakini haina mashiko kwa chama, umeielekeza sehemu batili Daktari Munga.

Hoja ya Tatu ya Dr Munga:

"CHADEMA mlichezea shilingi chooni ikadumbukia. Nawapa nafasi nyingine ya kunitukana. Mlichezea demokrasia na utawala bora wa sheria mkaikanyaga katiba yenu. Tafakarini sana. Sasa mnajifariji kwa maneno matupu yasiyoweza kuwanusuru. Ukweli ni kwamba mmekigonga chombo mwambani (you have rocked the ship). Tafakarini kwa makini juu ya huu uhamaji wa watu wenu".

Majibu yangu;

Unaposema CHADEMA tulichezea shilingi chooni ikadumbukia, ni katika mukdhada upi, kwamba tungesikiliza hoja zako hapo juu na kukushawushi uhamie CHADEMA? Kwamba tungepokea ushauri wako wowote kwakuwa tu wewe ni mtaalamu? Kwamba tulikosea kujitoa uchaguzi serikali za mitaa? Kwamba tulikosea kumpokea Lowassa? Hoja hii inaelea haina mizizi ya hoja imesimama kibinafsi na kiubora mimi zaidi. Hii si hoja inakufa hapa hapa.

Unasema tulichezea Demokrasia na urawala bora tukakanyaga katiba yetu, Huu ni uongo wa mchana ambapo kwa miaka kadhaa umehubiriwa na chama chako CCM bila kuthibitisha, Katiba ya CHADEMA imeandikwa 2006 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2016 na mwaka 2019 muda wote huo hakuna ilipowahi kukanyagwa. Labda ututhibitishie ni kifungu gani kiliwahi kukanyagwa na kwa dhumuni lipi.

Suala la kuhama wanachama kisiasa ni jambo la kawaida na linaweza kutafsirika katika aina kuu mbili, Mosi ni vyama vya siasa kukosa itikadi zinazotambuliwa na kukubakika kwa wanachama wake hali inayopelekea mtu kuhama chama kimoja kwenda kingine bila kuarmthiriwa na itikadi ya chama husika, Pili inaweza kutafsirika kuwa ni kukua kwa demokrasia na uhuru wa mawazo ya wanachama na wafuasi wa vyama kiasi ambacho mwanachama hajioni kubanwa akitaka kuhama chama.

Lakini kwa kesi ya aina ya uhamaji wa wanachama wa upinzani kwenda chamq tawala ni jambo lenye udharimu na ujinai mkubwa, Daktari Munga utakuwa shahidi na shuhuda kuwa Chadema iliwahi kuendesha uchunguzi binafsi kubaini nini kinawasukumu wanachama/viongozi wake kuhama chama, uchunguzi ulifanywa Arumeru na Arusha kwakutumia mitambo ya kamera na kunasa watendaji wa serikali kwa maana ya dola wakiwashaeishi viongozi wa CHADEMA kwa rushwa ya pesa na vyeo ili wahame. Ushahidi huu ulifia mikononi mwa TAKUKURU. Je unaweza kuokoteza sababu zingine nje ya hii iliyofanyiwa utafiti wa kijasusi na kianuwai? Hoja hii ni ya uongo, hivyo imekufa hapa hapa

Hoja ya Nne ya Dr Munga:

"Siasa ni mchezo ulio na sheria zake. Siasa sio uwanaharakati. Siasa ni taaluma inayohitaji umakini ili uvuke bahari salama na kutwaa dola. Uwanaharakati hausaidii katika uwanja wa mchezo wa siasa. Haisaidii kuwatukana na kuwashutumu wale wanaohama toka kwenu. Sikilizeni kwa makini na kutafakari kwa kina. CCM mnayopambana nayo ina magwiji wa siasa. Mimi najua hayo. Si jambo rahisi kupambana na CCM kwa mbinu za uwanaharakati. Wanao wanataaluma wengi wa masuala ya kisiasa ikiwemo propaganda".

Majibu yangu;

Nakubaliana na hoja hii kwa asilimia miamoja, Na kwa msingi huohuo, Chadema kimejihuisha tumebadili aina ya mbinu za kimapambano ambazo tunaingia nazo October, Jambo muhimu Dr Munga himiza Tume Huru ili ushuhudie kwa macho yako ya Nyama Tanzania ikimpata rais aliyechaguliwa na umma sio wa tume ya Rais ya uchaguzi.

Hoja ya Tano ya Dr Munga:

"Nazungumza haya kwa nia njema nikizingatia kwamba ili nchi ipate maendeleo ni lazima iwe utawala uwiano ambapo hakuna chama kimoja cha siasa kinachoweza kujitwalia hati miliki ya kutawala. Hiyo ndio maana nzima ya utawala wa kidemokrasia na utawala wa sheria. Kutaka kuwepo vyama vya siasa vya upinzani haina maana ya kuchukia au kupendelea chama chochote. Uwepo wa vyama vya siasa vya upinzani ni kutaka dhana nzima ya maendeleo katika mazingira ya uthibiti wa kisiasa (political determinism)".

Majibu yangu;

Hoja hii ni sawa na hoja ya pili, Hoja hui imekosea njia, inatakiwa umfikishie Mwenyekiti wako wa CCM kwamba aachane na ule mpango alioutangaza kwamba hadi 2020 ataufuta upinzani nchi, juhudi kadhaa zimejaribiwa kuufuta upinzania lakini amefeli, Chadema imezidi kuimarika zaidi na zaidi kwa mvuto wa sera zake, utikadi yake na wajihi wake.

Hoja ya Sita ya Dr Munga;

"Pamoja na kuipenda CCM bado kwa kuiheshimu katiba ya nchi tungali tunahitaji vyama vya upinzani vyenye nguvu. CHADEMA mlipata fursa hiyo lakini inaelekea mnaidondosha. Badala ya kutukana kaeni chini mjitafakari. Chama chochote cha siasa sio mali ya mtu bali ni mali ya umma. Nimetimiza wajibu wangu kwa Mungu na kwa umma wa Watanzania. Ninawashukuru kwa matusi yote mtakayonitukana.
Mungu ibariki Afrika.
Mungu ibariki Tanzania."

Majibu yangu;

Hoja hii haina mashiko kwasababu kuu kadhaa, moja umekiri wazi kwamba wewe ni mwanaccm ma unaipenda sana ccm, hivyo automatic huwezi kuiombea mema Chadema, Unasema Chadema tulipata fursa hiyo lakini tunaelekea kyidindosha, Zingatia kule juu ulishasema tumepoteza na chombo kimeshagonga mwamba, yaani umeshasahau kauli uliyoitamka wewe mwenyewe hapo juu Daktari?

Sasa ndio unsdhihirisha kwamba ulijaribu kujitegesha kwa chadema kama mshauri ukitaraji Chadema ikuone na kukukumbatia na sasa haijakuona unaaminisha umma wewe ni "fursa" tuliyoidondosha. Kule juu ulizungakazunguka lakini hatimae umegongesha yai kwenye shoka, Jambo la msingi jivue uanachama wako wa ccm, njoo chadems uombe uanachama utakabidhiwa kadi na chama kikiona kuns umuhimu wa kukutumia kitakutumia sawa na maelfu ya wanachama tulionao Tanzania.

Kimsingi naona Mzee wangy Askofu Munga umeamua kutubagaza, umechafukwa kwelikweli umejenga hoja nyingi kwa hisia na hasira zaidi kuliko utafiti yakinifu.

Nikutakie Kwaresma njema mzee wangu, mawazo hayapigwi rungu kama mzee wa Musoga alivyotuasa.

Na Yericko Nyerere
 
Yericko Nyerere,

Umejibu hoja kidhaifu mnoo. Ni bora ungekaa kimya kabisa. Unawezaje kusema Chadema eti imesajili wanachama milioni 8.5 nani anaweza kuthibitisha hili? Eti reference yako ni takwimu za Chadema msingi. Unawezaje kujifanyia tathmini mwenyewe halafu utuaminishe tuamini vile unavyojiona wewe.

Kuhusu Demokrasia ndani ya chama, ulitakiwa kueleza kwanni mbowe anagombea kwa zaidi ya miaka 20 sasa bila kupisha wengine? Kutueleza kwamba aligombea pamoja na kina mwambe bado haimaanishi kwamba Demokrasia ilikuepo. Yaani mbowe yeye ndie anaongoza Kamati kuu ya chama, yeye ndiye aongoze na kupanga uchaguzi wa chama huku akiwa nayeye ni mgombea halafu utegemee eti ashindwe uchaguzi. Hapo aliunda Kamati ndogo mbili moja inahusika na Kamati Kuu na nyingine ilikua ya Uchaguzi na zote zilikua zinaripoti kwake. Unaweza kufafanua hizi Kamati mbowe aliziunda kwasbbu gani? Kama siyo kujiimarisha kwa kutengeneza Mazingira ya kuendelea kukaa madarakani. JITAFAKARINI

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CHADEMA wanapaswa kujitafakari, japokuwa IT'S TOO LATE.

Mazingira ya siasa za Tanzania ni magumu lakini hilo haliwafanya wanachama wa vyama vya upinzani kuwa PERFECTIONISTS.

Tatizo Mbowe amekuwa kama Magufuli, Katengeneza LUNDO LA WATU wa kumnyenyekea na kumwabudu kama mungu.

Mbowe Amepoteza Wanasiasa Wengi Sana Makini Kwasababu Ya MASLAHI YAKE BINAFSI.

Na kibaya zaidi amekuwa akifanya MISIASA ILE ILE YA KIJINGA kama CCM.

Tofauti Yake Na CCM ni Moja tu, HANA DOLA.
 
kipande, Unataka kutuambia kuwa hata serikali inapojifanyia utafiti kuhusu kukua kwa hali ya uchumi nchini na serikali yenyewe kuja kututangazia kuwa uchumi umekua wanatulisha matango pori? Halafu kama chadema ndiyo wanaopita kusajiri wanachama wapya unashindwaje kuamini takwimu zao? Mbona CCM nao huwa wanatuletea takwimu zao? Kumbe wanaleta takwimu za uwongo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninachokiona hakuna tofauti kati ya Chadema na Ccm nahisi utofauti upo kwenye majina tu hakuna demokrasia kwenye hivi vyama vya siasa abadani na haitakuwepo kutokana na kuwa anayeshikilia wadhifa siku zote anapenda kuabudiwa kwenye hivi vyama
 
Sijui naye keshapewa mlungula, maana jiwe anajichotea tu pale kwa mpwa wake na kuzigawa kwa yule atakayekuwa tayari kulamba viatu vyake, ila askofu wangu ulianza vizuri kumbe na wewe unafika bei dah, siamini doctor kama wewe eti ukweli hauoni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa Maaskofu ndio waliomdanganya Lowassa kuwa Sasa Ni Zamu ya Lutheran kutawala. Ndiyo Maana Sumaye na Lowassa waliweza kuwa sehemu moja nadhani karata ya udhehebu ndiyo ilitumika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo pa Mbowe kuendesha Uchaguzi ndio kitu tunachohangaika nacho kwenye tume ya Uchaguzi yaani Magufuli ateue tume halafu upinzani wategemee kushinda?

Sent using Jamii Forums mobile app
Tume huru Zanzibar ilibadili nini? Kenya je? Raila aliisifia tume? Vipi Nyerere alidai tume huru ili kupata uhuru na kushinda uchaguzi?

Matatizo yenu ya ndani ni mazito kuliko hata hayo ya tume! Mnakimbizana na ajenda za kuwafanya muonekane mpo tu ruzuku ziingie!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom